Watanzania mlio nje ya nchi amkeni (Tanzanians in Diaspora Arise)

John Mnyika

Verified User
Joined
Jun 16, 2006
Messages
715
Likes
23
Points
0
Age
37

John Mnyika

Verified User
Joined Jun 16, 2006
715 23 0

Watanzania mlio nje ya nchi amkeni (Tanzanians in Diaspora Arise): Wakati Tanzania Bara (wakati huo ikiitwa Tanganyika) ikiwa katika harakati za kudai uhuru; tunasimuliwa na wazee wetu, vijana wa wakati huo kwamba palikuwa na mchango mkubwa sana wa watanzania waliokwenda kupigana vita nje ya mipaka ya nchi yetu. Hawa waliwaelewa vizuri wakoloni wa wakati huo kuanzia udhaifu wao na hata mbinu za kuwakabili; na kwa ujumla walijifunza kwamba nchi kupata uhuru inawezekana.

Ni hakika kwamba wakati taifa letu linapoendelea kukabiliwa na changamoto za maadui ujinga, umasikini na maradhi huku ukoloni mamboleo ukiweka mirija katika rasilimali na maliasili; tunahitaji mabadiliko ya kweli yenye kuleta uhuru wa kweli.

Katika mazingira haya, kama ilivyokuwa wakati wa kuundoa ukoloni mkongwe, mchango wa watanzania mlio nje ya nchi (Diaspora) ni wa muhimu sana.

Watanzania nyie mnaelewa matunda ya mabadiliko katika kukabiliana na changamoto za ujinga, umasikini na maradhi na mbinu za kidemokrasia za kufikia mabadiliko hayo. Katika kukabiliana na ukoloni mamboleo, watanzania mlio nje ya nchi mnafahamu udhaifu wa mabeberu hivyo mnauwezo wa kusimama kidete kuunganisha nguvu kujenga taifa lenye uwajibikaji na kutoa fursa kwa watanzania wengine walio wengi.

Kwa sasa mchango mkubwa wa watanzania mlio nje ya nchi umekuwa katika kuleta rasilimali kwa wenzenu walio nyumbani (remittances); kwa wachache uwekezaji na wengine kutoa uzoefu wao wa kitaalamu.

Tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; ni wakati wa Diaspora kuchukua hatua kama ilivyokuwa wakati wa kudai uhuru ili kuweke madarakani uongozi wenye dira, uadilifu na uwezo kuifikisha Tanzania katika kipeo cha demokrasia, maendeleo na ustawi wa watu wake. Mnaweza kufanya hivyo kwa wengine kujitokeza kugombea lakini wengi kuunga mkono harakati za mabadiliko kwa njia mbalimbali; kwa kutoa mawazo, kuchangia rasilimali na kupiga kura.

Naotoa ujumbe huu wakati huu Taifa likiwa katika mjadala wa sheria mbili muhimu zenye taathira katika uchaguzi ambazo watanzania mlio nje ya nchi mnapaswa kuzitazama kama kikwazo kwenu na kutoa maoni ya kuzibadili ili ziwe fursa kwenu kuwezesha mabadiliko kupitia uchaguzi.

Mosi; muswada wa marekebisho ya sheria za uchaguzi; huu umekwepa kuweka mabadiliko ya msingi ya kuwezesha uchaguzi kuwa huru na haki ikiwemo kutokuwepo mfumo huru wa usimamizi wa uchaguzi kama wadau walivyohitaji. Lakini kwenu mlio nje ya nchi, muswada huu haujaingiza ombi lenu la muda mrefu la kutaka mruhusiwe kupiga kura. Inashangaza kwamba nchi masikini kama Msumbiji, na nchi iliyotoka vitani karibuni kama Rwanda; raia wake wanawekewa utaratibu wa kupewa haki ya kupiga kura kupitia balozi zao katika nchi mbalimbali, Tanzania inashindwa kuweka kifungu hiki katika marekebisho ya sheria na hivyo kuendelea kunyima haki hii muhimu ya kikatiba kwa watanzania walio nje ya nchi.

Pili; Muswada wa Fedha za Uchaguzi wa mwaka 2010; huu pamoja na kuweka vifungu kuminya wagombea kuchangisha fedha za uchaguzi ndani ya nchi, na kutoa mianya ya wagombea kufutwa bila kupewa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa. Umelenga pia kudhibiti hata fedha za watanzania walio nje ya nchi kuchangia uchaguzi. Kama sheria hii itapita, watanzania mlio nje ya nchi, hamtaweza kuchangia vyama ama wagombea kwenye kampeni ya uchaguzi hata kama ni michango midogo midogo ya kuwezesha mabadiliko. Katika mazingira haya, uchaguzi wa mwaka 2010; mchango wenu utakuwa ni upi? Maana nyie ni raia halali, lakini hamtakuwa na haki ya kupiga kura wala hamtakuwa na haki hata ya kuchangia wagombea iwe ni fedha au rasilimali nyingine yoyote ile kwa chama ama kwa wagombea.

Amkeni sasa, wekeni msimamo wa kuwezesha taifa kuwa na sheria itayolinda uhuru wa nchi na kuweka uwanja sawa wa ushindani wa kisiasa wakati huo huo ikawawezesha kupata haki zenu za kikatiba muweze kutimiza wajibu wenu wa kidemokrasia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Ukimaliza kusoma ujumbe huu; tafadhali mtumie na mwenzako. Wako katika demokrasia na maendeleo: John Mnyika, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa (CHADEMA); tuwasiliane- 0754694553, mnyika@yahoo.com au mnyika@chadema.or.tz.

Chanzo: http://mnyika.blogspot.com/2010/01/watanzania-mlio-nje-ya-nchi-amkeni.html
 
Kiby

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2009
Messages
5,436
Likes
1,253
Points
280

Kiby

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2009
5,436 1,253 280
Ni kweli tunahitaji demokrasia ya kweli ni nia ya dhati ya mabadiliko kuelekea maendeleo ya kumkwamua raia na hasa zaidi katika nchi zinazoendelea nyingi zikiwa Africa Tanzania ni mojawapo. Tumeshuhudia pia usiri uliopo katika mikataba ya wale wanaoitwa wawekezaji na jinsi ilivyogubikwa na tofauti kubwa ya hata asilimia 3 kwa 97. Mnyika pamoja na kukujulisha kwamba tunauitikia wito wako positively, hebu tumbukiza huo muswada wa fedha za uchaguzi hapa jamvini ili tuweza kuufanyia tathmini baada ya kuupitia kipengele kimoja kimoja.
 
MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
35,816
Likes
132
Points
160

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
35,816 132 160
Mkuu,

Kuna mambo mengi sana ya kuangalia, na moja wapo ni jinsi Serikali ya CCM inavyo endesha nchi kwa kuto mjali kabisa mwananchi ambaye ndio chanzo kikuu cha utawala.

Kama ulivyosema kuhusu absentee votes/ballot: wananchi walio nje nafikiri wana haki kabisa ya kupiga kura. Lakini sijuwi ni kwanini Bunge letu na/au Wabunge wetu wameshindwa kuwa na veto clause ya kulishinikiza bunge kupitisha mada inayo mhusu raia wake aliye nje ya nchi kupiga kura.

Maswala ya fedha za uchaguzi, mimi nafikiri wabunge wana haki kabisa ya kuchangisha fedha. Kama bunge linataka kupisha mswada ambao utamyima haki mbunge ya kuchangisha fedha, basi nafikiri sasa umefika wakati wa wabunge wa upinzani kuwa wamoja na kuwa na veto clause against proposed mswada, na kuelewa kuwa Serikali ya CCM haimjali mwananchi kabisa zaidi ya matumbo yao.

In several occations, nimekutana na vizingiti vingi sana, ninapokuwa nafanya certain transaction na nchi yetu. Rushwa imekuwa mbele kila sehemu na hasa kwenye maofisi yote ya serikali. Hapo utakubaliana nami kwamba, ni vigumu sana kujenga nchi yenye mfumo unao tetea na kukumbatia rushwa na yenye viongozi wasio jali mwananchi. In more than one occation, nilitumia rafiki yangu mwenye rangi nyeupe waipendayo, na wakati wote nilipo tumia mtu mweupe, mambo yangu yanaenda vema na kwa urahisi.

Zaidi ya hapo, Serikali yetu imekuwa ikiendeshwa kama familia ya mtu, na Baba wa hiyo familia amekuwa akifanya apendavyo ilimradi afuraishe roho yake na wana familia yake.

Mungu ibariki Tanzania
 
Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
8,755
Likes
5,146
Points
280

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
8,755 5,146 280
Mkuu Max Shimba, heshima mbele.

Je unafikiri ni kwanini CCM imeanzisha matawi nje ya Afrika tena Ulaya na sio labda mlemle Afrika?

Nafikiri hapo wana maana yao au wewe unaonaje?
 
Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,571
Likes
1,934
Points
280

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,571 1,934 280
Huwezi kuamua kupigana vita na jeshi unalojua fika limekuzidi nguvu na maarifa bila kuwa na maandalizi. Mchango wa watanzania kwa sasa utakuwa na manufaa kama utaenda katika kuleta mapinduzi ya kweli katika elimu, na mambo mengine ya kimaendeleo.
Nionavyo mimi kwa sasa bado hakuna chama mbadala cha kuitoa nishai CCM.Vyama vya upinzani vinahitaji kujua umuhimu wa kujipanga vizuri na kutumia muda wao mwingi kujijenga especially maeneo ya vijijini.Pia vyama vya upinzani vitambue kwamba migogoro isiyokwisha inatupa shaka kama wao wakipewa dhamana ya kuongoza hawatafanya madudu kuliko haya tunayoyaona maana migogoro mingi imegubikwa na element za ubinafsi kuliko hoja za kweli za maendeleo
 
MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
35,816
Likes
132
Points
160

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
35,816 132 160
Mkuu Max Shimba, heshima mbele.

Je unafikiri ni kwanini CCM imeanzisha matawi nje ya Afrika tena Ulaya na sio labda mlemle Afrika?

Nafikiri hapo wana maana yao au wewe unaonaje?
CCM inafanya utafiti. Inaangalia ni Wananchi wangapi walio nje ya Tanzania wanaipenda, wakisha maliza utafiti wao, watakuwa mbele kupigia ndogo ndogo ruhusa ya Utaifa wa Nchi Mbili na kupiga kura za absentee ballots/votes.

Joined
Nov 5, 2009
Messages
73
Likes
1
Points
0

Mende dume

Member
Joined Nov 5, 2009
73 1 0

Amkeni sasa, wekeni msimamo wa kuwezesha taifa kuwa na sheria itayolinda uhuru wa nchi na kuweka uwanja sawa wa ushindani wa kisiasa wakati huo huo ikawawezesha kupata haki zenu za kikatiba muweze kutimiza wajibu wenu wa kidemokrasia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Ukimaliza kusoma ujumbe huu; tafadhali mtumie na mwenzako. Wako katika demokrasia na maendeleo: John Mnyika, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa (CHADEMA); tuwasiliane- 0754694553, mnyika@yahoo.com au mnyika@chadema.or.tz.

Chanzo: http://mnyika.blogspot.com/2010/01/watanzania-mlio-nje-ya-nchi-amkeni.html
I just like the effort you guys are making to reform the country. My observation to political dynamics in bongo! people want change fast and forever! But again the same people operate via the principle of IF YOU CANT BEAT THEM JOIN, this principle gives CCM an upper hand. Every enterprenuer is up for connection and networking, the network every one is aiming at is the network in power- the real mtandao. thanx GOD we know have some one carelessly running the current mtandao, to an extent that some people in the system are left out leading to MWANGA MBOGA TUMWAGE UGALI approach in every corner and more so in a bunge. previously we saw strong MPs being co-opted in the government. Not any more under this mtandao, where no matter how vocal u r if u r not part of the mtandao forget it! That is why you see people ready push the party to the corner.

Mnyika, if the opposition parties will sit down look at your philosophy consolidate your potentials, you can make it. I wish something happens (too late for 2010 elections) that one political party is formed where all opposition parties will defuse into, as opposed to forming coalition, and this party be led by the emerging politicians forget tha LIPUMBAs, MBOWE, MREMA, MBATIA, etc have these as back benchers to activate the political drive. redefine the philosophy, say something that every body will feel the change and believe in it.

as we stand now, people at least me we are confused, we dont know who to trust. We are all against clinging to power but that is what we see in all parties be it rulers or opposition! Ndo maana watu wanakadi kama line za simu, tigo, voda, zain, etc, tigo anatumia mchana, zantel for intenet, zaini akiwa mkoani, voda usiku akichombeza! Hatufiki.

vyama tunavipenda lakini hakuna tofauti ya falsafa! haiwekani republican akaenda Democrat na akawa kiongozi kama alivyo kuwa republican, no possible imani ya republican haendani nao, ni kama vile shekhe akiasi uislam hawezi dk ile ile akawa mchungaji pentekost- and vice versa, imani yao sio ya kuvua kama gagulo, afu unavaa jingine.
believe me you, people are tired they want a system that works, they want kids to go school, our mothers/ wives to get health care. we are not poor, we got gold, diamond and so much. so strange that we measure our shiling against dollar and we forget that the dollar is measured against our GOLD! sijui tumelaaniwa na nani sijui. why dont we tie our shiling to the GOLD, badala ya kuwaachia Barick wavune kama shamba la bibi?

jengeni vyema, unyesheni njia, people will join you, achen hivo vituko vya ajabu mara kiongozi kasema hivi mara yule kamsemea nani. have principles kama hakuna anayefaa katika nafasi, iachen wazi kuliko kuweka mtu afu mnatuambia hana maadili ya uongozi.

given the situation now, kila mtumish anayefikia ngazi za kuonekana katika jamii hawezi kubak non-partisan, that the reality atapswa aonyeshe kwa vitendo kuwa ni mwana CCM! hiyo tutake tusitake, lakini with strong political parties that can take power in alternating manner, hali ita-change.

SORRY GUYS I WISH I COULD MAKE IT SHORTER!
 
Jaman Diaspora are nothing but a social construction. is just a global trend. tunawataalam wetu ndani hatuja watumia vilivyo, hawa wanje watatufaa sana ukisha tumia kilakitu cha ndani, na tukajua nini mapungufu yetu tuongewe humu mlimo pungua. tuangalie hili wazo la diaspora linatoka wapi na asili yake nini?

hapo tunaweza kuona tunajenga jamii nyingine ya irresponsible non patriotic citizens. Kuna identity ya kila binadamu kuna kila mtu na root yake. ndo maana US wanaile kitu wanaita afro-americans, asian-amerikan, etc etc, being a tanzanian is your identity, if at one time you choose to throw away ur id, is fine but it should not be our role to finght it back for you, fight it urself. you had a choice is permanent resisdence if u wanted.

at time i feel the need to have every body responsible for their did. sio uende bongo unapiga kura unamweka kikwete ofisini afu unatoka mbio unaenda Nigeria unapiga kura uweka mwingine ofisin, afu wewe unaanza kuyumba kati, huku mmoto unarudi huku. NO put down ur ASS face ur concequence, unless upo kwa utafuataji tafuta ukiamua kubaki huko baki ukiona una unchungu na nchi yako japo inamafisadi rudi kwenu.
 
Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
7,930
Likes
134
Points
160

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
7,930 134 160
Mkuu Max Shimba, heshima mbele.

Je unafikiri ni kwanini CCM imeanzisha matawi nje ya Afrika tena Ulaya na sio labda mlemle Afrika?

Nafikiri hapo wana maana yao au wewe unaonaje?

cha ajabu wana support matawi ya chama chao nje ya nchi lakini hawa support watanzania waliokuwa nje ya nchi kupiga kura. na hapo naweza ku-quote maneno yako tena "nafikiri hapo wana maana yao".

ccm ni chama cha ajabu sana na wanachoniudhi mimi kikubwa ni lack of goals.kama chama chao kingekuwa na malengo tungefika mbali lakini kwa vile hawana malengo ndio maana unakuta mpaka leo zaidi ya miaka 40 ya uongozi wao bado vitu vidogo kama maji na umeme big deal na vya tabu.watu wanaangalia zaidi ya mafuta sisi ndio kwanza maji tu yanatushinda kutoka bombani.
 
BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
80,459
Likes
117,190
Points
280

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
80,459 117,190 280
cha ajabu wana support matawi ya chama chao nje ya nchi lakini hawa support watanzania waliokuwa nje ya nchi kupiga kura. na hapo naweza ku-quote maneno yako tena "nafikiri hapo wana maana yao".

ccm ni chama cha ajabu sana na wanachoniudhi mimi kikubwa ni lack of goals.kama chama chao kingekuwa na malengo tungefika mbali lakini kwa vile hawana malengo ndio maana unakuta mpaka leo zaidi ya miaka 40 ya uongozi wao bado vitu vidogo kama maji na umeme big deal na vya tabu.watu wanaangalia zaidi ya mafuta sisi ndio kwanza maji tu yanatushinda kutoka bombani.

Huu ndiyo undumilakuwili wa CCM na Serikali. Wanapokuwa nje ya nchi hutaka sana kukutana na Watanzania wanaoishi katika nchi hizo lakini hapo hapo wako mstari wa mbele katika kuminya haki za Watanzania hao katika kupiga kura na pia kuruhusu uDC angalau Watanzania waliozaliwa Tanzania na baadaye kuhamia nchi za nje na kuchukua uraia wa nchi nyingine wasipoteze Utanzania wao.

Unadhani lile tawi la CCM UK likichanga pound 10,000 na kutoa kama mchango wao katika uchaguzi wa 2010, CCM watazikataa!? Watazichukua kimya kimya na wakati huo huo kuwa mstari wa mbele kuendelea kuvizuia vyama vingine visifaidike na michango toka nje ya nchi.
 
Mbunge wa CCM

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2009
Messages
476
Likes
1
Points
0

Mbunge wa CCM

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2009
476 1 0
Watanzania mlio nje ya nchi amkeni (Tanzanians in Diaspora Arise): Wakati Tanzania Bara (wakati huo ikiitwa Tanganyika) ikiwa katika harakati za kudai uhuru; tunasimuliwa na wazee wetu, vijana wa wakati huo kwamba palikuwa na mchango mkubwa sana wa watanzania waliokwenda kupigana vita nje ya mipaka ya nchi yetu. Hawa waliwaelewa vizuri wakoloni wa wakati huo kuanzia udhaifu wao na hata mbinu za kuwakabili; na kwa ujumla walijifunza kwamba nchi kupata uhuru inawezekana.

Ni hakika kwamba wakati taifa letu linapoendelea kukabiliwa na changamoto za maadui ujinga, umasikini na maradhi huku ukoloni mamboleo ukiweka mirija katika rasilimali na maliasili; tunahitaji mabadiliko ya kweli yenye kuleta uhuru wa kweli.

Katika mazingira haya, kama ilivyokuwa wakati wa kuundoa ukoloni mkongwe, mchango wa watanzania mlio nje ya nchi (Diaspora) ni wa muhimu sana.

Watanzania nyie mnaelewa matunda ya mabadiliko katika kukabiliana na changamoto za ujinga, umasikini na maradhi na mbinu za kidemokrasia za kufikia mabadiliko hayo. Katika kukabiliana na ukoloni mamboleo, watanzania mlio nje ya nchi mnafahamu udhaifu wa mabeberu hivyo mnauwezo wa kusimama kidete kuunganisha nguvu kujenga taifa lenye uwajibikaji na kutoa fursa kwa watanzania wengine walio wengi.

.........................................................................
ndugu yangu mnyika, siku hizi hakuna kitu kinaitwa "watanzania waishio nje ya nchi" ama diaspora.

siku izi mtu akiishi nje ya nchi anabaki mtanzania kwa passport yake tu, laini matendo yake yote anakuwa raia wa nchi hizo za ng'ambo. wao walichoamka na wanachoshinikiza kwa sasa ni uraia wa nchi zaidi ya moja kuwarahisishia kuishi huko nje na sio kwarahishia kuishi tz.

wao hawahangaiki kuleta maisha bora tz bali huhangaika kusaka maisha bora kokote yanakopatikana utadhani yalinyesha kama mvua huko.

ukiwaambia wasimamame majukwaani, watasema wanawaachia watu kama mnyika na mgombea ubunge wagange njaa zao, na wakiona kitu hakiendi vizuri ndio wa kwanza kukosoa na kuapa kuwa hawatarudi hadi watz wabadilike.

masikini hawajui kuwa nao ni sehemumuhimu ya mabadiliko. ndio wale tulioambiwa kuwa siku zote hujiuliza tz itawafanyia nini warudi nyumbani badala ya kujiuliza wataifanyia na wanifanyia nini tz

ni hayo tu kamanda

tuko pamoja
 
Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
4,470
Likes
30
Points
135

Nyambala

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
4,470 30 135

Mkuu una uhakika na hizi allegations zako? Mbona mambo jumla jumla tu vp????????
 
M-Joka

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2007
Messages
308
Likes
4
Points
0

M-Joka

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2007
308 4 0
ndugu yangu mnyika, siku hizi hakuna kitu kinaitwa "watanzania waishio nje ya nchi" ama diaspora.

Siku izi mtu akiishi nje ya nchi anabaki mtanzania kwa passport yake tu, lakini matendo yake yote anakuwa raia wa nchi hizo za ng'ambo. Wao walichoamka na wanachoshinikiza kwa sasa ni uraia wa nchi zaidi ya moja kuwarahisishia kuishi huko nje na sio kwarahishia kuishi tz.

wao hawahangaiki kuleta maisha bora tz bali huhangaika kusaka maisha bora kokote yanakopatikana utadhani yalinyesha kama mvua huko.

ukiwaambia wasimamame majukwaani, watasema wanawaachia watu kama mnyika na mgombea ubunge wagange njaa zao, na wakiona kitu hakiendi vizuri ndio wa kwanza kukosoa na kuapa kuwa hawatarudi hadi watz wabadilike.

masikini hawajui kuwa nao ni sehemumuhimu ya mabadiliko. ndio wale tulioambiwa kuwa siku zote hujiuliza tz itawafanyia nini warudi nyumbani badala ya kujiuliza wataifanyia na wanifanyia nini tz

ni hayo tu kamanda

tuko pamoja
Vipi matendo yake huwa ya raia wa nchi hizo??? Kwa taarifa yako watu ninaowajua mimi wote ambao WAMENUNUA URAI WA NCHI NYENGINE wamefanya hivyo katika mazingira yafuatayo:

1. KUBIDI (NECESSITY): Watu huondoka TZ kwa sababu ,hali na njia tofauti tofauti. Baada ya mtu kuishi katika nchi hizo huzoea maisha na shughuli zao na familia zao pale kwa wakati ule wanapoendesha maisha yao. Kumbuka kwamba katika nchi nyingi zilizoendelea taratibu za maisha na haki za mwananchi ziko wazi na unaweza ku-achieve kwa kiasi cha uwezo Mungu aliokujaalia. Yapo baadhi ya mambo kwa mfano elimu ya juu, mikopo, baadhi ya kazi, nk huwezi kupata isipokuwa uwe raia wa nchi hizo. Na vilevile kuupata huo uraia, hapa natumia neno kununua huo uraia wa nchi hizo taratibu zake ni rahisi, wazi na zenye faida. Kwanini katika hali hii mtu asinunue na ilihali ya kuwa kuna maongezeko juu ya uTanzania wake ambao Mwenyezi Mungu tayaaaari ameshamjaalia kiuzawa kuwa nao.

Nataka ufahamu kwamba walio wengi, karibu wote wanaofanya hivyo hufanya hivyo bila ya mapenzi na hisia zao kuhusu nchi yetu TZ kupungua hata tone moja. Liyie vizuuuri akilini mwako hili, isitoshe badala yake mapenzi na hisia zo kwa nchi yao huongezeka maradufu kwa kujua kwamba wameongeza kitu (elimu, experience, nk) ambacho mahesabu ya faida za kitu kile yote huyaelekeza na kuyakusudia watakaporudi nayo makwao (TZ). Weka akili yako barabara usifanye matusi na wewe kabla ya hata bungeni hujaingia. Hakuna kizuizi wala ugumu wowote wakukirihisha katika kuyapata hayo (kuununua uraia wao) wala kuishi wakati unayatafuta hayo. Ugumu unakuja pale mtu anapobidi bila ya kupenda wala kutaka kunasa katika mtego wanaouwacha wazi wanasiasa wa TZ wasiotaka kuliweka sawa hili jambo la "dual citizenship" ili kumuwezesha mTZ wa namna hii kuendelea kumaintain mapenzi na huruma yake kwa nchi yake tukufu TZ, yaani ni kama kumsukumiza mtu huyu ajinase na ajihesabu kwamba kwa kufanya hivyo basi yeye ameukana uTZ, ameyakana mapenzi na huruma zake juu ya nchi yake tukufu. Kitu ambacho SIO KWELI, NI UONGO na MAFISADI wanasiasa wetu wanalijua hilo, na kama wewe hilo halikupitii akilini mwako basi unahitaji kukatwa kichwa labda ndio ufahamu. Kama mtu yule anayo nafasi atakataa katakata na kama ingeweza kuingia vitani kupinga hilo basi mtu yupo tayari kumwaga damu. Lielewe vizuuuuuuuri hilo wewe Mgombea Ubunge. HUU NI UFISADI , HAYA NI MADHILA, HUU NI UKATILI. Ni ukatili kuliko ukatili walioufanya watu wa ulaya dhidi ya wahindi wekundu wa Amerika au Aboriginal wa Australia walipovamia mabara hayo ya Amerika na Australia. Ni ukatili kuliko walioufanya makaburu wa Afrika ya Kusini dhidi ya ndugu zetu weusi wa Afrika ya kusini. Ni matusi sawa na kumwabia mtanzania huyu baada ya maisha yote aliyoishi ya pengine umri wa 30-40 na kumjua vilivyo nani baba yake na nani mama yake na kama wapi wamezikwa kama wazee wake hao ni marehemu, leo hii unamwambia kwamba yeye ni mtoto wa haramu na kwamba yule anayemjua baba yake sio baba yake, au kwa maana nyengine ni mtoto wa zinaa. Matusi makubwa wanayafanya wanasiasa wa CCM (wao ndio tawala) ambao wengi wao ni MAFISADI eti tu kwasababu katika MRADI wa kuyaweka sawa mambo ya dual citizenship hauna faida ya moja kwa moja ya matumbo yao ya mamia ya mamilioni au mabilioni ambazo watatia ndani. Hiyo ndio tu motivation yao ya kuyafanyia kazi masuala ambayo yanayo"greater good" tu na hayana "personal ufisadi". Ndio maana nasema MAFISADI ni najisi. Mbwa au nguruwe bora kuliko wao. As long as tuna viongozi mafisadi wanaijificha ndani ya CCM badala ya kufukuzwa ili watiwe mkononi na sheria, nchi yetu tukufu IMEFISIDIKA.

Sasa ndugu yangu Mgombea Ubunge MTU ATWEZAJE KURUDI NA KUSIMAMA JUKWAANI KISHERIA KATIKA HALI HII NA HALI YA KUWA MAFISADI WAMESHAMFUKUZA NA KUMNYANG'ANYA HATA KITAMBULISHO CHA URAIA WAKE???? Kwa taarifa yako wachache mno wa waTZ hao anesalimisha kitambulisho chake KWA HIYARI (soma chini), wengi wao huficha kuwaambia watoto wa mafisadi katika balozi zetu za nje kwamba wamenunua uraia mwengine, na hujumuika katika kila jambo la kiTZ, liwe la kitaifa au la kibinadamu wanapokuwa katika nchi hizo, na wengine huwa na vyeo na viongozi wazuri wa jumuia za waTZ wanaoishi katika nchi hizo, lakini kwa namna moja au nyengine wanapojulikana tu na hasa inapobidi kutaka kumaintain ile bond iliyopo na nchi na ndugu na jamaa zao waTZ kwa ziara ya matenbezi au shida ambapo hunyang'anywa vitambulisho vyao (pasipoti zao). Na inabidi nikupashe kwamba hakuna hata mmoja wa wanaonyang'anywa pasipoti zao asiyepata mshituko wa moyo, wengine huwa depressed for sometimes, it is emotionally traumatised, na ukiona venginevyo (kutoka juu) basi jua labda hao wana lao against TZ au ni watoto wa mafisadi fulani fulani ambao mapenzi na huruma na TZ tangu awali hawana kwa maana hawakujifunza hayo kutoka kwa wazazi wao ambao ni mafisadi na yeye mwenyewe kapelekwa huko ughaibuni kifisadi. Cha ajabu ni kwamba hizo nchi nyengine unaponunua uraia wa nchi zao hawakukatalii kukupa kitambulisho chao (pasipoti yao) na hawakunyang'anyi hicho ulichonacho cha uTZ. Hebu Mgombea ubunge ukipata nafasi muulize raisi wetu mpaka lini ukatili huu ataachwa uendelee???

Nakuhakikishia pindi mradi huu ungekuwa na udhamimi fulani na kwa kimahesabu mabilioni yanaweza yakatiwa ndani kinyemela, basi ungewaona vingunge wa mawizara mbalia mabli wanagombania mamlaka ya kuutekeleza MRADI huu na dual citizenship ingekuwepo na salama katika muda mfupi tu. Ungesikia hata kusikia sio wizara za Mambo ya ndani na Nje tu bali mpaka wizara na idara za kuchekesha ungeisikia zina namna fulani fulani ya kuhusika katika kuufanikisha. Ku-clarify hivi vitu ndio kazi zao wanasiasa wanaohusika, lakini vinataka moyo wa kujituma na kuipenda nchi sio kuabudu UFISADI.

Kama nipate uraisi mimi kwa muda wa miezi mitatu tu basi TZ lazima iwe safi kwa ufisadi, habaki hata mmoja, and I mean judicially thru the court of law. Hakuna ugumu kutangaza kuvua au kufukuza uanachama na kunyang'nya pasipoti, consequently ubunge na nafasi zao zote kuporomoka, kubadilisha sheria katika kikao cha dharura cha bunge na kupitisha sheria ya capital punishment kwa atakaetiwa hatiani kwa ufisadi, na adahabu kutekelezwa sio zaidi ya wiki tatu ya hukumu. Mbona Iraq (mapuppets) wameweza dhidi ya Saddam. Mbona watu wamewekwa Guantamo bila hata sheria kuwepo, mbona huyu jamaa Jamaican cleric anafukuzwa nchi na tunaambiwa ulimwengu mzima haumtaki hata kosa lake halijulikani, kama lilikuwepo basi aliadhibiwa na hao maadui zake na sasa ni mtu huru, na mengi mengineyo. Sio mada husika hapa, lakini inaonyesha uwezekano kwamba kila nchi ina uwezo wa kupitisha sheria zake kwa mahitaje yake na kwa wakati wake bila hata ya kujali sheria za kimataifa, MAFISADI hawana haki za binadamu.

Ama suala la dual citizenship halitachukuwa hata wiki mbili kuliweka sawa, na waTZ wanaohusika wataanza kujisikia kwamba wao ni "dual citizen" hata kabla ya muswada na sheria kupita, halafu ndio sheria itapita, nayo sio chini ya mwezi mmoja, na wakiingia mafisadi katika hili nalo basi watafuata mkondo ule ule hapo juu. Sasa si utamaliza watuuuu??? uwongo hawamaliziki, ni mafisadi tu ndio watakaomalizika. Ni najisi hawa na kuwasafisha ni kuitoharisha nchi.
 
Mkora

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
360
Likes
9
Points
35

Mkora

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
360 9 35
ndugu yangu mnyika, siku hizi hakuna kitu kinaitwa "watanzania waishio nje ya nchi" ama diaspora.

siku izi mtu akiishi nje ya nchi anabaki mtanzania kwa passport yake tu, laini matendo yake yote anakuwa raia wa nchi hizo za ng'ambo. wao walichoamka na wanachoshinikiza kwa sasa ni uraia wa nchi zaidi ya moja kuwarahisishia kuishi huko nje na sio kwarahishia kuishi tz.

wao hawahangaiki kuleta maisha bora tz bali huhangaika kusaka maisha bora kokote yanakopatikana utadhani yalinyesha kama mvua huko.

ukiwaambia wasimamame majukwaani, watasema wanawaachia watu kama mnyika na mgombea ubunge wagange njaa zao, na wakiona kitu hakiendi vizuri ndio wa kwanza kukosoa na kuapa kuwa hawatarudi hadi watz wabadilike.

masikini hawajui kuwa nao ni sehemumuhimu ya mabadiliko. ndio wale tulioambiwa kuwa siku zote hujiuliza tz itawafanyia nini warudi nyumbani badala ya kujiuliza wataifanyia na wanifanyia nini tz

ni hayo tu kamanda

tuko pamoja
Mkuu heshima mbele kama huo ndio kikomo cha upeo wako ni bora usitimize hilo lengo lako la kugombea ubunge (Yaani is too low ku comment)
 
M-Joka

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2007
Messages
308
Likes
4
Points
0

M-Joka

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2007
308 4 0
kwa kweli ikitokea mie nakamata madaraka, huyu nungunungu anayeitwa dual citizenship mtamsahau labisa
MAFISADI ni najisi na viburi wa kweli. Hakuna kitakachowatosheleza hapa duniani ila ni upanga tu (adhabu ya kifo ) ambayo ni sawa na kuitoharisha(kuisafisha na najisi) nchi. Na kwa viburi vyao huko kesho akhera amewaharamishia Mwenyezi Mungu pepo au kwa uzima wa milele na amewahalalishia adhabu kali ya moto wa jahannan, hawatotoka humo milele.

Hachagui mtu kuzaliwa mahala gani, wazazi wepi na wakati gani. Hizi ni chaguzi zake Mwenyezi Mungu (SW) na hatotutia hesabuni (accountability/ reckoning) kutokana na hayo. Kisha Mwenyezi Mungu akatufundhisha na kutufaradhishia maungano (ties) na wajibu (duties) tulionao kuhusiana na makwetu (homeland) na wazazi, ndugu na jamaa zetu zikiwemo utakatifu (sacredness), mapenzi(love) na huruma(mercy) kuhusiana na vitu na watu hao. Vilevile Mwenyezi Mungu akatufundisha na kutufaradhishia kuhusiana na maisha yetu: zikiwemo haki, halali, heshima na taadhima na unyenyekevu katika ardhi (popote duniani alipokujaalia Mola kufika katika kujitafutia maisha). Na kisha Mwenyezi Mungu atatutia hesabuni (accountability/reckoning) kutokana na maisha hayo.

Haiwezekani (impossible) na hakuna yeyote mwenye uwezo na haki ya kumvua au kumpokonya mtu uzawa wake. Ni haki ya kuzaliwa aliyoiamrisha Mwenyezi Mungu juu ya ulimwengu. Inawezekana kwamba kwa hapo zamani ilikuwa haikuwepo haja, pengine umuhimu wa suala hili "uraia wa nchi zaidi ya moja" specifically dual citizenship lilikuwa halipo, halikuwa na msingi wowote kulifafanua au halikuwa kikwazo chochote. Lakini inapobidi linakuwa kikwazo, basi haikuwa kwa wanasiasa isipokuwa kazi yao ni kuliwekea misingi na taratibu zake sawa tu sio kuliongezea vikwazo. Kuliongezea vikwazo ni dhulma tu, na kama vikwazo hivi vinatokana na kiburi kama unachojidai kuwa nacho wewe, basi hugeuka ni uhaini na ufisadi, si venginevyo. Na hakuna kitakachowatosheleza MAFISADI zaidi ya KIFO na KUTAIFISHWA MALI ZAO ZOOOTE.

Narudia tena!!! Laiti kama kungekuwa kuna mamia ya mamilioni au mabilioni ya kutia ndani kinyemela kwa faida binafsi (UFISADI) katika MRADI (Project au Task) hii ya ku-endevor kuliwekea utaratibu na misingi suala hili badala ya ONLY GREATER GOOD kwa ajili ya nchi na watu wake tu, basi UNGEONA WIZARA zinagombaniana kuutekeleza mradi huo.
 
John Mnyika

Verified User
Joined
Jun 16, 2006
Messages
715
Likes
23
Points
0
Age
37

John Mnyika

Verified User
Joined Jun 16, 2006
715 23 0
Ingawa mimi si mfuasi wa Michiavellism, kwa imani yao wanaamini kwamba watawala mara nyingi hufanya jambo kwa hofu na mara chache sana hufanya kwa upendo.

Kama hivyo ndivyo, kwa wale ambao mnataka uraia wa nchi mbili(dual citizenship) hamuoni kwamba kudai haki za kisiasa kunaweza kuwa njia ya kuwapa watawala hofu na kutekeleza matakwa yenu?

Mathalani, kama mkaweza kuzuia kipengele cha watanzania walio nje ya nchi kukatazwa kuchangia uchaguzi Tanzania ambacho kitajadiliwa na Kamati ya Bunge kuanzia wiki ijayo; na wakati wa uchaguzi mkachangia kwa hali na mali wagombea, ni wazi kwamba watawala watajipendeza kwenu. Na wakijipendekeza mnaweza kuwapa masharti ya kuingiza suala lenu katika ilani/ahadi za kampeni.

Au kuna muswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambao pia utajadiliwa na kamati za bunge kuanzia wiki ijayo, mnaweza kabisa kutaka kipengele cha watanzania walio nje ya nchi kuruhusiwa kupiga kura. Mkishakubaliwa kupiga kura, vyama vitawajibika kujinadi kwenu kwa ilani/ahadi za kampeni. Sasa kati ya mambo ambayo yatalengwa na kampeni hizo kwa hofu(au mara chache upendo) juu ya nyinyi wapiga kura si litakuwa hilo suala la uraia wa nchi mbili?

JJ
 
Forum statistics

Threads 1,189,736
Members 450,798
Posts 27,645,707