Watanzania kuonja shubiri ya mafuta ya taa wiki hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania kuonja shubiri ya mafuta ya taa wiki hii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Jun 29, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Watanzania kuonja shubiri ya mafuta ya taa wiki hii
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 28 June 2011 20:25 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Leon Bahati
  WATANZANIA wataanza kufaidika na punguzo la mafuta ya petroli na dizeli kuanzia keshokutwa kutokana na kuanza kutumika kwa sheria mpya ya punguzo la kodi iliyopitishwa bungeni wiki iliyopita.Pia, siku hiyo watumiaji mafuta ya taa wataanza kuonja shubiri ya bei kubwa ya bidhaa hiyo kutokana na serikali kupandisha kodi yake kwa Sh400.30 kwa lita.

  Hayo yamebainishwa katika mkutano wa wadau wa sekta ya mafuta nchini uliofanyika Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu, aliweka wazi jinsi mkakati huo utakavyotekelezwa.

  “Tayari sheria hiyo imepitishwa na kutangazwa kwenye gazeti la serikali na itaanza kutumika rasmi Julai Mosi (kesho kutwa),” alisema Masebu.
  Aliweka wazi kuwa kodi inayotozwa kwenye mafuta ya dizeli itapungua kutoka Sh314 hadi Sh215, hivyo bei mpya itapungua kwa wastani wa Sh100 kwa lita, wakati kwenye mafuta ya taa kodi imeongezwa kutoka Sh52 hadi kufikia Sh400 kwa lita.Kulingana na takwimu za mkurugenzi huyo, punguzo la mafuta ya dizeli ambayo Dar es Salaam inauzwa kwa wastani wa Sh2,000 inatarajiwa kushuka kufikia kadirio la Sh1,900 kwa lita.

  Takwimu hizo zinaashiria bei ya mafuta ya taa itaongezeka kutoka Sh1,500 kwa lita hadi kufikia Sh1,900 kwa lita, bei ambayo haitakuwa na tofauti na ile ya petroli na dizeli.

  Kwa mujibu wa Masebu, bei ya mafuta ya taa itakuwa chini zaidi ya ile ya dizeli kwa wastani wa Sh15 kwa litaMasebu alifafanua kuwa lengo la serikali la kupandisha kodi ya mafuta ya taa siyo kuwakomoa watumiaji wa bidhaa hiyo inayotumika kwa wingi, hasa maeneo ya vijijini wanapoishi Watanzania wengi na ambako hakuna umeme, bali ni kukabiliana na tatizo la uchakachuaji mafuta.

  Alisema tatizo kubwa la uchakachuaji lilikuwa likifanywa na wafanyabiashara kwa kuchanganya dizeli na mafuta ya taa, wakati huo serikali ikiwa inatoza kodi kidogo kwa bidhaa hiyo inayotumiwa na sehemu kubwa ya Watanzania ambao ni maskini."Kwa sasa bei ya mafuta ya taa haitatofautiana sana na ya dizeli," alisema Masebu akifafanua kuwa anatarajia bei ya mafuta ya taa itakuwa chini kidogo.

  Kulingana na utaratibu uliowekwa na Ewura, Masebu alisema punguzo hilo litafanyika kwa awamu mbili, Julai Mosi na Agosti Mosi, mwaka huu.
  Masebu alisema awamu ya kwanza itatokana na mafuta yanayouzwa nchini kushuka bei kulingana na kupunguzwa kwa kodi kwenye mafuta na awamu yapili itazingatia gharama za uagizaji mafuta wa pamoja.

  Mchakato wa kuelekea kwenye mkakati wa wafanyabiashara kuagiza mafuta kwa pamoja, utaanza Jumatatu ijayo na watachagua bodi ya usimamizi ya watu sita miongoni mwa wafanyabiashara.Masebu alisema bodi hiyo itashirikiana na serikali kupanga bei na kuchagua zabuni kwa wafanyabiashara watakaoonyesha uwezo wa kununua mafuta kwa pamoja.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  watumiaji wakubwa wa mafuta ya taa ni hasa maeneo ya vijijini wanapoishi Watanzania wengi na ambako hakuna umeme
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  huu ni wehu.watumiaji wa mafuta ya taa ni hasa maeneo ya vijijini wanapoishi Watanzania wengi na ambako hakuna umeme
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  imepitaaaaaaaa.lol!
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Mimi nilishaitangazia familia yangu The state of emergence tangu Janualy, kwahiyo hakuna kipya kwangu najihesabu ni sawa na mkimbizi tu ndani ya nchi yangu, na hili jambo linanifurahisha mno maana ccm huwa inapigiwa kura na watu maskini wa kutupwa, sasa wacha wapate displin ndio watakuwa na akili. na watajuwa nini maana ya kura, na nini ubaya wa Tshirt na kofia za magamba.
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Hizi ni shida za kujitakia.

  Halafu unaweza kumpata huyu dada zaidi hapa.

  • [​IMG]Lisa M Rockefeller
   Tanzania, Tears of Thee......How can these irresponsible regimes survive for so long? If Tanzania cannot uprise against Kikwete's regime, then their condition will never change. Bombs will always explode. RIP the victims of Bongo-La-Mboto.

   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Hapa sasa hakuna unafuu wa maisha...
   
 8. M

  Mwadilifu Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si kweli kuwa waishio vijijini ndo wa2miaji wakubwa wa kerosene,mijini 2na2mia sana 2,kwl hii ndo best way kupigana na uchakachuaji? At z xpense of majority?
   
 9. K

  KWELIMT Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  EeehWanaJF kuongeza bei ya mafuta ya taa 1500 hadi 1900 ni nafuu kweli kwa mlala hoi wa vijijini au kwa wafanyabiashara? Mwaka jana nakumbuka kuna mbunge (sikumbuki wa chama gani) alisimama bungeni akatoa huo ushauri wa kuongeza bei ya mafuta ya taa naona huo uamuzi ndiyo utekelezaji wenyewe.

  1.ILA MIMI NAONA NI UAMUZI USIOJALI MANUFAA YA WENGI,AU SERIKALI KWENYE KUMBUKUMBU ZAKE INAJUA TZ NI DSM ambako watumiaji wa mafuta si wengi kama maeneo ya vijijini?

  2.NA HUU MGAO WA UMEME,WANANCHI HATA WA MJINI TUTAPONA NA HII ONGEZEKO?Au ndiyo wafanyabiashara wa mafuta wafaidike huku walalahoi wakiendelea kulia na kupanda kwa gharama za maisha?IKO WAPI DHAMIRA YA SERIKALI YA KUWAPUNGUZIA WANANCHI UGUMU WA
  MAISHA?

  3.KWELI WABUNGE WETU WAMEKUBALIANA NA HILI WAZO LA SERIKALI KWA MANUFAA YA NANI?yaani nchi hii mlalahoi hana nafasi,kama bei ilivyokuwa 1500 koroboi ndo ilikuwa zetu,1900 tutatumia nini?tunarudishana zama za kale jamani.............Aah! Waheshimiwa wetu wameunga hoja MIA kwa MIA,ila itakula kwao 2015.

  4.SIUNGI MKONO UCHAKACHUAJI WA MAFUTA KABISAA,LAKINI OPTION NDIYO HIYO PEKEE?Siamini kama ni sahihi kwa EWURA WANGEWEZESHWA ZAIDI ili wawe wanakagua mafuta kwenye vituo kuangalia kama yanachakachuliwa.mi si mtaalamu sana wa mafuta lakini naamini wataalamu tunao wangepewa nafasi wangetusaidia sana kutafuta njia mbadala ya kudhibiti uchakachuaji.

  ENYI WAHESHIMIWA WETU HUKO DODOMA NAAMINI KWELI MWENYE SHIBE HAWEZI KUJUA MAANA YA NJAA.MTAWAAMBIA NINI WAPIGA KURA MAJIMBONI MWENU KUWA MMEPANDISHA BEI MAFUTA YA TAA KUWAKOMOA WAFANYABIASHARA WACHAKACHUAJI AU WAO WAPIGA KURA?

  EE MOLA TUNAKUOMBA ULIBARIKI BUNGE LETU TUKUFU ILI UWAONGOZE,UWAPE UJASIRI,HEKIMA NA BUSARA WAWEZE KUJADILI MATATIZO YA WANANCHI KWA TAFAKURI YA KINANA BILA UNAFIKI.ameni.

   
 10. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu ni kweli kabisa. Mimi naishangaa Serikali yetu yaani Wameshindwa kabisa kuzibiti uchakachuaji wa mafuta mpaka? Nakumbuka Jk alipoingia madarakani alikuja na azimio la kuondoa matumizi ya nishati zote zinazotokana miti (Mkaa na Kuni), hapo serikali ikato ruzuku ya mafuta ya taa ili yawe bei chini. Leo tunaambiwa kuwa mafuta ya taa yanatumika sana ktk uchakachuaji hivyo bei yake iwe juu, Je hawa Ewura kazi yao ni nini? Na lile azimio la kuondoa matumizi ya mkaa limeishia wapi? Sijui lini tutakuwa na Serikali makini maana sioni jipya hapa zaidi ya wao kujikanyaga.
   
 11. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  jaman jaman jaman hii serikal tetu inakwenda wap, mbona kila siku inazidi kuumiza watanzania? hiv kweli serikali inapokaa na kuamua kupunguza kod ya petrol na diesel na kuongeza kod kwenye mafuta ya taa inamaanisha nin, watu wa vijijin watatumia nn maskin! hebu jaman serikal wakae na kutafakari hili jambo, watanzania wanaumia sana sio siri kutokana na mfumo wa usimamizi wa mambo mbalimbali wa serikal yetu. kingine ni kwamba katika hali ya kawaida huwez ukasema umepunguza bei ya petrol kwa Tsh 100 halafu ukasema utaleta unafuu wa maisha kwa Watanzania, huu ni utani tena utan wa kupigana ngumi za uso live. Kwa utaratibu huu kwa kweli haya ndo maendeleo? au kudhihak Watanzania. Rais kikwete kaza buti rais wetu baadhi ya wasaidiz wako wanakuangusha Mr. President
   
 12. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Watanzania wenzangu nchi hii ni wafanyabiashara kwa sababu hata viongozi ni wafanyabiashara na si wakulima.Ikumbukwe kwamba TZ wafanyabiashara wa mafuta ni wachache ukilinganisha na wananchi wa kawaida.Kwa kuwa serikali ipo ICU imeshindwa kuwadhibiti wafanyabiashara ili waache uchakachuaji badala yake njia rahisi kwao ni kukandamiza walalahoi.Kwamba watapunguza diesel na petrol ni kiini macho ,bei haitapungua lengo lao likikamilika bei zote zitakuwa sawa 2000-2500 kwa lita.Serikali ya Tanzania inaendeshwa na kodi za maskini wanaponunua bidhaa na kodi ya wafanyakazi,hivyo haitatokea hata siku moja mtanzania ataishi maisha bora ni viongozi na wafavyabiashara wataendelea kutanua.Watu tuamke tuache uvyama ,tuungane kudai haki.
   
Loading...