Watanzania Kuomba ni Asili Yetu Wala Tusimlaumu JK Kwakuomba Misaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania Kuomba ni Asili Yetu Wala Tusimlaumu JK Kwakuomba Misaada

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndallo, Feb 7, 2012.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Hii nimejaribu kufuatilia kwa kina sana ili nijue ni nini asili ya sisi KUOMBA! tumemshuhudia Raisi Kikwete kila kukicha yeye ni mguu na njia kwenda kuomba misaada! Katika kufuatilia kwangu kwa kina ili nijue ni nini asili ya Watanzania neno kuomba ni asili yetu hembu angalia hii:

  Mteja anaingia Hotelini au dukani:

  Mteja - Habari za saa hizi?
  Muhudumu - Nzuri.
  Mteja - Naomba Menu! - Anapewa Menu
  Mteja - Naomba Chai - Anapewa Chai.
  Mteja - Naomba Kulipa - Analipa
  Mteja - Naomba Change - Anapewa Change

  Hapa ni mfano kidogo tu ambao nimeupata simaanishi kua ni lazima tutumie ubabe kwenye kuagiza au la! lakini naona hii ni hulka ya sisi kila kitu ni kuomba kuomba sijui na wenzangu mnamtazamo gani kwenye hili. Nawasilisha.
   
Loading...