Watanzania milioni moja – One –MT project ni sawa na NICOL?

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Watanzania milioni moja – One –MT project

Nimekaa nikifikiria kuhusu ujasiriamali nikajikuta naona mradi madhubuti ambao kama kweli, kwa nia moja na thabiti isiyo na chembe ya ufisadi inaweza kubadili kabisa mustakabali wan nchi yetu.

Watanzania milioni moja katika mradi huu kila mmoja anatakiwa kutoa US $ 1000, that sums up to US$ 1,000,000,000. Nikiwa kama mhandisi miradi niliyesimamia miradi mingi na yenye thamani mpaka kufikia US $ 400,000,00 ntajaribu kuiweka hoja yangu katika mtizamo huo.

Ieleweke kwamba tangu nchi yetu ipate uhuru hakuna mradi hata mmoja uliowahi kujengwa kwa gharama ya one billion US dollars na si hapa tu hata katika nchi zote za Africa miradi hiyo inahesabika. Hivyo basi that is a huge amount of money!!!!!!! Kumbe watanzania milioni moja……

1.Tunaweza kujenga barabara ya lami ya kisasa kabisa kutoka Dar mpaka Mwanza.

2.Tunaweza kimiliki Liganga – Mchuchuma kwa asilimia 100.
3.Tunaweza kujenga shule za kisasa kabisa say kwa US $500,000 each elfu mbili.
4.Tunaweza kujenga hospitali bora na za kisasa kabisa say kwa US $1, 000,000 each elfu moja.
5.Tunaweza kujenga bomba la maji kutoka Mwanza mpaka Dodoma na mikoa ya jirani
6.Tunaweza kujenga reli kutoka mtwara mpaka makambako.
7.Tunaweza kujenga PP'F towers 200
8.Tunaweza kujenga bandari zote tatu kubwa – sea ports (Dar, Tanga, Mtwara)
9.Tunaweza kumiliki mabasi yoote Tanzania.
10.Tunaweza kujenga mijengo ya Balali kwa bei halali kama mitano hivi.
11.Tunaweza kumiliki migodi yote iliyopo Tanzania kwa sasa
12.Tunaweza kujenga gas - power station Kubwa kuliko zote in East ,Central and Western Africa.
13.Tunaweza kuweka lami barabara zote za jiji la Dar.
14.Tunaweza kujenga viwanja vya michezo mithili ya ule wa mpya wa taifa kila moka
15.Tunaweza kuwa na capital kuliko fisadi yeyote hapa nchini.
16.Tunaweza kutoa ajira hizo milioni zilizo ahidiwa na JK.
17.Tunaweza kuunganisha mikoa yoote ya pembezoni mwa TZ kwa lami.
18.Tutakuwa tuna hela nyingi kuliko hata zile alizotoa Joji kichaka.
19.Tunaweza pia kununua Man U, Arsenal na Chelsea.
20.Tunaweza kufanya mengi tuuuuuuuu Kubwa zaidi hata yale Ambayo serikali imeshindwa kabisa kuyafanya toka tupate uhuru.

Truth: Watanzania milioni moja wanaoipenda nchi yao wanaweza kuiboresha nchi yao kwa mengi.

Challenge: Inawezekana kweli kukusanya watu milioni moja kuwauzia hii hoja ikakubalika na kutekelezeka?Who Hill manage this Project? Sounds not really uhhhh!!!!!

Ok let's work it out this way- Katika watanzania milioni moja, nusu yake yaani laki tano wawe ni govt fund. The remaining laki tano gawa kwa kumi = 50,000. Hivi haiwezekani kupata watanzania 50,000 wenye $10,000 kila mmoja tukatekeleza hii One –MT project (One million Tanzanians project).

Nakaribisha mawazo na njia mbadala, we can work thru One –MT project. Ninaamini tunaweza kufanya makubwa yasiyotarajika. Kama sikosei akina Mosha na ile NICO ni the same idea!!!!!!! Well but this is One –MT project.

Nawakilisha.
 
Well, it's a good patriotic idea!
Lakini, hebu tujadili status ya NICO tujue kama mawazo uliyotoa sio waliyofikiria awali. Kama ndio lilikuwa lengo lao na wameshindwa kufika basi nini kikwazo. Tukipata majibu basi nina hakikka One-MT haitakwama!
 
Ni wazo zuri you know what kuna watanzania ambao wanapesa nyingi sana sasa hivi lakini they do not know how to invest, wanaishia kujenga baa, guest house, saloon, maduka,nk Can you imagine a professor in Engineering own a bar and guest house? I am telling you we need revolution inour ideas of investiment. Utakuta mbunge na posho zake zote anatengeneza genge la kitimoto kimara. Hili ni tatizo kubwa kwa nchi yetu we do not invest according to our profession and experience.

Tukija ktk mada inafaa kubainisha miradi kwa kutoa maelezo ya kina kuhusu umuhimu wake kwa watu wenyewe. Hali ya kisiasa tulionayo kwa sasa Tanzania ni mbaya, hatuaminiani, watu wengi watasema wewe ni taperi unataka kufisadi.
 
Duh hii kali mwanangu! nimecheka sana..ila ndo ukweli...Africa kazi tunayo!!!
 
Nyambala,

Akili tunazo, uchumi tunao, vyote tumevikalia!

Tatizo si hela au kudai utapata wapi mtanzania mwenye shillingi 1.2 million, tatizo ni wito na kuwa na nia ya kujituma bila kuwa na kisingizio!

Hata kama ni if, if, if, bottom line it can be done if we will be open minded to embrace the idea and to put it incto actions without fear.

Kinacho tukwamisha Watanzania ni kusubiri fulani na fulani wakifanye, au tufanyiwe na mwingie tuangalie vikiundwa, lakini tunasahau kuwa tuna uwezo mkubwa wa akili, mali, maarifa na vibarua kuhakikisha kazi hizi zinafanyika.

Ni wakati utashi wa maendeleo uanze kutoka nafsi zetu na si kutegemea Serikali ifanye kila kitu. Tunategemea Serikali ifikirie, ipange, itoe pesa, iendeshe na kufanya kila kitu na sisi kazi ni kusubiri na tukikosa tunakimbilia kulaumu na kupandisha mori!

Penye nia, pana njia. Laweza kufanyika, ni jukumu la kila mtu kujituma na kutumika.
 
Tuanze na wanachama wa JF,...........tujitolee kusaidia uendeshaji wa JF............baada ya hapo nina imani hii hii JF itakuwa chanzo kizuri cha kuhamasisha watu kushiriki ktk mawazo kama hayo
 
Tatizo la miradi mingi bongo, ina endeshwa na watu wenye private agenda, na si kwa maslahi ya share holders, hivyo inakuwa ngumu kuwashawishi watu ku-invest.
Eg TOL kuna watu walinunua share wakati ule Tshs 500.00 wakiwa na matumaini, sasa hivi nearly 10 years sana sana wamerudi nyuma share a valued at 250 tshs couple na devaluation of tshs , value yake tunaweza sema ni tshs 10 kwasasa na hakuna cha dividend au nini, na watu wanaoiendesha kuanzia Board na Management wanaangalia maslahi yao na familia zao , na kuwaacha solemba shareholders.
Wakisubiri huyo strategic au wakichelewesha kupata strategic investor kwa sababu maslahi yao hayapo.
Sasa kwa hili ningeomba serekali iingilie kati kuwanusuru shareholders wanao buruzwa na wenzao na pia kwa maendeleo ya taifa, kwani kufunguka kwa mlango moja unawezesha kufunguka kwa milango mingine.
Kutokana na Somo la hapo juu, utaona Tanzania tunacho kosa ni kutokujua tofauti ya kitu cha public na kitu cha binafsi.
Ukianzisha public thing lazima uwe tayari for transparecy na kuchunguzwa, sasa mtu mwingine ukimwambia hivyo ana ng'aka " nyie mnafikiri mimi nimekuja kuiba hela zenu au mimi nilikuwa tajiri toka zamani etc etc.

Sasa ili kufikia hili lengo
Moja vyombo vya serekali vitekeleze majukumu yake kwenye kupigia pange vitu hivi, na vinavyokwenda na vitu kama hivi, kama annual general meeting, auditing na kuziweka wazi hizo report na mipango ya maendeleo. na ikiwezekana Registrar akiona Management au Some Board memers wanafanya sivyo kuwaeleza shareholders ili mambo yarekebishwe mapema.
Sababu uelewa wea shareholders wengi wa tanzania ni mdogo hivyo wanahitaji kinga ya serekali kwa muda na sheria nyingine ndogo ndogo.
Pili viongozi wa such Public institution wakubali kuwa wawazi , wakiulizwa wasikasirike hiyo ni part and parcel of something being public, aidha mtu unaficha ficha mambo, kulikoni? utajihisi vibaya ikiwa umefanya vibaya.

Last but not the least naunga mkono hoja ya mtoa mada na wachangiaji wengine, ili mradi transaction zipitie bank iwe deposit au matumizi , na bank statement iwe wazi kwa shareholders, tujengane imani.
 
This is a good idea. NICO are already doing something similar BUT What if we did it somehow differently...

We can take example of donors who issue loans/grants to push specific projects. We on the other hand can become internal loaners (with interest which is better than outside) and push what we think are key projects.

Lets say we get 6000 people to start with and each INVESTS (forget donate) 1000usd. We will have 6,000,000 million dollars. Then lets say we loan the government this money with interest payable in 4 years. Interest only 10%. We end up with 1100usd each at the end of four years and we will have contributed to the development of our country.

The key projects which I think we can afford and which can push the economy are:-

1)______________________________
2)______________________________
3)______________________________

The big task will be to sit with the government and convince them to take our loan on these projects.

We can call this group the SIX MILLION GROUP.
 
A grand project or investment scheme of this nature will not succeed in Tanzania because Tanzanian society is not ethnically uniform. A majority of people still strongly identify themselves on the basis of ethnicity and hold significant loyalties to their own ethnic groups or tribes (You all saw how 2 days ago a whole bunch of Wasukuma spent a whole 48 hours online passionately defending Mr. Chenge - in what appears to me to be a well organized PR exercise by those involved), and this is more so in rural localities.

Any existing notions of nationality and citizenship are at best shallow and do not hold in certain important aspects of life especially those that have to do with access to and distribution of scarce resources. National cohesiveness and unity work best only at formal official levels. Private development projects should therefore be left only to ethnic-based development associations to handle.
 
Huu mradi wako mzuri wa kufikirika unaweza pia kuwa mwanya mzuri sana wa ufisadi!Kuna watu udenda unawadondoka wakati wakisoma hapa!
 
Watanzania milioni moja – One –MT project

Nimekaa nikifikiria kuhusu ujasiriamali nikajikuta naona mradi madhubuti ambao kama kweli, kwa nia moja na thabiti isiyo na chembe ya ufisadi inaweza kubadili kabisa mustakabali wan nchi yetu.

Watanzania milioni moja katika mradi huu kila mmoja anatakiwa kutoa US $ 1000, that sums up to US$ 1,000,000,000. Nikiwa kama mhandisi miradi niliyesimamia miradi mingi na yenye thamani mpaka kufikia US $ 400,000,00 ntajaribu kuiweka hoja yangu katika mtizamo huo.

Ieleweke kwamba tangu nchi yetu ipate uhuru hakuna mradi hata mmoja uliowahi kujengwa kwa gharama ya one billion US dollars na si hapa tu hata katika nchi zote za Africa miradi hiyo inahesabika. Hivyo basi that is a huge amount of money!!!!!!! Kumbe watanzania milioni moja……

1.Tunaweza kujenga barabara ya lami ya kisasa kabisa kutoka Dar mpaka Mwanza.

2.Tunaweza kimiliki Liganga – Mchuchuma kwa asilimia 100.
3.Tunaweza kujenga shule za kisasa kabisa say kwa US $500,000 each elfu mbili.
4.Tunaweza kujenga hospitali bora na za kisasa kabisa say kwa US $1, 000,000 each elfu moja.
5.Tunaweza kujenga bomba la maji kutoka Mwanza mpaka Dodoma na mikoa ya jirani
6.Tunaweza kujenga reli kutoka mtwara mpaka makambako.
7.Tunaweza kujenga PP’F towers 200
8.Tunaweza kujenga bandari zote tatu kubwa – sea ports (Dar, Tanga, Mtwara)
9.Tunaweza kumiliki mabasi yoote Tanzania.
10.Tunaweza kujenga mijengo ya Balali kwa bei halali kama mitano hivi.
11.Tunaweza kumiliki migodi yote iliyopo Tanzania kwa sasa
12.Tunaweza kujenga gas - power station Kubwa kuliko zote in East ,Central and Western Africa.
13.Tunaweza kuweka lami barabara zote za jiji la Dar.
14.Tunaweza kujenga viwanja vya michezo mithili ya ule wa mpya wa taifa kila moka
15.Tunaweza kuwa na capital kuliko fisadi yeyote hapa nchini.
16.Tunaweza kutoa ajira hizo milioni zilizo ahidiwa na JK.
17.Tunaweza kuunganisha mikoa yoote ya pembezoni mwa TZ kwa lami.
18.Tutakuwa tuna hela nyingi kuliko hata zile alizotoa Joji kichaka.
19.Tunaweza pia kununua Man U, Arsenal na Chelsea.
20.Tunaweza kufanya mengi tuuuuuuuu Kubwa zaidi hata yale Ambayo serikali imeshindwa kabisa kuyafanya toka tupate uhuru.

Truth: Watanzania milioni moja wanaoipenda nchi yao wanaweza kuiboresha nchi yao kwa mengi.

Challenge: Inawezekana kweli kukusanya watu milioni moja kuwauzia hii hoja ikakubalika na kutekelezeka?Who Hill manage this Project? Sounds not really uhhhh!!!!!

Ok let’s work it out this way- Katika watanzania milioni moja, nusu yake yaani laki tano wawe ni govt fund. The remaining laki tano gawa kwa kumi = 50,000. Hivi haiwezekani kupata watanzania 50,000 wenye $10,000 kila mmoja tukatekeleza hii One –MT project (One million Tanzanians project).

Nakaribisha mawazo na njia mbadala, we can work thru One –MT project. Ninaamini tunaweza kufanya makubwa yasiyotarajika. Kama sikosei akina Mosha na ile NICO ni the same idea!!!!!!! Well but this is One –MT project.

Nawakilisha.

..mtu kutoa milioni moja sio issue. issue ni atapata faida gani yeye binafsi? jua,hiyo itakuwa kama uwekezaji fulani!

..pili,atakuwa na uhakika gani wa hiyo fedha kutumika ipasavyo?. kwani,tuna historia ya kutumia vibaya fedha za miradi!
 
Hivi na UMOJA FUND bado ipo, wameshanunua NBC na kuwekeza kwenye makampuni makubwa au bado wana mobilise funds?
 
Watanzania ni mabingwa wa skepticism!

This is why we are failing to make any development progress that is self innitiated.

Angekuja mzungu na kutoa mwamko na mawazo kama haya, tungeyapokea bila kusita wala kuanza kutoa vijisababu kabla ya kazi kuanza.

Sisi ni mabingwa wa udhuru, hatupendi kujaribu na kufanya mambo bila kuona fulani kfanya na kafanikiwa kiasi gani.

Kila mradi una gharama, kutakuwa na ubinafsi, ubangaizaji, na hata kuwepo wenye nia ya kuhujumu.

Angalia makanisani na misikitini, ni tabia za kibinadamu.

Lakini, kukataa kabisa hata kufikira na kujiuliza kwa mtizamo chanya kuwa malengo haya yatatufikisha wapi na kutuinua kiasi gani hatutaki. Tunakimbilia kuanza kutafuta sababu za kuvunja nguvu za msukumo huo wa kuanza kujijenga na kuendeleza.

Faida ya mafanikio ya mradi kama huu, ni yetu sote na si ya mtu mmoja.

Mimi nilifikiri Jambo Forum ni mahali ambapo tunapigania maslahi ya Taifa na tunaweza kuweka nguvu zetu kujenga Taifa linalojitegemea na lililoendelea bila kujali ni nani atanufaika. Sasa kama vitu Nyambala alivyosema ambavyo manufaa yake ni kwa Taifa zima vinaonekana kuwa vitamnufaisha mtu binafsi kwa mawazo ya wengine , basi nafikiri kwa kutumia kiingereza "we are all not on the same page" kuhusu kupigania maslahi na maendeleo ya kulijenga Taifa letu.
 
Ni wazo zuri sana hili Rev, lkn wasiwasi unakuja kwa vile miaka kadhaa iliyopita ilikuja kwa mbwembwe sana UMOJA funds, watuwakanunua shares kama hawana akili kwa kujua kuwa wale waliokuwa wadau wakuu wa mfuko huu ni watu wa kuheshimika sana Tanzania. Lengo lao kubwa lilikuwa kumobilise funds na kununua vitega uchumi au kuwa wabia katika mashirika makubwa badala ya kuwaachia wawekezaji kutoka nje. Lakini hadi leo hii sijui ni mafanikio gani yamepatikana. Na sasa kuna kitu inaitwa NICO na wenyewe wanashawishi watu kununua shares ili kuwawezesha watanzania kumiliki uchumi wao wenyewe. Sijui na hili limefikia wapi. Labda mwenye kujua zaidi anaweza akatuelewesha na then kuweza kufanya analysis kabla ya kuanza kuifikiria kwa undani MT project, inasound ni yenye manufaa sana.
 
A grand project or investment scheme of this nature will not succeed in Tanzania because Tanzanian society is not ethnically uniform. A majority of people still strongly identify themselves on the basis of ethnicity and hold significant loyalties to their own ethnic groups or tribes (You all saw how 2 days ago a whole bunch of Wasukuma spent a whole 48 hours online passionately defending Mr. Chenge - in what appears to me to be a well organized PR exercise by those involved), and this is more so in rural localities.

Any existing notions of nationality and citizenship are at best shallow and do not hold in certain important aspects of life especially those that have to do with access to and distribution of scarce resources. National cohesiveness and unity work best only at formal official levels. Private development projects should therefore be left only to ethnic-based development associations to handle.

Bullshi.t! Who are those "a whole bunch of Wasukuma"? What made you conclude that those who "passionately" defended Mr. Chenge were Wasukuma? Why couldn't they be Wanyaturu or Wangoni, bent, or straight?

Dude, no evidence no right to accuse! Get it?
 
I suggest you read through the relevant thread post by post while paying close attention to what one "Matiksa" wrote. It is my belief that this individual together with "zeenam" and the thread starter (among others) colluded with each other in a joint effort to introduce "reasonable doubt" in the court of public opinion against Mr. Chenge.
 
Ni wazo zuri sana hili Rev, lkn wasiwasi unakuja kwa vile miaka kadhaa iliyopita ilikuja kwa mbwembwe sana UMOJA funds, watuwakanunua shares kama hawana akili kwa kujua kuwa wale waliokuwa wadau wakuu wa mfuko huu ni watu wa kuheshimika sana Tanzania. Lengo lao kubwa lilikuwa kumobilise funds na kununua vitega uchumi au kuwa wabia katika mashirika makubwa badala ya kuwaachia wawekezaji kutoka nje. Lakini hadi leo hii sijui ni mafanikio gani yamepatikana. Na sasa kuna kitu inaitwa NICO na wenyewe wanashawishi watu kununua shares ili kuwawezesha watanzania kumiliki uchumi wao wenyewe. Sijui na hili limefikia wapi. Labda mwenye kujua zaidi anaweza akatuelewesha na then kuweza kufanya analysis kabla ya kuanza kuifikiria kwa undani MT project, inasound ni yenye manufaa sana.

Mama,

Tatizo letu bado linarudi kwenye kutaka mambo kwa urahisi, kuacha kufuatilia na kusubiri wengine wafanye kazi.

Kwenye hiyo issue ya UMOJA na hata NICO, ni watu wangapi walisoma proxy na addendum ambazo zilijenga hizo FUND?

Je ni wangapi wanajua haki zao kwa kusoma articles za incoporation na makbrasha mengine kuhusu kuundwa kwa Funds hizi, uongozi wake, maamuzi yake, mgawanyo wa mapato na mambo mengine ya kisheria ili mtu alinde mtaji na investment yake?

Sasa kama mtu alikimbilia kuchangia mfuko kwa kuwa alisikia kuwa atajipatia hela marudufu katika miaka miwili lakini hakusoma vile vipengele vya kisheria kuhusu wajibu wake na haki yake kwa dhati, basi tunabakia kuwa wadandiadi miradi, mithili ya Upatu kwa kuwa tumeweka mbele TAMAA ya kupata pesa na si kujifunza kwanza ni wapi tunaweka pesa zetu na zitatuzalishia nini na kwa muda gani na manufaa yake ni nini!

Kila kitu na mradi una mipango, sheria au mkataba. je ni kazi gani ngumu kupitia mkataba na mipango kabla hujamwaga fedha zako ndani ya kisahani cha SADAKA?
 
Back
Top Bottom