Watanzania mbona tunakuwa kama Makondoo??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania mbona tunakuwa kama Makondoo???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mantuntunu, Jun 28, 2012.

 1. M

  Mantuntunu Senior Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nia yangu sio kutukana ila jamani mimi maongezi yamenichosha, tunaingia humu tunachonga weee, tunaongea weee, tunaandika wee, labda nikubali kuwa hii ni namna ya kupunguza hasira zetu tu. Tuliwachagua wabunge wetu watuwakilishe na kutuhabarisha mambo yote yanayotendeka serikalini. Kwa kweli naomba niseme kwamba, especially wabunge wa upinzani wamejitahidi sana ktk kutuhabarisha na kutujulisha mapungufu na Madhaifu ya serikali yetu. Kuanzia EPA, Richmond, Kiwira, Rada, Ngege ya Rais,fedha za Uswiss, etc, etc.

  Tunaona yaliyotokea kwa Mwakyembe, na sasa Ulimboka na wengine ambao kwa namna moja au nyingine wameadhibiwa katika kujaribu kutetea maslahi ya wananchi. Wengine hata walifikia kuhoji kwa nini aliukubali Uwaziri, na wengine kusema kwamba Mwakyembe kaufyata hivi mlitaka afanye nini?? Sisi kama watanzania tumempa support gani? hata ningekuwa mimi ningeufyata manake wale unaofanya jitihada ya kuwatetea hawaonyeshi hata nguvu angalau nusu ya kukuunga mkono kwenye harakati hizi.

  Tumuangalie Ulimboka, kapigwa karibu ya kuuawa, tusubiri tuone sisi kama watanzania tutafanya nini angalau kuunga mkono ujasiri wake wa kutetea maslahi ya wenzake. Sirikali inasema madaktari watafute njia nyingine ya kudai madai yao na sio mgomo, hiyo sirikali imeona njia ya kumuadhibu Ulimboka ni sahihi? Anyway tuyaache hayo.

  Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kuanzia sasa tusiwalaumu wabunge wetu kwa lolote lile tena hapa naongelea pia baadhi ya wabunge wa CCM ambao wameonyesha kuipinga sirikali wazi wazi. Hawa watu wameishafanya ya kutosha kutuhabarisha mabovu ya sirikali yetu, wizi, mikataba mibovu, ubinafsishaji kwa maslahi binafsi, n.k. Sisi kama Watanzania tunawapa support gani?? Jamani kama hatufahamu sisi ndio wamiliki halali wa nchi hii, tuna sauti kubwa na yenye nguvu sana kama tutaamua leo hii kwamba huu upuuzi wa viongozi wetu basi. Tafakari Chukua Hatua!
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,909
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  Mkuu tangulia mwenyewe Mabwe Pande!!
   
 3. M

  Mantuntunu Senior Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na hicho ndo kinachotuharibu, hakuna cha wewe tangulia, ingekuwa sawa kama ungesema tuungane kwa pamoja watanzania wote na tuone hao polisi kama idadi yao itaweza kutumudu!
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kondoo dhaifu.
   
 5. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  jishtukie ww
   
 6. K

  KISIMASA Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siyo makondoo ni uoga uliokithiri. Halafu kuteteana,halafu kupeana madaraka hata kama hukidhi viwango. Mfano kwenye hili sakata la madaktari bado wapo wenzao tena senior members tu ambao wamekuwepo tangu enzi ndani ya udhaifu huu na wako kimya kabisa. Wanalinda seat zao. Tunahitaji mabadiliko
   
 7. M

  Mantuntunu Senior Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na hicho ndo ninachokisema mimi, we need changes and that starts with us! Kinatakiwa kiwe kitu cha pamoja na sio watu wachache!
   
 8. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Tukianza na wale wakuu Wa hospitali za Mbeya, Bugando na Dodoma wanaofukuza interns doctors itakuwa mwanzo mzuri
   
Loading...