Watanzania kwanini tunakubali Rais wetu adhalilishwe na media za nje kwa kuitwa "The 'Bulldozer' Tanzanian President"?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Hili ni bandiko la wito kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema na taifa letu, kwa nini tunakubali rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, adhalilishwe na Media za Nje kwa kuitwa The 'Bulldozer' Tanzanian President!, na sisi tunakubali na kunyamaza tuu?! huku Kurugenzi yetu ya Mawasiliano Ikulu ipo?, Idara yetu ya Habari Maelezo ipo?, Waziri wetu wa Habari yupo?.

Soma hii
Dangote accuses 'Bulldozer' Tanzanian president of scaring away ...
What does this statement kuachwa tuu bila kukanushwa, mean to Tanzania investment climate?.
Na hii sio mara ya kwanza kwa rais Magufuli kuitwa hivi, aliwahi kuitwa hivi
John Magufuli - Tanzania's 'Bulldozer' president in profile - BBC News
Tanzania's new president, 'The Bulldozer' Magufuli » Capital News
Tanzania: Tension Between Tanzania's 'Bulldozer' President and ...
Tanzania's bulldozer president takes on London miner - Financial Times
Tanzania's President John Magufuli: The bulldozer crushing ...
Behind Tanzania's President John 'The Bulldozer' Magufuli's mining ...
Tanzania's new president, 'The Bulldozer' Magufuli - Nairobi News

Kwa nini rais wetu, asemwe vibaya na sisi tupo, tunakubali na huku tumenyaza tuu?!. Kurugenzi yetu ya Mawasiliano si ipo?, kwa nini inakubali na kukaa kimya?!,
Idara yetu ya Habari Maelezo si ipo?, kwa nini inakubali na kukaa kimya?!.
Waziri wetu wa Habari si yupo?, kwa nini anakubali na kukaa kimya?!.

Swali msingi ni Jee ni kweli rais Magufuli ni The 'Bulldozer' Tanzanian president?!. Japo kuna wengi watatafsiri Bulldozer kama Tingatinga, lakini kwa wazungu, Bulldozer ni someone who bullies, ambalo sio jina zuri. Jee kweli rasi wetu ni bully?. Kama sii kweli, kwanini tunanyamaza tuu bila kukanusha, maana uongo ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wake sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali mwisho wake hugeuka ni ukweli!.

Mimi naomba kujipambanua kuwa ni Mtanzania Mzalendo wa kweli kwenye media, na kwa mujibu wa fani yangu, kazi yangu na uwezo wangu ni kushauri tuu kwa kuandika au kusema au kutangaza.
  1. Rais wetu alipotuhumiwa kuhongwa suti nilipinga na kushauri.Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi ...
  2. Hata kelele kuhusu udikikiteta wa Magufuli ziliposhika kasi nilishauriUdikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
  3. Magufuli aliposemwa vibaya na SABC, nilishauriSerikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
  4. Rais Magufuli aliposemwa vibaya kuhusu Mimba za utotoni, pia nilishauriJe, Huku Sio Kudhalilishwa Kwa Rais Wetu na Media za Nje?. Jee ...
  5. Juzi kati hapa srikali yetu ilipoitwa Sinister na Authoritarian, pia nilishauri
    Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli ...
Na sasa hapa rais wetu anaposemwa vibaya, na kuitwa The 'Bulldozer' Tanzanian president!, nimeandika na kushauri tusikubali, tusikae kimya, tukanushe unless kama yanayosemwa kumhusu rais Magufuli ni kweli kuwa ni bully anayefanya bullying kustahili kuitwa "The 'Bulldozer' Tanzanian president", vinginevyo tusikubali, tukanushe na tumtetee rais wetu kuwa he is not a bully, hafanyi bullying na sio a bulldozer president!.

Mungu ibariki Tanzania.

Paskali
Alichosema Dangote Mwanzo
Africa's Richest Man Aliko Dangote Criticizes Tanzanian President ...

Alichojibu Waziri Mwijage.
Tanzania: Mwijage Defends JPM Against Dangote Criticism - allAfrica ...

Alichosema Dangote Sasa Kurekebisha Kauli
Dangote says “Sometimes it is just a matter of communication ...
 
bull·doz·er
ˈbo͝olˌdōzər/
noun
noun: bulldozer; plural noun: bulldozers
  1. a powerful tractor with a broad upright blade at the front for clearing ground.
    • a person or group exercising irresistible power, especially in disposing of obstacles or opposition.
      "he was a political bulldozer"
Ni hayo Paskali homeboy! Nitafutie kazi rafiki
 
Sikuile jk alipomsimika kupeperusha bendera ya chama ,ndie aliembatiza na kumpa hilo jina na kummwagia sifa kedekede na yeye mwenyewe akitabasam ,
Sasa leo utamlam Nani,wakati majina wamepeaana wenyewe ccm.

Jk alisimama jukwaani akasema kwa lugha ya msoga kua yeye ndio mwenemwana yaani ndio mwenye mtoto.

Akampa jina mtoto na mtoto kakubali na tabasam aliitoa.
 
Sasa Mkuu unataka wamrembe kwa poda na mafuta ya kunukia na kuandika kitu ambacho si cha kweli? Hata udikteta uchwara wake utaupinga. Anaukubali mfumo wa vyama vingi lakini hapo hapo hataki vyama vya upinzani viendelee kufanya shughuli zake na pia kuviingilia kwa kila namna ikiwemo kuvipiga marufuku kufanya shughuli zake nchini, kuwakamata kila kukicha wabunge wa upinzani, kuwateka, kuwatesa na sasa hata kuwaua wale wote wanaomkosoa huyo dhalimu iwe kupitia vyombo vya habari au social media.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la wito kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema na taifa letu, kwa nini tunakubali rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, adhalilishwe na Media za Nje kwa kuitwa The 'Bulldozer' Tanzanian President!, na sisi tunakubali na kunyamaza tuu?! huku Kurugenzi yetu ya Mawasiliano Ikulu ipo?, Idara yetu ya Habari Maelezo ipo?, Waziri wetu wa Habari yupo?.

Soma hii
Dangote accuses 'Bulldozer' Tanzanian president of scaring away ...
What does this statement kuachwa tuu bila kukanushwa, mean to Tanzania investment climate?.
Na hii sio mara ya kwanza kwa rais Magufuli kuitwa hivi, aliwahi kuitwa hivi
John Magufuli - Tanzania's 'Bulldozer' president in profile - BBC News
Tanzania's new president, 'The Bulldozer' Magufuli » Capital News
Tanzania: Tension Between Tanzania's 'Bulldozer' President and ...
Tanzania's bulldozer president takes on London miner - Financial Times
Tanzania's President John Magufuli: The bulldozer crushing ...
Behind Tanzania's President John 'The Bulldozer' Magufuli's mining ...
Tanzania's new president, 'The Bulldozer' Magufuli - Nairobi News

Kwa nini rais wetu, asemwe vibaya na sisi tupo, tunakubali na huku tumenyaza tuu?!. Kurugenzi yetu ya Mawasiliano si ipo?, kwa nini inakubali na kukaa kimya?!,
Idara yetu ya Habari Maelezo si ipo?, kwa nini inakubali na kukaa kimya?!.
Waziri wetu wa Habari si yupo?, kwa nini anakubali na kukaa kimya?!.

Swali msingi ni Jee ni kweli rais Magufuli ni The 'Bulldozer' Tanzanian president?!. Kama sii kweli, kwanini tunanyamaza tuu bila kukanusha, maana uongo ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wake sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali mwisho wake hugeuka ni ukweli!.

Mimi naomba kujipambanua kuwa ni Mtanzania Mzalendo wa kweli kwenye media, na kwa mujibu wa fani yangu, kazi yangu na uwezo wangu ni kushauri tuu kwa kuandika au kusema au kutangaza.
  1. Rais wetu alipotuhumiwa kuhongwa suti nilipinga na kushauri.Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi ...
  2. Hata kelele kuhusu udikikiteta wa Magufuli ziliposhika kasi nilishauriUdikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
  3. Magufuli aliposemwa vibaya na SABC, nilishauriSerikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
  4. Rais Magufuli aliposemwa vibaya kuhusu Mimba za utotoni, pia nilishauriJe, Huku Sio Kudhalilishwa Kwa Rais Wetu na Media za Nje?. Jee ...
  5. Juzi kati hapa srikali yetu ilipoitwa Sinister na Authoritarian, pia nilishauri
    Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli ...
Na sasa hapa rais wetu anaposemwa vibaya, na kuitwa The 'Bulldozer' Tanzanian president!, nimeandika na kushauri tusikubali, tusikae kimya, tukanushe unless kama yanayosemwa kumhusu rais Magufuli ni kweli kuwa ni The 'Bulldozer' Tanzanian president, vinginevyo tukanushe.

Mungu ibariki Tanzania.

Paskali
Lile swali ulilomtwanga jpm siku ile ikulu uliotea nini mbona siku hizi huchanganui vitu ?
 
Back
Top Bottom