Beberu
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 3,935
- 7,915
Nawasalimu katika jina la jamhuri ya muungano wa Tz (Hata usipojibu mi naendelea tu)
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakati Tv ndo zinapata umaarufu hapa nchini watu walipinga sana hii issue wakisema itatuharibu macho, maadili na pia ni kazi ya shetani
Wakati simu za mkononi zinashika kasi pia watu walisema hii ni kazi ya freemason anataka kutuua waafrica na wachungaji kwa masheikh mbalimbali walijitokeza kukemea waumin kumiliki simu kwa kuwa ni kazi ya shetani leo wote wanamiliki smartphone
Wakati Obama analeta vyandarua watu walisema ule ulikuwa mpango wa kutupunguza nguvu za kiume ili tusizaliane waje wachukue madini yetu watu walikuwa hawataki lalia vyandarua kisa hio na wengine wakavitupa kabisa wakihoji iweje marekani atupe vyandarua bure bure tu? leo wote wanalalia vyandarua sijui kama nguvu za kiume zimepungua au Lah
Wakati smartphone (simu za touch) zinaingia watu walizipinga wakidai zinanyonya damu + habari za ufreemason leo hii sitak kusema how wanatumia smartphone zao kwa burudani.
Wakati internet inapata umaarufu Tz hapa ndo palikuwa kasheshe kwa sababu watu wakatafsiri kuwa INTER ni kuingia na NET ni nyavu ko ukiingia internet jua upo nyavuni na umeshadakwa na freemason ko huwez toka hivo watu wakatumia mikutano na radio zao kuweza kukataza watu kutumia internet
Anyway nina mifano mingi sana jins waTz tunavyopenda kupinga kitu kipya bila kufanyia wala kutafuta maelezo ya kitaalamu
Mtu anasema vyandarua vinapunguza nguvu za kiume unamuuliza unajua dawa inayowekwa kwenye chandarua ni ipi na inafanyaje kazi ? Hajui anabaki kusema wazungu hawatupendi mara freemasons blah blah blah
Naomba niwashauri waTz wenzangu kabla hujatoa maoni kuhusiana na jambo lolote lile bas hakikisha una maarifa na ufahamu sahihi wa hilo jambo leo Gwajima anapinga chanjo ya corona lakini wote mnajua maelezo yake bungen alipotaka kuelezea mRNA zinavyofanya kazi yalikuwa utopolo wa kiwango cha juu kuonesha hakuna anachojua juu ya mRNA lakin anapenda tu kupiga kelele na kuleta umuch know kwenye mambo ya kitaalamu
NB: Tuheshimu taaluma za watu
Imeandikwa na Beberu mweusi