Watanzania msipopaza sauti juu ya walimu na madaktari mbele ni kiza na maafa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania msipopaza sauti juu ya walimu na madaktari mbele ni kiza na maafa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkisumuno, Aug 2, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nchi ya Tanzania imefika pabaya, kwani sasa hakuna kufuata sheria, maana kama walimu tumefuata sheria lakini hukumu ndiyo hii. Sawa tutaenda shuleni na kuendelea na mgomo barafu na hapo ndo kitaeleweka kuwa punda hawezi kulazimishwa kunywa maji.

  Nimeamini watawala wanaajenda ya siri kutaka wawarithishe madaraka watoto wao kwani Watoto wa watanzania hawatapata elimu sitahiki. Na uthibitisho wa mgomo mkubwa ni jinsi walimu walivyoonyesha msimamo, hivyo tegemeeni hali mbaya sana kielimu. Asasi, mashirika ya dini na jamii nzima pazeni sauti juu ya udikiteta wa Rais kikwete, Mahakama na polisi vinginevyo Tanzania ya watu mbumbu zaidi inakuja.

  Hata huyo jaji aliyepindisha sheria kwa ajili ya kujipendekeza atajibia siku moja uovu huo. Kikwete kuwa Rais isiwe tiketi ya kuwanyanyasa watanzania. Muogope Mungu. Hiv hujiulizi kwamba ukiondoka utakumbukwa kwa lipi. Kikwete hafai kwa ustawi wa Taifa letu. Nimeamini kweli alichakachua ndiyo maana ya matatizo hayo yote.

  Watanzania tutubu makosa yetu kwa mwenyezi mungu atusamehe, maana maandiko yanasema Hata uongozi mbaya hutoka kwa Mungu ili kuwakomesha watenda mabaya. Tutafakari tumekosea wapi hata kustahili kuongozwa na mtu huyo asiyefikiri hata athari ya maamuzi yake.

  Mahakama ama kweli zimepoteza mwelekeo. Tunachopaswa sasa ni kuchukua uamuzi wowote kwani Mahakama ni chombo binafsi cha Kikwete.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Wewe wa wapi?
   
 3. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mahakama gani, hakuna mahakama kama muhimili siku hizi, ila kuna CCMahakama, utashinda wapi?
   
 4. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukichagua CCM mbele ni kiza na maafa.
   
 5. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapana kikwete ni chagua la Mungu Mungu anatufundisha jambo hapo
   
 6. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Ni kweli watz sasa tuache ushabiki wa kisiasa na tuangalie hali halisi ya ustawi wa taifa letu hasa kwenye elimu. Serikali na mahakama vinafanya mzaha kwenye hili. Ni kweli serikali imeshinda na kusherejekea kishabiki...viongozi wa serikali walioshinda kesi hawasomeshi watoto wao kwenye shule hizo halafu wananchi wasiofikiri wanashabikia jambo hili. Watz amkeni kwa haraka mumpinge Kikwete na mahakama ili kuponya taifa letu
   
 7. damper

  damper JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Una chuki zako tu wewe hilo giza utaliona wewe na familia yako ya kichawi.
  Vimaneno maneno utafikiri........
  Kwani lazima uwe mwalimu!! Jaribu sasa huo mgomo barafu uone kilichomzuia ng'ombe kuwa na ndevu.
  Unajaribu kutaka kuungwa mkono na watanzania kwa hoja dhaifu, utafikiri hii ni nchi ya wafanyakazi pekee. ukweli ndo huo serikali haiwezi kulipa mshahara uliopanda kwa asilimia 100 tena elimu pekee!!!!!!!!!!
  Hata kama hali sio nzuri sana kwa waalimu lakini UKWELI huwezi linganisha hiyo hali ya mwalimu wa leo na miaka kumi iliyopita. Hii awamu ya Kikwete itapita lakini si ajabu wewe huyo huyo ukaja tena hapa na kuumpa sifa tele kwamba nafuu na utawala wake.
   
 8. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Rais na serikali dhaifu wanaitumia mahakama kama kichaka cha kujificha mahakama umekuwa ndioo mzee tusitegemee jipya kwenye kesi za wananchi dhidi ya serikali dhaifu
   
 9. d

  dada jane JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu damper nahic ni mmoja ya washauri wa ikulu. Mnamkosea sana Kikwete na watanzania kwa ujumla.
   
 10. Mangimeli

  Mangimeli JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Damper,,una akili sana,uyu jamaa wa wapi uyu??aelewi ata anachoongea!!
   
 11. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Walimu fikirini kwa mapana. Hao mnaokataa kuwafundisha ndo watoto wenu, mnaowagomea watoto wao hawasomi kayumba. Tenda wema nenda zako, haki haiibwi kama ipo labda itacheleweshwa tu. Jengeni Tz yetu jamani. Tatizo linakuja huko bungeni ambako tunaambiwa keki ndogo yet waheshimiwa wanavuta mil 11, wengine hata ngazi ya ualimu hawakuifikia. Du!
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  taahila mzoefu
   
 13. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ushabiki bwana, wewe siyo mwalimu ndiyo maana unaongea kwa jeuri kubwa kiasi hicho. Sawa, ukisema kama hatuwezi ualimu tuache, upo sahihi pia, lakini kumbuka athari kubwa zitapatikana kwa watoto wa masikini kama sisi, lakini siku zote MTU HUFANYA KITU AMBACHO KINAMPA FAIDA ZAIDI, nawashauri waalimu, tutafute kitu ambacho kitatupa faida zaidi, anagawa siyo wote, lakini wengi tufanye kazi tuachane na hii profession ya KIPUUZI.
   
Loading...