Watanzania mteremko mpaka lini? Ilianza kwa Miss Tz alipoenda Miss World na sasa kwa Diamond na Kiba

youngdonats18

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
685
443
Hii kitu nimeanza kuwaza toka usiku na nimeamka asubuh moja kwa moja mpaka JF celebrities forum kutoa mapovu yangu kwa watz ama wabongo.

Huu uzi unatokana na tabia ya wabongo kuamini ktk mtelemko katika kushiriki na kushinda matuzo makubwa kama Miss World na BET na mengineyo.

Kipindi Miss Tanzania, alipokuwa kwenye mashindano ya Miss World watu wakaanza kusema eti ingia kwny page ya Miss World Instagram then tafuta picha ya Miss Tanzania yaani Diana Mmasai ike, share na comment neno TANZANIA na ikawa ni likes nyingi kuliko hata followers wake kumuwezesha kushinda lkn mwisho wa cku akaangukia pua hata top 50 hakuwepo, hizi iman za kijinga sijui zimetoka wapi aisee, so sad kwa watanzania!

Na hivi juzi tu kabla ya waandaaji wa tuzo za BET kutoa majina ya washiriki wa tuzo mbalimbali kwny kipengele cha Best International Act in Africa waliuliza fans wachague wanaomtaka wao, asee fans wa Diamond walifurika comment laki ngap cjui zote mara kwa mara [HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG].

Ali Kiba haya ndio imekuaje sasa hakuna cha Diamond wala Kiba kwenye hicho kipengele waliofanya vizuri tumewaona wamechaguliwa kuwania hiyo tuzo.

Maoni: Ifikie hatua watanzania tuamini katika kufanya kazi nzuri ili tufike mbali na sio kufikir kulike na kucomment ndio kushinda.

Mhariri: DONATUS JULIUS ANDREW(Youngdonats18)
 
Ukweli mchungu,halafu wakati mwingine wabongo wanatoa aibu kwenye page za watu , mfano Davido katangaza kuwepo kipengele flan cha BET na anawaomba mafans wake wamsupport basi hapo viluilui wa Diamond wamejaaaa wanacomment balaa Diamond ndo anafaa diamond ndo anafaa utadhani Davido ndo BET..

Hawajaishia hapo wakaenda hadi kwa Wizkid ambaye alipoona wanazingua na ushamba wao kaamua kuzima comments kwenye post zake...


Watanzania tubadilike, na mpenda Diamond na Kiba ila mashabiki wa diamond mmezidi wengine hata mada hawazielewi zimeandikwa kiingerez wao wanaandik tu diamond....

Jamani tunaonekana vitukoooo huko nchi za nje .

Tukubali tu kwasasa tuzo yoyote ambayo msanii wetu kawekwa na Wizkid hatuwezi shinda hata tukeshe uchi tuna vote maana wizkid kwasas sio level ya Africa tena , wewe ukitamba na Marry you sijui Aje remix mwenzio ana DADIYO na COME CLOSER
 
upo sawa
ila kumbuka ni ishu hizo hizo za wabongo zilinfanya Kiba amny'anye tuzo Wizkid
some times inasaidia
 
Back
Top Bottom