Watanzania kwa sasa matumaini yao ni kwa CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania kwa sasa matumaini yao ni kwa CHADEMA!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by KakaKiiza, Apr 18, 2012.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,236
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka mwaka 2005 watu walijua wamepata mkombozi wao ambaye ni J.Kikwete Edward Lowassa!Kutokana na historia ya Lowassa wakajua basi mambo yamepata mwenyewe na wakadriki hata kupanga safu ya utendaji kura nyingi zikitaka Waziri Mkuu awe Lowassa wakijua ule ukapa walio taabika nao kwakipindi cha miaka kumi(10) sasa utaisha na maisha yatakuwa tambarale!

  Ahaa mambo yakaenda ndivyo sivyo bwana!yakawa yanageuka kila kukicha!Na kwakuwa kibwagizo ilikuwa "Hari mpya,kasi mpya,Maisha Bora kwa kila Mtanzania"!

  Na kila mmoja akavutiwa na maneno haya na wakajua huyu ni Nyerere kutokana na falsafa zake alizopenda kuzitumia, nakumbuka akiwa jangwani aliwahi kusema nyumba za serikali lazima zirudishwe kwa serikali watu wakalipuka kwakushangilia!!Na nadhani kuna hata wapinzani walithubutu kumpa kura wakasema ubunge tunawapa wapinzani,na CCM tunawapa kura za uraisi wabunge waliopata wa CCM wengi walitumia njia chafu kupata ubunge.

  Baada ya hapo CCM ikawa na mbawa ikapaa ikaachana na mzungumzo ya kampeni ikasahau kama iliwahaidi wananchi!!Lakini baada ya miaka mitano(5) watu wakawa wanapiga mihayo wakilia maisha magumu bora Mkapa!,Katika mikutano wakaambiwa kwenye na wapinzani msilie nyinyi ndo mlio ichagua CCM!na mpaka sasa wananchi wapo hoi!!
  Hawajui wapi pakwenda na ninani wakumlilia!

  Lakini baada ya CHADEMA kufanya mikutano nakuwamwagia sera kwa watanzania wanaanza kupata tumaini jipya sasa wanona mtu wakuwakomboa kwenye lindi laumasikini,wakuondoa ufisadi na kweka serikali yenye utii kwa wananchi ni CHADEMA!
  Nasema kwa sasa watanzania wote wanaiangalia CHADEMA kama mkombozi wao!

  CHADEMA IMARISHENI MATAWI YA VIJIJINI AMBAKO WATU HAWANA UELEWA WA SIASA! CHADEMA TUTASHINDA 2015!
   
Loading...