Uchaguzi 2020 Watanzania milioni 29,188,347 kuwahukumu akina Magufuli (CCM), Lissu (CHADEMA) na Membe (ACT-Wazalendo) Oktoba 28, 2020

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa mstaafu, Semistocles Kaijage, amesema daftari la wapiga kura lina wapigakura milioni 29,188,347.

Nipashe.

Kimahesabu hapo najua Magufuli ana Kura zake Milioni 20 Kamili, Lissu ana Kura Milioni 9,188,347 na Membe ana 0. Mshindi kuwa John Magufuli.

===
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa mstaafu, Semistocles Kaijage, amesema daftari la wapiga kura lina wapigakura milioni 29,188,347.

Amesema hayo leo katika kikao baina ya NEC na vyama vya siasa nchini. Amesema bajeti inayotarajiwa kutumika katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu ni Sh. Bilioni 331.7.

Amesema kutakuwa na vituo 80,155 vya kupigia kura na kila kimoja kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500. Jaji wa Rufaa mstaafu Kaijage amesema jumla ya asasi za kiraia 97 zenye nia ya kuwa watazamaji wa uchaguzi ndizo zimekidhi vigezo na tayari zimepewa taarifa na zinasubiri kupewa vibali wakati ukifika.

Amesema kwa upande wa watazamaji wa uchaguzi wa Kimataifa mwaliko umetolewa na mchakato wa kupokea maombi unaendelea."Wakati ukifika tutawajulisha idadi ya waombaji hao," amesema.

Kuhusu malalamiko ya baadhi ya watendaji wa uchaguzi kutokuwapo ofisini wakati wa uteuzi wa wagombea, Kaijage amesema kitendo hicho ni kinyume cha maadili na kwa namna yoyote hakikubaliki.

" Tume tayari imekutana na wasimamizi wote wa uchaguzi upande wa Tanzania Bara Julai24, jijini Dodoma na msisitizo uliotokewa wazingatie maadili ya Uchaguzi na maelekezo yanayotolewa na NEC,"

Amesema tayari wasimamizi wa uchaguzi wamekwisha kuteuliwa na wanaendelea na mafunzo ambayo yatakamilika Jumatatu.

Pia, amevitaka vyama kuwasisitizia wagombea wahakikishe wanajaza fomu kwa usahihi ili kuepuka dosari zinazoweza kuwafanya kushindwa kushindwa kuteuliwa.

Amesema wagombea wana haki ya kisheria ya kuweka pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake na kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msajili wa Vyama vya Siasa ni miongoni mwa waliopewa haki hiyo.

Mkurugenzi wa NEC, Dk. Wilson Charles, amesema katika kampeni za uchaguzi wagombea wanatakiwa kutumia lugha ya Kiswahili tu na kama eneo husika hawajui pawepo mkalimani.

Pia amesema haitaruhusiwa kampeni kwenye nyumba za ibada au kutumia viongozi wa dini kuwafanyia kampeni.

Chanzo: IPP Media
 
Waliojiandikisha wote ni CCM, wapinzani waligoma kushiriki. Wakipigwa wasilalamike

Wapigwe au ' automatically ' hapo ni kwamba tayari wameshapigwa na sasa tunasubiri tu CCM yetu Ishinde na Magufuli atuongoze tena ili tudumu.
 
Sisi hiyo hatujali sana Mkuu ila Kikubwa tunachokitaka tu ni CCM yetu Kushinda Ushindi wa Kishindo na ' Mwamba ' Magufuli aendelee Kutuongoza.
Tatizo Jpm akipewa tena mitano, tutagawanyika mno kama taifa.Tatizo Ni mbaguzi sana
 
Hao wenye huo ' Full Upepo ' wako huko Mtaani / Mitaani una uhakika kuwa wamejiandikisha? Tena ninakushauri Mkuu usiwaamini hao wa Mtaani.
Sawa, tume itende haki, tunataka uwazi toka kampeni, upigaji kura , uhesabuji kura na utangazaji matokeo.Media ziruhusiwe kuingia vyumba vya kuhesabia.
 
Mimi nadhani ataibuka Mshindi wa hata 97% Mkuu kwani huyu ' Mwamba ' kafanya Makubwa sana ndani ya Miaka hii Mitano na yanaonekana pia.
kuliko JK? I don't think so... check your facts.

the first 5 years JK alichangia per capital income growth by $230B.
huyu kwenye miaka 5 ya kwanza amezalisha only $100B (less than 50% ya alichozalisha JK for the same time span).

uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu sana kwa chama chetu CCM kuliko miaka yote, hususani ukizingatia ndani ya CCM pia kuna kamati ya roho mbaya (ambayo mimi ni mmoja wa WAJUMBE!)
 
Sawa, tume itende haki, tunataka uwazi toka kampeni, upigaji kura , uhesabuji kura na utangazaji matokeo.Media ziruhusiwe kuingia vyumba vya kuhesabia.

Kalitafute Taifa lako ndiyo uwape haya Masharti yako Mkuu, ila kwa Tanzania NEC na Serikali ina taratibu zake zilizo ndani ya Katiba yetu pia sawa?
 
Back
Top Bottom