mpatto
JF-Expert Member
- Apr 28, 2017
- 766
- 1,027
Yaani Sheria ya kiasi. Kwamba chochote mtu anachokifanya, basi afanye kwa kiasi cha kumtosha yeye pasi na kuzidisha.
Watanzania, na pengine Waafrika kwa ujumla, jambo hili limetushinda kabisa, na sijui sababu ni ipi, lakini mi huwa nadhani sababu kubwa ni umasikini wetu. Nitatoa mifano ili nieleweke!
#Kuna ofisi fulani wafanya kazi hupata chakula palepale muda wa mchana. Sasa hawagaiwi, yaani hakuna mtu spesheli wa kuwapimia chakula kwenye sahani zao. Yaani watu wale kama sio wafanya kazi aisee, mtu akichelewa kidogo tu, tayari hakuti chakula, na wakati chakula kimepimwa cha kuwatosha wote, yaani wanaokuja wa kwanza, wanachukua to excess mpaka matokeo yake hawakimalizi na wanamwaga kingine. Sio hapo tu, jambo hilo nimeliona sehemu nyingi sana. Khaa!!
#Kuna kiwanda fulani cha saruji, wafanyakazi walikuwa wakipewa maziwa, sasa baadhi ya wafanya kazi wale kumbe huku mitaani walikokuwa wakiishi tayari walikuwa wameshaweka bili. Kwamba akichukuwa maziwa fresh kule kiwandani, basi anakuja kuyauza huku mtaani. Hali hiyo ilifanya watu wawe wana "fight" kule kiwandani ili waweze kupewa maziwa mengi zaidi. Sasa hapo unashangaa, kwamba mbona huyu jamaa anafanya hivyo ili hali analipwa vizuri tu!? Mmmh!!
Mifano ni mingi, lakini nyie wadau mnaonaje!?
Ni kipi ambacho watanzania tunakwama!?
Hali kama hizo wanapoziona wazungu hutucheka sana na kutuona hamnazo!!
Jamani, tubadilike, kama tunahusika na mitindo hiyo!!
Nawasilisha!!
Sent using Jamii Forums mobile app