Watanzania mmefanya makosakuchagua serikali ambayo ndiyo chama tawala pia

Mbunge

Senior Member
Aug 7, 2008
104
10
Watanzania sio tu wabunge ambao ndio wawakilishi mliowachagua wenyewe kwa huba na mapenzi yenu sio tu wanaamini kuwa wana haki ya kuwa na mishahara, marupurupu na posho kubwa kubwa, bali pia kwa kukataa kwao bungeni kuzungumzia masuala ya kufa au kupona kwa upande wenu kutokana na mgomo wa madaktari wamewapa ushahidi tosha kwamba WABUNGE WENU HAWAJALI KAMA MNAUMWA, MNA DHIKI, MNA MATATIZO AU MNAKUFA, kwani wana mambo muhimu na makubwa zaidi ya kujadili na siyo vifo au matatizo ya wale wanaowawakilisha.Kosa lenu ambalo mnafaa mjicheke wenyewe ni lile la kuirudisha CCM kwa zaidi ya asilimia 88 ya viti, hii ikiwa ina maana kwamba kwa hali yoyote ile ilivyo hapa nchini-SERIKALI ndiyo BUNGE, na BUNGE ndiyo SERIKALI.Wapinzani hata wakiwa wazuri na wenye uchungu na wagonjwa na wale wanaokufa mahospitalini hawawezi kufanya lolote kwani idadi mliyowachagua kwenda bungeni ni kama asilimia 10 tu ya wabunge.Hadi hapa ninaamini wenye kuona na kusikia, na wenye akili wamejifunza kitu muhimu. Na walio werevu na wajanja zaidi watachukua muda huu kujua kwamba, na hasa kina mama, kwamba.... ukipokea kanga au fulana au vitenge vya CCM au kula pilau ya CCM siku moja itakuja kukutokea puani utakapokwenda hospitali kujifungua, lakini daktari kagoma na BUNGE la CCM ambalo ndio SERIKALI pia haliwezi kujidhibiti achilia mbali kulifuta kazi, maana limegandamana kama kupe kwenye ngozi ya ng'ombe.Wagonjwa wote poleni. Mnaokufa wafungueni wengine macho, kwamba kama nyie leo, basi wao kesho.mbunge njaakali,Hatuwezi kuwasaidia bila nyie wenyewe kujisaidia kwanza kwa kuchagua wabunge wanaofaa zaidi kuingia bungeni na sio wale wanaowapa rushwa mkaipokea na kisha kuwachagua!
 
Back
Top Bottom