Watanzania na hadithi ya Mtoto wa baba Mlevi

Aug 1, 2020
46
26
Nikiwa ningali mdogo nimeshuhudi jinsi familia (Kaya) ilivyokuwa na ushirikiano wa kutosha. Ni nadra kumkuta mtoto akikubali kukuta Baba, na Mama yake wanasemwa vibaya hata kama wazazi wale ni walevi chakari na wanatia aibu mtaani au kijijini, mtoto hatawasema vibaya wazazi wake badala yake atawakingia kifua ikiwezekana hata kupigana kisa mzazi wake kasemwa vibaya kwa mujibu wake ingawa yasemwayo yote ni kweli.

Juzi, jirani kwetu tuna shule ya kata! Nimekuta watoto wa kiume wanafunzi nje ya jengo moja, wanalofanya bweni kipindi hiki wameweka kambi kujiandaa na mitihani mwisho wa mwaka.

Wanapigana ngumi za kweli kweli mmoja anavuja damu a.k.a (nkune) hiyo ni kikwetu. Nilipowahoji baada ya mimi na rafiki yangu kufanya jitihada ya kuwaamulia wakaniambia mmoja wao alikuja mzazi wake wa kiume BABA bila kufuata taratibu na akiwa amelewa akawa anaongea na mwanae na kabla ya kwisha mazungumzo alitoa dudu yake na kukojoa mbele ya wanafunzi wengine. Likaisha Hilo!

Waliporudi bwenini mmoja wa mashuhuda akawa anawaambia wenzie mzazi wa mwanafunzi X alikuwa anakojoa hapo nje bila haya wala hidaya! Kosa kubwa hili, mwenye mzazi akaja juu kwanini unamdhalilisha BABA yangu?

Nirudi kwenye lengo, kwanini watanzania tunashindwa kuwa kama huyu mtoto wa mzazi mlevi! Yuko tayari kuona MAMA Tanzania anadhalilishwa, anafedheheshwa, anatukanwa, anadharauliwa, anakejeliwa?
 
Back
Top Bottom