Watanzania kwa pamoja tuungane kumsaidia Bi Hindu

The best 007

JF-Expert Member
Oct 6, 2019
13,529
2,000
Kwa mujibu wa familia, nguli huyu wa filamu na michezo ya kuigiza hapa nchini yupo kitandani kwa takribani miezi 9 ss, lakini inaonekana hajapata tiba stahiki ya maradhi yanayomsibu bibi huyu, binafsi nadhani Tanzania bado inamhitaji sn bi hindu, bado tunahitaji sn busara zake, tusisubiri mpaka maradhi haya yakapelekea umauti wake ndiyo tuanze kuchangishana mana umekua utaratibu hasa kwa nchi zetu za kiafrika mtu anapohitaji msaada wa matibabu anaangaliwa tu lakini pale anapokufa ndio utasikia sifa zake zikiambatana na michango mingi ya fedha, najua kama mwanadamu yapo ambayo atakuwa amekosea lkn hiyo ndiyo sifa ya mwanadamu kwani kukosea tumeumbiwa.

Kwa dhati ya moyo kabisa ningeomba watanzania tumsaidie legend huyu kwa hali na mali, uongozi wa klabu ya simba ikiongozwa na mwenyekiti wao Mo naomba mlichukulie kwa uzito hili jambo kwani huyu ni balozi mkubwa wa klabu ya simba, amechangia mengi katika kuijenga simba, binafsi ni mpenzi wa Yanga lkn bibi huyu amenigusa sn kwa namna moja au nyingine japo huwa ana maneno yake ya kishabiki hasa pale Yanga inapokutana na simba lkn huo ndiyo ushabiki wenyewe na huwa ananifurahisha sana.

Sijataja Simba kwa kumaanisha kwamba hili ni la Simba peke yao hapana, bali Simba wanapaswa kuonyesha uwepo wao katika hili kwa hali zote kuwa naye bega kwa bega ili kumfariji yeye binafsi na familia yake kwa ujumla. Ningependa kuiomba serikali iangalie pia namna ya kumsaidia bibi huyu kwa hali na mali kwakuwa bibi huyu ana mchango mkubwa katika taifa na jamii kwa ujumla, pia niwaombe wapenzi wa Yanga waonyeshe kuguswa katika hili kama walivyoonyesha kuguswa wakati wa ugonjwa wa Haji Manara kwakuwa michezo maana yake furaha na upendo.

Ewe Mwenyezi Mungu mjalie mja wako bi hindu afya njema apate kulitumikia taifa lake kwa kadri ya mapenzi yako, Ameen.

Naomba kuwasilisha.

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom