Watanzania msiogope, shilingi haishuki thamani kwa mtindo huu

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Watanzania wenzangu habarini,

Nachukua nafasi hii kwa kutaka kujaribu kwa ufupi kueleza ki nadharia na ki uhalisia kile ambacho kimetokea kwa siku mbili tatu zilizopita kuhusu thamani ya fedha yetu dhidi ya dola.

Ili reportiwa na inaendelea ku reportiwa na baadhi ya vyombo na mitandao ya ki fedha mikubwa ulimwenguni kuwa thamani ya dola moja ya marekani imefikia shilingi 2500 kutoka bei iliyokuwepo awali ya kati ya Shilingi 2250.

Mwenyewe nilivoona habar hii japo ni ya kutisha ila haikunistua maana moja kwa moja nilijua ni kitu kisichowezekana. Kulingana na kwamba huwa nazifuatilia hizi rate kutoka website ya BOT na ki ukweli na kila mtu lazima aelewe.. Thamani ya dolla dhidi ya shilingi yetu japo inaangalia forces za Demand and Supply ila pia BOT wapo macho sana ku regulate rate in case kunakuwa na shortage kubwa ya Dolla ama wingi mkubwa wa dolla kwa kuuza ama kununua.

Kwa hiyo nataka tuelewane kwamba mfumo tulionao sio floating exchange rate system kwa maana kuna wakati intercention zinafanyika.

Ila haimaanishi pia kwamba rate haiwez kufika 2500 inaweza hata kufika 3000 endapo kutakuwa na upungufu mkubwa wa dolla dhidi ya mahitaji yaliyopo kiasi kwamba mpaka BOT wenyewe wakashindwa kufanya intervention na kuamua kuachia soko liende kwenye hizo rate za 2500 ama hata 3000 hakuna immunity kwenye hilo.

Ila kwa kwa kilichotokea mwisho wa wiki iliyopita ghafla bin vuu unaona $ imehit 2500, hakuna kitu kama hicho na hakiwezekani kitu kama hicho.

(mwishoni kidogo naweza kugusia conspiracy theory juu ya kilichotokea wiki iliyopita)

Kwa wale ma banker wanao deal na haya masuala ya kubadilisha fedha, kuna kitu tunakiita order flow,, yaani ili useme umeuza dola kwa sh 2500 ama hata 2400 ama 2300 ni lazima uonyeshe volume.

Mimi naweza kusema ama ku quote Dolla kwa kuiuza 2500, akaja mtu asiyejua akanunua $ 10 kwa sh 2500, ki nadharia unaweza kusema $ 1 ni shilingi 2500 ila ki uhalisia hai make sense volume ya $10 ikufanye useme sasa shillingi imeporomoka thamani. Huo ni ujinga.

Ila akitokea mtu akanunua $ millioni 900 kwa shillingi 2500 hapo tutaweza kusema by 95% shillingi yetu imeporomoka thamani kweli maana hata volume inakuambia wazi kabisa..

Sidhani kama naeleweka maana nna ka usingizi hapa ika naamini mtakuwa mmeelewa kidogo kwamba, kama shillingi kuporomoka sio kitu kama mvua ya ghafla inanyesha tu, ni kitu kinaanza kuonekana tangu mbali na chimbuko lake huwa soko la ndani la fedha na sio hivo vyombo kama Bloomberg mnavovihofia nyie.



Issue nyingine ni nataka kugusia ni kwamba hii issue ki conspiracy theory imenifanya nimfikirie bwana mmoja anaitwa George Soros na kwa kiasi fulani nimeogopa.

Huyu jamaa ni Hedge Fund manager na billionaire mkubwa ambaye ni mwanzilishi wa taasisi fulani inaitwa 'OPEN SOCIETY ORG'

Hi taasisi msingi wake mkubwa ni kupigania Demokrasia ulimwenguni, na inasemekana huyu jamaa amekuwa aki destabilize sana nchi ambazo zinapinga Demokrasia kwa mbinu kama hizi za kuangusha thamani ya fedha ya nchi.

Anashutumiwa sana na nchi za Asia kwa michezo aliyoicheza, ni mtu hatari mno huyu na ni mtu mwenye mtandao mkubwa sana.

Tukio la juzi lililofanywa na Bloomberg bado linanifikirisha sana, wale watu usidhani kama wamekosea makusudi. Kwa kutizama Historia ya Dunia mi bado nna imani 96% huenda kuna mipango ipo njiani ni hii ni moja ya majaribio yao.

Ukisoma nadharia ya soko inatosha kukuambia kwamba kitendo cha juzi kingeweza kuwatisha investors na public ambapo wangehisi kweli shilingi inapoteza thamani na kama wote wange act rationally ina maana notionally demand ya $ tayar ingezidi supply na rate lazima ingeshoot.

Na kwa mazingira kama hayo kungeweza kutokea some scenarios ikazidi ku shoot maradufu..



** WALICHOFANYA BLOOMBERG NI KITENDO CHA HATARI MNOO, NI KITENDO CHA UHUJUMU UCHUMI WA LEVEL YA JUU KABISA**

Sijui kama kwenye usalama wa taifa kuna kitengo cha kumulika hizi haya mambo ama labda BOT walivoandika barua yao ndo imetosha.

Ila ushauri wa mwisho kabisa kwa serikali, hili jambo lisiachwe likapita hivi hivi lifuatiliwe..

Mikono ya watu kama kina George Soros ni mikono mirefu mno na ni genge la watu wenye akili mno.. Hapa intelligence itumike vinginevo naona yale ya Zimbabwe yanatufika na hatutajua nini kimeenda vibaya..
 
Nimeamua kutojibu hii makala yako baada ya kukumbuka kuna nafasi 9 za uDC ziko wazi na leo zimeongezeka 2 za ukurugenzi, hivyo jumla imekuwa 11. Kukujibu accordingly ni kujichosha tu, akili yako haijatulia labda hadi pale hizo nafasi zitakapojazwa!
 
Siku zote tatizo la nchi za Kiafrika ni kiongozi mwenye madaraka ya Mungu. Kiongozi asiyejua elimu ya uchumi, lakini wanataka waongoze sera za uchumi!
Si siri kwamba hivi karibuni kumekuwa na maamuzi mengi ya kuteteresha uchumi. Sizungumzii madini, Dangote nk ambayo yameleta woga mkubwa... bali pia kufuatwa fuatwa kwa matajiri ambao ndio waajiri wakuu, kupandisha kiholela VAT, kuzuia sukari bila ya kwanza kujua kuna uwezo gani....matamshi ya kutojali juu ya wanafunzi wa kike, Wasenge ...(Hata kama nakubaliana na baadhi ya hoja, ila ya nini kupiga kelele na kujitoa kifua mbele?). Kwa ujinga wao hawajui kabisa kuwa siku hizi kutokana na utandawazi, habari kama hizi zitaumiza uchumi. Kama ambavyo shambulio la kigaidi lingeteteresha uchumi, mambo kama haya pia. Lakini, Alas! Tuna viongozi wanaodhani bado tuko miaka ya 70 na kwamba Mtanzania likitokea lolote ni rahisi kwake kurudi kijijini kujilia mhogo wake chini ya mti!
Utake usitake, uchumi wa Tanzania uisha ingia katika mfungamano na uchumi wa dunia: unaweza kuathiri na kuathiriwa. Usishangae kuwa hata benki kuu ya Tanzania KAMWE haimilikiwi na serikali ya Tanzania, fungu kubwa! Hivyo sishangai kwa kuporomoka huku kukubwa kwa Shilingi.. Na kila anayesema hii ni ' a passing cloud' anaota!
Katika nchi zinazojua uongozi, na kutambua athari ya jambo kama hili, ungesikia Waziri wa Fedha au Mkuu wa Benki Kuu...na hata Waziri Mkuu....wamejiuzulu. Hizo zinaitwa nchi za "waliostaarabika".
Yawezekana pia ni hawa wacheza currency wanataka kuiadhibu Tanzania kwa kuwabana Wazungu wenzao....yawezekana sana. Na ndiyo maana ukiwa kiongozi lazima uwe na busara na ujue "world order' inakwendaje. Si kwamba usifanye maamuzi yako, ila unayafanya kwa akili zaidi. Hii kulifanyia "uvuvuzele" suala la Acacia kwa kutaka kiki za kisiasa kwa kweli ni upumbavu, na haya ndiyo matokeo. Ingewezekana kabisa, kwa kutuliza vichwa na kutumia akili, kufikia matokeo hayo hayo.
Nasikitika kwamba watakaoumia zaidi na mshuko huu mkubwa wa shilingi.....guess..... ni maskini wasio hatia walioponzwa na viongozi wao!
 
Nimeamua kutojibu hii makala yako baada ya kukumbuka kuna nafasi 9 za uDC ziko wazi na leo zimeongezeka 2 za ukurugenzi, hivyo jumla imekuwa 11. Kukujibu accordingly ni kujichosha tu, akili yako haijatulia labda hadi pale hizo nafasi zitakapojazwa!
We utakuwa unawashwawashwa si bure
 
Back
Top Bottom