Watanzania na "Law of Average"

mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Messages
565
Points
1,000
mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2017
565 1,000
Yaani Sheria ya kiasi. Kwamba chochote mtu anachokifanya, basi afanye kwa kiasi cha kumtosha yeye pasi na kuzidisha.

Watanzania, na pengine Waafrika kwa ujumla, jambo hili limetushinda kabisa, na sijui sababu ni ipi, lakini mi huwa nadhani sababu kubwa ni umasikini wetu. Nitatoa mifano ili nieleweke!

#Kuna ofisi flani wafanya kazi hupata chakula palepale muda wa mchana. Sasa hawagaiwi, yaani hakuna mtu spesheli wa kuwapimia chakula kwenye sahani zao. Yaani watu wale kama sio wafanya kazi aisee, mtu akichelewa kidogo tu, tayari hakuti chakula, na wakati chakula kimepimwa cha kuwatosha wote, yaani wanaokuja wa kwanza, wanachukua to excess mpaka matokeo yake hawakimalizi na wanamwaga kingine. Sio hapo tu, jambo hilo nimeliona sehemu nyingi sana. Khaa!!

#Kuna kiwanda flani cha saruji, wafanyakazi walikuwa wakipewa maziwa, sasa baadhi ya wafanya kazi wale kumbe huku mitaani walikokuwa wakiishi tayari walikuwa wameshaweka bili. Kwamba akichukuwa maziwa fresh kule kiwandani, basi anakuja kuyauza huku mtaani. Hali hiyo ilifanya watu wawe wana "fight" kule kiwandani ili waweze kupewa maziwa mengi zaidi. Sasa hapo unashangaa, kwamba mbona huyu jamaa anafanya hivyo ili hali analipwa vizuri tu!? Mmmh!!

Mifano ni mingi, lakini nyie wadau mnaonaje!?
Ninkipi ambacho watanzania tunakwama!?

Hali kama hizo wanapoziona wazungu hutucheka sana na kutuona hamnazo!!

Jamani, tubadilike, kama tunahusika na mitindo hiyo!!

Nawasilisha!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Messages
565
Points
1,000
mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2017
565 1,000
Walikumalizia msosi hao magumbaru, dawa yao siku nyingine uwe unawahi na wewe uwamalizie

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaa!!
Hapana mkuu, wala mimi huwa sibabaiki sana kwenye misosi ya kwenye umma!!

Lakini hiki kitu kipo sana baina yetu waTz na pengine waAfrika kwa ujumla. Na sio swala la msosi tu hata sehemu zingine hali ni hivihivi.

Kuna siku jamaa kwa furaha ya simba kushinda (sikumbuki ni mechi gani), aliamua kutoa ofa ya kreti moja la soda kwa yeyote mwenye hamu. Tazizo sio jinsi wadau walivyogombania kupata, ila shida ni pale, mtu kaisha pata moja, anaificha na kukausha na kutaka kuchukua nyingine kana kwamba hajapata kabisa. Sasa hapo ukiuliza, wewe unywe soda mbili, na wakati kuna mwenzako hajapata, hiyo maana yake nini!?

Ni uchoyo, au umasikini!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S

Shaka-Zulu

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Messages
285
Points
500
S

Shaka-Zulu

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2018
285 500
"There is enough in this world for a man's NEEDS, but not enough for his GREED!" Tamaa ya kujilumbikizia, iwe chakula, maziwa, soda, utajiri, ndiyo inayofanya wengine wakose mahitaji yao! Kama tungejali mahitaji ya wenzetu, sote tungeishi kwa amani!!!
 
mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Messages
565
Points
1,000
mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2017
565 1,000
"There is enough in this world for a man's NEEDS, but not enough for his GREED!" Tamaa ya kujilumbikizia, iwe chakula, maziwa, soda, utajiri, ndiyo inayofanya wengine wakose mahitaji yao! Kama tungejali mahitaji ya wenzetu, sote tungeishi kwa amani!!!
Ni kweli mkuu!!

Lakini mbona mambo haya ni kwetu tu afrika!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S

Shaka-Zulu

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Messages
285
Points
500
S

Shaka-Zulu

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2018
285 500
Ni kweli mkuu!!
Lakini mbona mambo haya ni kwetu tu afrika!?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, tabia hii ipo kwenye jamii zote za kimaskini ( maskini halisi na maskini wa kifkra) duniani kote. Inasababishwa na kutokua na uhakika wa kupata chakula muda ujao. Watu kama hao wakiona chakula cha mchana wanajipakulia ya jioni na ya kesho pia! Watu waliokulia kwenye mazingira magumu wanaishi na hofu ya njaa na fursa ikijitokeza wanachota!!!!! Watu wa aina hii wanakumbwa na Scarcity Mentality - hakuna ya kutosha kwa wote, bora nijilumbikize! Opposite yake ni wale wenye Abundant Mentality - ipo ya kutosha wote, na hata nikikosa leo kesho nitapata!
 
mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Messages
565
Points
1,000
mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2017
565 1,000
Mkuu, tabia hii ipo kwenye jamii zote za kimaskini ( maskini halisi na maskini wa kifkra) duniani kote. Inasababishwa na kutokua na uhakika wa kupata chakula muda ujao. Watu kama hao wakiona chakula cha mchana wanajipakulia ya jioni na ya kesho pia! Watu waliokulia kwenye mazingira magumu wanaishi na hofu ya njaa na fursa ikijitokeza wanachota!!!!! Watu wa aina hii wanakumbwa na Scarcity Mentality - hakuna ya kutosha kwa wote, bora nijilumbikize! Opposite yake ni wale wenye Abundant Mentality - ipo ya kutosha wote, na hata nikikosa leo kesho nitapata!
Umeongea vizuri mkuu Shaka-Zulu.

Asante kwa maoni yako!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dumbi

dumbi

Senior Member
Joined
Jan 15, 2018
Messages
167
Points
250
dumbi

dumbi

Senior Member
Joined Jan 15, 2018
167 250
Mkuu sio kwenye chakula tu hata viongozi wetu ndo wanachofanya ndomana umaskini hauishi chakula wanacho kingi wachache walopewa dhamana.

tatizo lugha
 
GANG MO

GANG MO

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2016
Messages
1,446
Points
2,000
GANG MO

GANG MO

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2016
1,446 2,000
Waafrika wengi tuna spirit ya selfishness ndio maana tunashindwa kuendana na law of average. Mwafrika yeyote akipata kitu anatamani apate zaid ya kile bila hata kujari mwenzie atapatavkiasi gani. Asante kwa post nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Messages
565
Points
1,000
mpatto

mpatto

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2017
565 1,000
Waafrika wengi tuna spirit ya selfishness ndio maana tunashindwa kuendana na law of average. Mwafrika yeyote akipata kitu anatamani apate zaid ya kile bila hata kujari mwenzie atapatavkiasi gani. Asante kwa post nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu, na pengine ni sahihi kabisa kuwa waafrika kiasili tuna sprit ya selfishness!! We angalia jambo hili kwa mfano:

Niliwahi kufanikiwa kuwa mkufunzi katika taasisi flabi ya elimu, sasa ikatokea chaki pamoja na board markers zimeisha!!

Kumbe kuna mmoja alikuwa ameficha box zima la chaki kwenye droo ya meza yake!

Akazitoa na kusema kuwa, basi kila mmoja achukue walau mbilimbili ili kila mmoja apate!! Kilichotokea, watu walichukua nyinginyingi kiasi wengine hawakupata!!

Sasa hapo unaweza ukawaza, inakuwaje mtu hata hana session kwa sasa, lakini kachukua chaki nyingi kwa matumizi ya baadaye, Vipi kama hiyo baadaye zikaletwa zingine!?

Kama mdau mmoja aliposema hapa, tatizo ni umasikini na selfishness!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GANG MO

GANG MO

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2016
Messages
1,446
Points
2,000
GANG MO

GANG MO

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2016
1,446 2,000
Hahahaha nouma sana
Ni kweli mkuu, na pengine ni sahihi kabisa kuwa waafrika kiasili tuna sprit ya selfishness!! We angalia jambo hili kwa mfano:

Niliwahi kufanikiwa kuwa mkufunzi katika taasisi flabi ya elimu, sasa ikatokea chaki pamoja na board markers zimeisha!!

Kumbe kuna mmoja alikuwa ameficha box zima la chaki kwenye droo ya meza yake!

Akazitoa na kusema kuwa, basi kila mmoja achukue walau mbilimbili ili kila mmoja apate!! Kilichotokea, watu walichukua nyinginyingi kiasi wengine hawakupata!!

Sasa hapo unaweza ukawaza, inakuwaje mtu hata hana session kwa sasa, lakini kachukua chaki nyingi kwa matumizi ya baadaye, Vipi kama hiyo baadaye zikaletwa zingine!?

Kama mdau mmoja aliposema hapa, tatizo ni umasikini na selfishness!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,284,193
Members 493,978
Posts 30,816,726
Top