Watanzania mnamshauri nini Rais wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania mnamshauri nini Rais wetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Domo Kaya, Oct 29, 2008.

 1. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania mnamshauri nini Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete???????? Maana mwezi huu tu maandamano kibao
  1. Waalimu - Maandamano
  2.Wahariri - Maandamano
  3.Wazee - Maandamano

  Tumshaurini afanye nini maana kila kukicha matatizo yanaongezeka, NAULI BEI JUU, MAISHA MAGUMU, AJIRA HAKUNA -BADALA YA AJIRA MILION MOJA ZIMEPUNGUA MILION MOJA, WAMACHINGA KILA SIKU WANAKIMBIZANA NA MGAMBO. KILA KITU KIPO JUU, KILICHOBAKI NI KULIPIA HEWA TUNAYOVUTA.

  1.Je Ajiuzuru
  2.Je Akimbie nchi (Apotee)
  3.Je Asigombee term ya pili
  4. Au oungozi unaomzunguka ni mbovu?
  AU AFANYAJE??????????
   
 2. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa jinsi mambo yanavo kwenda namshauri awanunulie viongozi wote HELMETS za kujikinga na mawe.
   
 3. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #3
  Oct 29, 2008
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo Yeye mwenyewe ni mbovu na tatizo kubwa zaidi ni kuwa wasaidizi wake aliowachagua wengi ni wabovu karibu kila eneo sababu vigezo alivyotumia kuwaweka ni tu kama ni wana mtandao au washikaji waliomsaidia kwenye kampeni au watoto au ndugu wa washikaji au aliwahi fanya nao kazi zamani hivyo hafuatilii watu hao kama bado wachapa kazi au la.

  Wasaidizi wake Wengine wameamua kuwa wabovu baada ya kuona kuwa na yeye si mtu serious wakaamua nao kutokuwa serious.

  Wasaidizi wake wengine hawako serious sababu wanamjua udhaifu wake kutoka A-Z hivyo hawaogopi wanasema akitugusa tunamwanika.Hivyo naye anawaogopa.Sasa kama anawaogopa kwa nini aliwachagua.Cheo humpi mtu kwa kuwa unamwogopa unampa kwa kuwa ni mchapa kazi.

  Cha kufanya abadilike utendaji wake.Muda mwingi atulie ofisini afanye kazi.

  Watu wanasema nchi haijapata Raisi bado ina waziri wa mambo ya nchi za nje kutokana na anavyosafiri nje ya nchi.

  Wengine hadi wanasingizia kuwa hataki kutulia ofisini sababu ni mshirikina kwa kuwa waganga wamemwambia Ikulu hapafai kukaa kuna mashetani mabaya kwake kwa hiyo ndiyo maana anakwepa ofisi. Akitoka safari za nje ya nchi anahamia kutembelea mikoani ili mradi asiweko ofisini kwa woga wa kishirikina.

  Anachotakiwa kufanya angalau kwa sasa kwa kuanzia kama atapenda nitataja machache:

  1.Abadilike utendaji wake na wa walio chini yake ili arudishe imani ya wananchi kwake.

  2.Atulie nchini na ofisini kwake Ikulu afanye kazi aache kuruka ruka.Aliomba kazi ofisini Ikulu ni vizuri awepo ofisini.

  3.Atafute wasaidizi wazuri wajuao kazi kila eneo hata kama hawapendi na si washkaji au wanamtandao iko haja ya kufanya mabadiliko makubwa katika serikali yake kwa wasaidizi wake inabidi apange upya safu zake za uongozi

  4.Awe na maamuzi kwenye masuala mazito yeye mwenyewe.watu wamechoka na hizo tume zake zisizoisha nchi inaendeshwa na Raisi siyo na tume.Watu wanasema nchi sasa hivi haiendeshwi na Raisi bali tume ndizo zinaongoza nchi.

  5.Wakati wote azingatie katiba katika utendaji wake.Kitu kama hakipo katika katiba ya sasa ambayo haijabadilika asithubutu kukivalia njuga.Mfano mambo ya Kadhi na OIC aachane nayo.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,195
  Trophy Points: 280
  Ainusuru nchi yetu na janga kubwa lililo usoni. Ajiuzulu ili tumpate kiongozi jasiri asiyemuogopa mtu na ambaye siku zote ataweka mbele maslahi ya Tazania na Watanzania badala ya mtu mwingine yeyote yule.
   
 5. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kivuko nacho leo kimekorofisha.
   
 6. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2008
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Kudai haki ni uhuru na madai ya hawa watu yameanza zamani sana. Kumlaumu Kikwete kwa haya si vyema na kwa mawazo yangu haya matatizo ni ya muda mrefu sana.
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nashauri kuwe na utaratibu wa 'daftari la mahudhurio' pale ikulu ambalo sisi waajiri wa Rais tunaweza kulikagua bila usumbufu wala bughudha ili tujue kwa mwezi mwajiriwa wetu kafanya kazi siku ngapi ofisini.
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  akumbushwe kuwa uraisi si urahisi!
  Akaze buti.
   
 9. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani Rais haelewi kuwa kuna matatizo kwa kuwa hana muda wa kukaa Tanzania na kufahamu hali halisi.

  Pia amejizungushia makerubi ambao kwa muda mchache wa takriban masaa 2 labda kwa wiki ambapo wanampa briefing za yote yaliyotokea Tanzania pale anaporejea kutoka kuvinjari hawampi ukweli.

  La kumshauri kubwa, akae nyumbani apitie yote aliyoanza nayo wakati anatembelea mawaziri wake na kuwapa majukumu, atathmini kuwa walifanikiwa kiasi gani, na pia arejee kwenye makabrasha yake aone aliyowaahidi wananchi na zimefanikiwa kwa kiasi gani.

  Mkiweza kumshauri afanye haya, mbona hamtawasikia tena kina chiligati.
   
 10. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani,haya ndio madhara ya serikali au chama kushinda uchaguzi kutokana na nyota ya mtu mmoja.
  Kuna uwezekano mkubwa kwamba JK ni mtu safi,ila wanao mzunguka ndio waliotufikisha hapa,baada ya kuona jamaa ana influence kubwa na ana-support ya wananchi (mwanzoni mwa utawala wake) wakaamua kumgeuka.

  Siku zote,nchi yoyote Rais au waziri ni figure/stuture kazzote zinafanywa na washauri na makatibu wakuu kwani ndio watendaji wao ni ku-sign miswada na uwakilishaji wa nafasi zao au kufanya marekebisho madogo madogo kwenye speech.

  Nani asiye jua kua kwamba nchi hii haijawai kuwa na uongozi mbovu kama wa awamu ya nne ya Uncle Ben? Lakini look, watu wa Usalama wa Taifa walifanya kazi kubwa ya kuficha yote mabaya kwani Mkapa alikua ana support ya ndani serikalini na hata kichama ndio maana Mangura alikaa pale CCM kwa miaka 10 yote ya Ben ,just to say the least.

  Kwahiyo nadhani,tunapotaka kumshauri huyu bwana mkubwa lazima tuangalie nini hasa tuzungumzacho,any ways kila mtu ana uhuru wa maoni haya ni ya wangu.

  Kila bin damu ana makosa yake,kama ilivyokua kwa Julius,Mwinyi,Mkapa na hata sasa JK (naomba mnielewe si semi kwamba the guy is Perfect) ila watu walikua tayari kufukia mashimo.sasa hivi Jk akionekana Kona JF utaona habari muda huo huo au kwenye mitandao ya simu au watu watafukuavisima vya kale.
  Na kila mtu atasema anajua hapa,ila ongea kuhusu wqaliopita mpaka leo watu wamejawa na kasumbu wanatetea.

  Namaliza kwa kusema embu,tuangalie hawa watendaji wetu kina nani hasa na wanafanya nini maofisini mwao,na je wanatimiza wajibu wao na si kila kitu kukilaumu kwa Raisi.
  Ila Rais nae afanye mpango wa KUWALIPA HAO WAZEE WA EAST AFRICA COMMMUNITY KWA KUTUMIA PESA ZA EPA BADALA YA KUNUNULIA MBOLEA(hiyo mbolea yenyewe enaweza isifike watu wakpiga bao VIJISENT)
   
 11. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2008
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ushauri wangu kwa Jk ni mdogo sana::

  Mr. Presida look @ your people's plight and try to better the life of Tanzanians through common sense approach.
   
 12. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Moelex,

  Mi naungana na wewe moja kwa moja Jk kwa ku-prove watu wrong angeamua kufanya mambo moja kwa moja badala ya kufata procedures,akaamua kua Dictator of some sort mpaka nuda wake uishe na kwa kipinde hicho at least ajitahidi kulipa wananchi walio muaamini na kumpa ushindi wa kishindo vinginevyo hao jamaa zake hawata lest mpaka wamuone anaondoshwa kwenye madaraka kwa nguvu ya umma au hata kwa nguvu za ziada kama walivyo aanza kwa hii social un-rest kidogo kidogo mpaka kutakua hakukaliki tena hapa
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Oct 29, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,112
  Trophy Points: 280
  Sanda Matuta,

  ..Kikwete hana uwezo na hafai.

  ..mtasingizia sana kuwa tatizo ni wasaidizi.

  ..Civil Service ni ileile iliyofanya kazi na Mkapa. sasa mbona huyu mkwere anapwaya?

  ..hata hotuba za kila mwezi amekimbia hatoi tena.

  ..majukumu ya Uraisi hayaendani na mtu anayependa starehe na mizaha.
   
 14. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Mkulu Joka Kuu,

  Kama utasoma vizuri bandiko langu,sipo mbali na maneno yako ila sehemu moja tu,hii, "
  ..Civil Service ni ileile iliyofanya kazi na Mkapa. sasa mbona huyu mkwere anapwaya?"

  Ambayo wewe mwenye unaji-contradict,Ikiwa civil servant ni walele nini kinashindikana wasifanye kazi zao kama wakati ule wa Ben?
  Hii ndio inaletelea ile fact kwamba,kuna watu wamemgeuka humo humo chamani au serikalini kwa kutumia hizo influence walizonazo kwa maslai yao ili as you have put it,Mkwele aonekane hafai.

  Hivi,kuna asiyekua anajua kwamba Uncle Ben ni mtu wa mtungi mpaka anasinzia mahara,mtungi unaenda na mambo yake wote tunaya jua hizi nazo si ni starehe?
  Eti,mizaha uliza waliokua na Ben pale Sayansi na tekinologia(Jamuhuri street)watakuambia Ben ni waina ipi hana tofauti na Mkwele.

  Alafu,by the way,kumwita huyo JK kwa jina la kabila lake na jinsi ulivyo litumia in your sentence,i for one kama mtu wa pwani i felt offended naona ile dhana ya watu wa mwambao hawezi kitu bado unayo.
  Na nadhani nastahili samahani kutoka kwako.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hebu niulize: Hivi anashaurika?
   
 16. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Jasusi,

  kwa kweli hapana jua.

  it more like tunajishauri wenyewe na kusoma posts zetu wenyewe,haina uhakika kama Jk anapata hata nafasi kuingia humu barazani.
  Si unasikia kila siku yuko angani ankula nchi,na juzi tu nimesoma hapa sijui Laptop yake imepotea.....!
   
 17. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Naona ni vyema akubali kushindwa na arudi chalinze kulima mananasi. Halitakuwa jambo la aibu bali litakuwa ni jambo la busara na heshima kubwa kwake na kwa Taifa.
   
 18. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wazo la yeye kuachia ngazi ajiuzulu au apotee yote sawa. Huyu mtu tatizo kubwa ni yeye mwenyewe halafu hayo mengine ni madogo. Jk hana presidencial power. Hana internal force inayoweza kumfanya atoa maamuzi au kutenda chochote.

  Tatizo kubwa JK hajui tatizo ni nini? kwa mtaji huo hakuna analoweza kufanya kafa huku akiwa anatembea.
  Wananchi waendelee kupiga misafara yote ya serikali mawe kuonyesha kuwa hakuna serikali wala utawala.
  Kikwete ajiuzulu kuokoa taifa.
   
 19. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Namshauri ACHAPISHE NOTI MPYA na aweke sura yake halafu yeye ajiuzuru coz kama ni kutaka ionekane na yeye alishawahi kuwa Rais tutakuwa tunakumbuka noti hizo.
   
 20. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani kwa hali ilivyo sasa hivi Rais wetu atakuwa anajifungia ndani na kulia mpk anachoka then akitoka nnje anatabasamu, maana matatizo yanayomuandama hawezi kuwa haimuumizi, Juzi juzi tu kazomewa mbeya, mara msafara wake umepigwa mawe, mara waalimu wameandamana na kumpiga Rais wao, mara Wahariri wameandamana, na siku inayofuata mazee wameandamana, kuhu Pantoni limenasa kwenye mchanga, na huko Mbagala Daraja limeenda na maji.

  Kwa hayo tu jamaa lazima atakuwa amechanganyikiwa.
   
Loading...