Watanzania kushangilia kuangushwa kwa Makonda katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni kunaashiria nini?

UTABIRI: Makonda anaandaliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma ili kuongeza kasi ya ujenzi wa mji huo. Hii yote ni kutokana na uwezo wake wa kusimamia mambo kwa kasi kwa kuwa Magufuli ana hamu ya kuona kwamba kabla hajondoka madarakani Dodoma inakuwa na sura halisi ya makao makuu ya nchi. Jambo ambalo litamjengea historia kubwa.
Lina ukweli,Ila ni Hadi ashinde October,siasa ni upepo sio hesabu chochote chaweza tokea.
 
UTABIRI: Makonda anaandaliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma ili kuongeza kasi ya ujenzi wa mji huo. Hii yote ni kutokana na uwezo wake wa kusimamia mambo kwa kasi kwa kuwa Magufuli ana hamu ya kuona kwamba kabla hajondoka madarakani Dodoma inakuwa na sura halisi ya makao makuu ya nchi. Jambo ambalo litamjengea historia kubwa.
Kutumia Kodi zetu kwenda kupendezesha dodoma then kusiwe na tija kiuchumi na kuacha vipaumbele muhimu vya kuchochea uchumi lengo tu ni kutafuta kukumbukwa ni matumizi mabaya ya Kodi zetu ni ubinafsi wa kiwango cha juu sana.
 
Kuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima

Hivi hali hiyo inaweza ikawa inaashiria nini?

Hivi inawezekanaje kwa mkuu wa mkoa, ambaye mara kwa Mara amekuwa akisifiwa hadharani na Rais Magufuli aliyemteua na kumtaja kuwa ndiye mkuu wa mkoa bora kabisa hapa nchini na wakuu wa mikoa wengine, wanapaswa waige mfano wa uchapaji kazi wa huyo Paul Makonda, wanaccm wa Kigamboni waamue kumnyima kura?

Licha ya malalamiko mengi sana ya wananchi kuwa Mkuu huyo wa mkoa hafai na kumwomba Rais Magufuli atengue uteuzi wake................

Hata hivyo Rais Magufuli amekuwa akiweka pamba masikioni na kutotaka kabisa kusikiliza maoni hayo ya wananchi, hadi wakati fulani aliwahi sikika Rais Magufuli akimwambia Mkuu huyo wa mkoa aendelee kuchapa kazi na asisikilize hizo shutuma zinazotolewa na wananchi walio wengi na akaendelea kumsifia kuwa yeye Makonda ndiye RC bora kabisa hapa nchini, ambapo maRC wengine wanapaswa wamuige yeye Makonda kwa.uchapaji kazi wake!

Je ni kiburi hicho alichopewa na Mheshimiwa Rais, ndicho kilichompa kichwa hadi kuwadharau watanzania wote hadi wakuu wake wa kazi?

Bila shaka wananchi bado hawajasahau lile sakata la namna mkuu huyo wa mkoa, Paul Makonda, alivyoweza kutunushiana "msuli" na waziri wa Fedha, Mheshimiwa Philipo Mpango, kuhusu yale makontena yake ya "fanicha" aliyotaka kuyaingiiza nchini bila ya kuyalipia ushuru, hadi pale Mheshimiwa Rais alipoingilia kati na "kumwamuru" mkuu huyo wa mkoa ayalipie ushuru stahiki makontena hayo

Kutokana na kiburi chake kilichopitiliza wananchi walifikia hatua ya kumbatiza cheo kisichokuwepo cha "Naibu Rais" wa Tanzania!

Hata hivyo wananchi wote wa nchi nzima, hatuna budi kuwapa pongezi wajumbe wa mkutano wa kutoa mapendekezo kwa Jimbo la Kigamboni kwa kufanya kazi iliyotukuka ya "kulikata" jina la Paul Makonda!

Ni matumaini ya wananchi wote kuwa kwenye vikao vilivyosalia vya juu zaidi vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, vitatia "tiki" uamuzi wa wanakigamboni na kutolirejesha jina la Paul Makonda kuwa ndiye mpeperusha bendera za ubunge kwa tiketi ya CCM na kuunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na wanaccm wa Kigamboni kuwa Faustine Ndugulile ndiye apeperushe bendera ya CCM kugombea ubunge huo baadaye mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapa nchini

Mungu ibariki Tanzania
Wengi wanamchukia Makonda kwa sababu ya wivu tu. Makonda sio lazima awe Mbunge hiyo ndio ilikuwa nia yake lakini Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema amependezwa zaidi afanye kazi nyingine. Ukiona nchi kubwa kama USA inadiriki kumpiga marufuku kwenda USA ati kwa sababu amekataa ushoga kuenea kwenye mkoa wa dar Es Salaam au madawa ya kulevya aliweza kupambana nayo lazima ufahamu kwamba alitimiza wajibu wake kuendeleza gurudumu la kuendeleza imani na tamaduni zetu. Makonda hawezi kukata tamaa atafanya kazi nyingine kama Mtanzania yoyote yule.

Kuvunjika kwa ungo sio mwisho wa kupepeta.
 
Makonda alichanga vibaya karata zake alikuwa anatakiwa Jimbo la Ukonga kule angeshinda sababu waitara alishakimbia Jimbo lipo wazi.Thus wameona wampe Jerry
 
Kura za maoni zisikupumbaze mimi naamini Makonda ndio mkuu wa mkoa bora kabisa kuwahi kutokea, ni kiongozi mwenye uthubutu na mwenye maono na anayependa kujaribu. Naamini kama Makonda akifanikiwa kuingia kwenye baraza la mawaziri na akapewa wizara ya kilimo ambayo imeajiri watu wengi basi kutakuwa na mapinduzi makubwa sana ya kilimo wakulima watanufaika sana

Nilichokigundua mimi ni kwamba kuna nguvu kubwa sana ya media hasa mitandao ya kijamii inatumika kuaminisha uma kuwa Makonda ni kiongozi mbaya, na hii ni kutokana na ujasiri wake uliochangia kuokoa vijana wengi wa Tanzania waliokuwa wakiteketea, sasa wanufaika wote wakahakikisha wanaelekeza nguvu zao kuhakikisha wanamchafua. Kiongozi mzuri hawezi pimwa kwa wingi wa kura pekee yawezekana wale wajumbe waliopiga kura za maoni wakawa sio wafuasi wake, lakini ikumbukwe wananchi hawapigi kura kwa kuangalia ufuasi, wao huangalia ni kipi kiongozi alichowafanyia au atachowafanyia, na kama hivi ndivyo ilivyo naamini Makonda anaweza shinda jimbo lolote lile ndani ya Tanzania kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ya kuokoa kizazi chetu hasa vijana . Ni binadamu wachache sana wenye uthubutu hapa duniani na hawa huwa ni tunu.
Kwa hiyo Marekani hawana akili kumzuia kukanyaga USA?
 
Samahani mkuu sijasema kwamba hamna akili naheshimu sana mawazo ya watu na wewe yakupasa hueshimu yangu, binafsi sioni makosa ya Makonda ambayo husababisha jamii kumchukia na wala jamii haimchukii Makonda kama baadhi ya watu wanavyojaribu kutuaminisha naamini kwa kazi alilizozifanya Makonda anaweza shinda jimbo lolote la Dar ikiwa kura zitapigwa na wananchi wa kawaida.

Mimi na tabia ya kumpima mtu kwa kazi zake sio majungu au prejudice. Tangu Makonda ameingia madarakani madawa ya kulevya yameisha Dar kam sio kupungua, wako wapi panya road, vipi kuhusu usafi wa jiji, vipi kuhusu kipindupindu Dar kipo tena? Sasa unaanzaje kumchukia mtu huyu?
Kwahiyo hayo yote uliyoorodhesha kama mafanikio una hakika ni kwa juhudi zake? Halafu mkuu yaani kama huelewi kwanini watu hawampendi basi umeamua tu kutoelewa, kama sivyo basi kuna tatizo la msingi.
 
Yaaan furaha haielezeki niliyonayo, tangu nmezaliwa sijawahi hata kunywa soda maan nna allergy na vinywaji vya viwandani,
Lakini leo nimedufua heinken nzima. ,
jamani sijui wajumbe wa CCM Kigamboni niwape zawadi gani wallah
Usiwape chochote kwa sasa mpaka baada ya vikao vya juu maana yule ni kipenzi cha Mwenyekiti wa hivyo vikao na ni homeboy. Awamu hii kila kitu kinafanikiwa kutokana na watu wanavyoamka siku ya tukio.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema.
Kiongozi akionekana na mama wa barabarani huyo hafai kuwa kiongozi. Aliyemchagua anatakiwa kuweka mtu mwingine badala yake bila hata kumjulisha.
Kuhusu Mh. Makonda, shutuma zilizokuwa zinatolewa kwake bila kujali ni za uongo au kweli na hasa za kielimu na zinazohusu uhai wa watu ni shutuma mbaya sana na zinaharibu image ya mtu mbele ya umma na hata kwa vizazi vijavyo.
Hakuna shutuma mbaya kama ya kumsingizia mtu kuwa anatoa uhai wa mtu mwingine. Ni ngumu sana kumsafisha na yeyote anayetoa tuhuma kama hizi ni ngumu pia kusema nilikosea.
Yaliyotokea kwa mh Makonda ni ajali ya Kisiasa kama ilivyomtokea Lowasa wakati wa Sakata la Richmond.
NI uongozi wa pamoja lakini inapotokea dosari ni lazima moja awajibike.
Pia hakuna jambo baya kama kiongozi kutumia kofia ya mkubwa katika kutawala watu ( kuwa na father god). Watu watakuheshimu kwa sababu ya uwezo wako katika utendaji kazi lakini watu watakuogopa kama unatumia madaraka ya Rais wa INCHI katika kuwatawala.
 
Mimi binafsi namkubali sana makonda,ni kijana ambaye ametuwakilisha vizuri sana . hao wanaomchukia ni wivu tu unawasumbua
 
Kwahiyo hayo yote uliyoorodhesha kama mafanikio una hakika ni kwa juhudi zake? Halafu mkuu yaani kama huelewi kwanini watu hawampendi basi umeamua tu kutoelewa, kama sivyo basi kuna tatizo la msingi.
Kwa juhudi za nani sasa mimi huwa sina prejudice napenda kiongizi anayejihusisha na matatizo ya wananchi moja kwa moja, mambo aliyefanya Makonda yaliwashinda viongozi wengi tu na ndio point inayombeba hayo mengine mimi kama mwananchi wa kawaida siyajui, mimi nazungumzia uwezo wake wakufanya kazi na kusimamia haki katika jamii anayoiongoza.
 
Back
Top Bottom