MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,744
- 48,385
- Thread starter
- #221
wee mbuzi kweli,hivi unaelewa ninachokwambia!!!
haya endeleeni kupanua gape maana raha na marengo yenu ni kuona mnaipiku tanzania meanwhile hata tunashangaa GDP yenu ina faida gani.
Enzi za Nyerere ilikua sio kubwa sana ila akawaghubika na Ujamaa ikaanza kutanua, akaja Mwinyi akawaambia yote ruksa, mkawa na kamuamko, ila bado mlikua mumechelewa tayari, mkampa Mkapa, yule alikua mchapa kazi sema akaachia mafisadi ikawa bado mnahangaika hamtufikii, kisha akaja Kikwete, kwa namna fulani sijui ilitokeaje ila enzi za Kikwete mumetufukuzia, hapo nakiri mlikua nusra mtunusie makalio, ila miaka yake ikaisha akajindokea.
Mkampa Magu, yeye akaja kinamna fulani cha tumbua tumbua, ikawa haeleweki sera zake, mkaingiwa na uwoga nchi yote, ikawa hamuhoji chochote, kanunua mindege ambayo mumeipaki, mara korosho full vurugu, mara hiki mara kile, mpaka sasa hatujajua nini haswa kinahusu awamu ya tano, ila tulichofaulu kushuhudia ni kwamba kwa awamu hii pengo baina yetu kiuchumi iliongezeka kwa kasi, tukawaacha na tunazidi kuwaacha kwa mbali, kingine ambacho nilikishangaa ni mauzo yetu kwenu yameongezeka sana kwenye awamu hii, nilidhani yatapungua haswa mlipoanza kutia kuku wetu viberiti, mara mkamate ng'ombe, nilishangaa sana kwenye hizo takwimu.
Halafu ndio mshafaulu kufuta upinzani, yaani nyie tuwewapa buriani kabisa, msubiri Uganda wawapiku, sijui nani atakuja awaokoe....