Watanzania mlichomfanyia Tundu Lissu ''Mungu'' anawaona!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Enyi Watanzania mtapata ''laana'' kwa kile ambacho mmemfanyia Tundu Lissu katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2020!

Mlianza kumwaminisha kuwa ni NI YEYE, NI YEYE wakati akiwa Ulaya mpaka akaamua kufunga safari ya kuja nchini ili mumkabidhi Ikulu pamoja na kusita kurudi nchini kwa miaka 3 akidai hawezi kuja Tanzania kwa sababu serikali haijamhakikishia ulinzi!

Imani yake ilianza kuongezeka siku alipofika kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege Dar es Salaam na kusindikizwa na kundi la Watanzania mpaka kwenye ofisi za CHADEMA zilizoko mtaa wa Ufipa, Kinondoni!

Imani yake ilizidi kuongezeka zaidi baada ya kuanza kampezi za Uchaguzi Mkuu kutokana na watu waliokuwa wanahudhuria mikutano yake!

Imani aliyodhani mmempa ilimfanya aanze kuongea kwenye mikutano kama mwanasiasa ambaye tayari ameishakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania!

Kama hiyo haitoshi, aliamua pia kumleta Sheikh Ponda Issa Ponda kwenye mikutano yake ili aanze kuwalisha viapo vya kumchagua yeye au kuingia barabarani kama atawataka kufanya hivyo!

Kukubali enyi Watanzania kulishwa viapo na Sheikh Ponda ilizidi kumuaminisha kuwa yoyote atakayo waambia mtafanya! Kujiamini huko kukazaa Dharau na Kejeli kwa mgombea wa chama cha ''kijani'' . Nawaambia hivi, kura za Magufuli zisipotosha tutamuondoa Ikulu kwa heri au kwa shari! Mimi sio kama Lowassa, oooh, amelegea mpaka anapiga magoti kuomba kura na nawaambia wiki ijayo atalala chali!

Kila mara akiongea maneno ya dharau na kejeli kwa mgombea wa chama cha kijani mlikuwa mnashangilia!

Tarehe 29 Oktoba ilikuwa ni siku ambayo Tundu Lissu hawezi kuwasahau enyi Watanzania! Nilimuona siku hiyo wakati akiongea na vyombo vya habari akiwa Singida kwa jinsi ambavyo alikuwa ''amenyong'onyea'' baada ya kuanza kugundua kama Watanzania ''hawasomeki''.

Siku ya Jumamosi ya tarehe 31 Oktoba ilikuwa ni siku ambayo viongozi wa CHADEMA na ACT-Wazalendo wakakaa kikao na kutoka na maazimio ambapo mojawapo ni kuanza kwa maandamano siku ya Jumatatu yasiyo na kikomo nchi nzima ili kumuondoa Rais Magufuli Ikulu kwa heri au shari!

Jumatatu ya tarehe 2 Oktoba ilikuwa ni siku ambayo Watanzania walimuonyesha Tundu Lissu ''rangi zao'' kama wajumbe wa CCM walivyowaonyesha wagombea udiwani na ubunge ndani ya CCM! Hakuna cha maandamano wala ndugu yake na maandamano. Kibaya zaidi, watanzania walionekana wakiendelea na kazi zao za kila siku!

Walewale waliokuwa wakimshangilia na kumwambia aitishe maandamano na wako tayari kwa lolote hawakuonekana barabarani bali walionekana kwenye mitandao ya kijamii wakisadifu ule usemi usemao, ''debe tupu haliachi kuvuma''.

Tundu Lissu hakuwa na nafasi nyingine bali kujisalimisha kwenye balozi za Ulaya ili arudi kule alikokuwa anaishi kuanzia mwaka 2017.

Nilimsikia kwenye redio ya Sauti ya Marekani (VoA) baada ya kurudi Ubelgiji akisema kwa unyonge kuwa kwa sasa amegundua kuwa Watanzania hawajawa tayari kwa mabadiliko na kwamba yeye ametimiza wajibu wake!

Nadhani mshituko alioupata umemfanya mpaka amekosa cha kusema kwenye akaunti zake za mitandao. Yuko kimya tokea tarehe 2 Novemba baada ya kugundua ''rangi halisi'' za Watanzania! Akaunti zake bado zina bango linalosema, Tundu Lissu, Rais 2020!

Tundu Lissu anashindwa kuelewa kuwa mwanasiasa anayehamasisha na kuandaa watu kufanya jambo lakini baadaye wasilifanye anakuwa mshindwa ni yeye na sio aliowahamasisha kwa sababu hawakumuomba kufanya hivyo!

Kwa kweli, Watanzania mlichomfanyia Tundu Lissu ''mungu'' anawaona!
 
Mbona hujamalizia mlivyoshinda uchaguzi kwa kura za kwenye mabegi meusi, ungeonekana wa maana kama ungeelezea jinsi mlivyopata "ushindi wenu feki"

Endelea kujifanya kipofu na hii mipasho yako wakati mliokula vyao wameanza kuwadai mvitapike, akili zitawarudia tu, beberu keshapunguza misaada ndio mjitutumue sasa na "donor kantre"
 
Back
Top Bottom