Watanzania msilale Jamani!!!

BabaH

JF-Expert Member
Jan 25, 2008
704
225
Jamani mimi sielewi
Inakuwaje kweli pamoja na kupiga kote kelele za ufisadi lakini bado watanzania wanaendelea kulala, Ni juzi tu BOT kumepotea pesa kibao ambazo zingewasaidia watanzania, Ebu angalia hii
Juzi FISADI mkuu KIKWETE alikuwa Bukoba katika Ziara zake zisizo kuwa na maana yoyote, ameenda anawatembeaa watoto yatima na maskin wasio kuwa na hata pesa ya kula, na kuendeleza slogani zake za ndoto(Ari pya, kasi mpya na Nguvu mpya)
Chakusikitisha ni kwamba wakati anatoa hizo kauli zake, watanzania hata hawakumbuki kama kuna pesa zetu zimeliwa huko BOT na yeye ni muhusika mkuu kabisa, ila wanaendelea kumshangilia na kumtukuza tu.Hakuna hata mtanzania aliyejaribu kuulizia hayo mambo,..
Haya leo tunaambiwa matumizi ya mawaziri kwenda kuinadi Bajeti 2007/2008, Huu ni upumbavu kabisa na naomba Selikali ijui **** 80% ya viongozi hawatumii akili kabisa, Bajeti inanadiwa jamani???? . Na nini kazi ya wabunge, kwanini unamtuma waziri kama sio njia za kupoteza pesa za wananchi wanaolipa kodi.

Nawaombeni watanzania wenzangu, hii tabia ya kununuliwa kwa kupewa vijitishite vya CCM na kanga, haitatufikisha mahali popote
Tunatoa kura zetu kwa shilingi mia tano, kijitishite , vikofia, kanga na kupigiwa taarabu za TOT, sasa angalia tunapoteza pesa kiasi gani na kusababisha Mama zetu wanakufa mahospitalini kwa kukosa Dawa, watoto wanakosa malezi na Elimu bora.
Kwanini tunashindwa kuelewa mambo madogo tu, ukimpa kura mtu anayekununua, fikilia mara mbili, yeye anapigana kukupa wewe pesa bure ili aingie madarakani, lakini akishaingia atarudisha hizo pesa zake, atazirudisha vipi?? UFISADI.
Tujiandae jamani kupinga ujinga huu jamani, ni mwaka wa tatu sasa huku hakuna cha Ari mpya kasi mpya wala nguvu mpya, ila mambo yanazidi kuwa mabaya.
Ebuu amkeni jamani tupigane jamani, la sivyo tutafika mahali pabaya
amkeni amkeni jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,862
1,250
Ulikuwa wapi ? Ukipata nafasi ya kuuliza uliza lakini jamaa huwa hayuko makini atacheka na kukueleza kwamba ameagiza kazi ifanyike .Now leo wanapitisha sheria ya kuchunguza na kukamata tu pale pakiwa na ushahidi. Wategemea nini ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom