Watanzania mwenye YouTube hivi mna akili gani, mbona bado tunazidi kuwa wajinga hadi lini

Masseto

JF-Expert Member
May 14, 2020
1,574
3,071
Huwa napenda nikitazama video YouTube ninasoma na Comments ili kutanua upeo wangu zaidi kwa kuyasoma mawazo ya wachangiaji tofauti tofauti kwenye kipengele cha comment,

NIKITAZAMA CHANNEL ZA NJE HUWA WANACOMMENTS MAMBO SAFI SANA WALE JAMAA NI MAMASTER MIND KWAKWELI, UNAWEZA UKABAKI KWENYE KIPENGELE CHA COMMENTS TU NA UKAELEWA VIDEO INAHUSU NIN

Lakin sisi bhana hakuna lolote linalofanyika kwenye kile kipengele adi wanaboa, utakuta channel ime-upload video ihusuyo maybe siasa, uchumi, historia, tukio au maafa n.k lakin ukija kwenye Comment kupanua wigo wako wa kufikiri na kujua zaidi unakutana na watu wa ajabu kama hawa,

-Leo nimewahi naomba likes zenu.

-sijawahi kupata likes nyingi, leo naombeni likes zenu.

- safiiii,. Vizurii,

IKIWA TUKIO LA KIFO BASI COMMENTS ZOTE ZITATAWALA
R.I.P,,. INALILAHI, APUMZIKE KWA AMANI, ALAZWE MAALI PEMA,

Yaani unaweza ukakuta hata watu 200 hakuna mchango wa maoni unaoeleweka zote upuuzi tu.

Tunakwama wapi au elimu zetu finyu sana kuchangia maoni heri usikomenti basi tunakuwa kama hatuna AKILI
 
Wakati mwingine kukosa cha kusema na kusema tu 'apumzike kwa amani' ni mchango tosha maana kifo huwa kinafikirisha sana. Mfano, mtu unazungumza naye na kuachana salama na kesho yake asubuhi unakuta habari kwamba amefariki (kwa ajali, pressure, moyo, kisukari etc). Itakuchukua muda kuamini hivyo.

Mimi nilishawahi kumpeleka wife wangu kwa kwanza hospitali kwa ajili ya kujifungua. Vipimo vya clinic vilionyesha yuko vizuri: mtoto ameshageuka, damu ni ya kutosha (hakuna sababu ya kuongezewa damu) na hadi naambiwa hospitali 'tumeshampokea na hapa haturuhusu mtu kubaki njoo kamjulie kesho asubuhi' tuliagana vizuri...Asubuhi alikuwa mzima, ila alidai hajapata huduma yoyote na alikuwa akisikia maumivu tumboni.

Mimi na watu tuliombatana nao tulijitahidi kumjulia hali mchana na hatukufanikiwa. Kwenye saa 9 nikaitwa mimi na kuambiwa 'pole sana, mkeo kaaga dunia asubuhi saa 3'. Sikuamini na nili'faint' kwa muda. Nilipopata fahamu nilijikuta nimelazwa wodini napungiwa upepo! Kifo ni kitu kingine kabisa!
 
Sasa ukiingia 'fesibuku' na kuanza kusoma hizo comment si ndo utazimia kabisa na ukija kuzinduka 'sonona' hii hapa!
 
Wakati mwingine kukosa cha kusema na kusema tu 'apumzike kwa amani' ni mchango tosha maana kifo huwa kinafikirisha sana. Mfano, mtu unazungumza naye na kuachana salama na kesho yake asubuhi unakuta habari kwamba amefariki (kwa ajali, pressure, moyo, kisukari etc). Itakuchukua muda kuamini hivyo...
Pole sana bro, lakin apa nimelenga hasa mfano vifo vya viongozi hasa vioo vya jamii. Kila Comment unayokutana nayo ni R.I.P tofauti na wenzeti wamagharibi Comments zako zinafikirisha sana. Sijui ndio tuseme vichwa vyao vinajua mengi maana wanakoment adi jins tukio lilivyokuwa, njoo bongo ni inalilah tuuuuuuu
 
Lakini hata wao wanaandika upuuzi sana ni kwa vile huwa hatutilii manani comment zao
Hapana bro wamagharibi wengi ni maClever sana kwenye Comments, ukute ni asilimia ndogo sana ndio uandika ujinga, ukitazama ata ktk uzinduzi wao kiteknolojia Comments uwa zinadadavua mambo mengi sana tena kiutaalamu. Sisi tunaomba likes
 
Leo nimewahi naomba likes zenu.

-sijawahi kupata likes nyingi, leo naombeni likes zenu.

- safiiii,. Vizurii,

IKIWA TUKIO LA KIFO BASI COMMENTS ZOTE ZITATAWALA
R.I.P,,. INALILAHI, APUMZIKE KWA AMANI, ALAZWE MAALI PEMA,

Bundle na MB zinasumbua, watu hawatazami video kwa kuwa pesa hakuna wanategemea kusoma comments huku hawajui kuwa wamepotezwa aidha na mashabiki wa team AliKiba au Team Lumumba wafia chama wenye kusifu, kutukuza.

Na hivyo ndiyo serikali ya CCM inataka watu wasipate habari sahihi na hivi pia waTanzania lugha ya Kigeni haipandi basi tumeishia kutazama misiba na habari za maisha ya macelebrity wa mtaani kwetu.
 
40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom