Watanzania kwa rasilimali za taifa ni kama Bakhressa kwa Azam group

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Watanzania hatujitambui

Rasilimali za tanzania ni mali ya watanzania kwa maana watanzania ni wakugerugenzi katika kampuni inayoitwa serikali ya tanzania

Na kampuni hii kazi yake ni simamia rasilimali zetu kwa ajili ya kuboresha maisha yetu.

Rais ni kama mkurugenzi mtendaji wa kuendesha kampuni yetu.

Hivyo sisi watanzania ndio wenye uchungu na mali zetu,

Haya nayasema kutokana na kuona watendaji wa kampuni hii kwa maana ya watumishi wa serikali kutapanya mali za wananchi na wananchi kutokujua kuwa ndio wamiliki na ndio wanaotakiwa kuwa na machungu na kuwajibisha badala yake kusubiri mkurugenzi mtendaji (kwa maana ya raisi) afanye maamuzi na asipofanya maamuzi wanabaki kulilia wafadhili.

Inasikitisha!

Hebu fikiria unakuwa waziri au raisi unaiba bilioni moja tu ya umma na kuifanya ya kwako. sasa wale wanaowasaidia wanaona na mmekaa kimya wanakataa kuwasaidia. hivi mnafikiri yule mwizi aliyewaibia atakuwa na machungu kwa wananchi vijijini kukosa umeme na arudishe fedha aliyoiba na kuachia ngazi, hivi inawezekana eti nchi imenyimwa misaada kama umeiba fedha ya umma unauwezekano wa kuishi kama mfalme eti urudishe fedha hii ya masikini ili wao wasaidiwe?

Anayeweza kudhani hilo linawezekana ni mjinga wa kufikiri. kama mwizi hakuwahurumia masikini hawa kuwaibia atawahurumiaje kunyimwa misaada kwa kutomshughulikia?

Mali za watanzania ni mali ya watanzania na watanzania ndio wanaopewa presha na watoa misaada kuchukua hatua kwa wezi.

Hivyo wafadhili kutunyima misaada si kuwaadhibu viongozi bali ni muendelezo wa maumivu kwa watanzania wanyonge ili wafanye maamuzi.

Kutunyima misaada si kuwaadhibu wezi bali ni presha kwetu ili tuwakamate wezi.

Tunayo mambo mawili ya kuangalia

1. Ama kuwasikiliza wezi na kuwaunga mkono ili tuendelee kuumia
2. Kuchukua hatua kwa wezi waliotuibia ili waendelee kutusaidia.

Uchaguzi ni wa kwetu.
 
Back
Top Bottom