Watanzania kumbe tunaogopa tu kutembelea vivutio vyetu vya utalii

Mar 12, 2016
71
125
Watanzania kumbe tunaogopa tu kutembelea vivutio vyetu vya utalii. Tukisingizia gharama kumbe si kweli.

Nimekuja Serengeti, nimelipa 11,800 pamoja na VA, m'bongo ni nafuu mno. Mgeni kutoka USA niliyekuwa naye kalipa dola 70, km Tsh.laki na elfu 54.

Swali ni je? Watz tunaogomba nini kutembelea vivutio vyetu vya utalii japo mara moja kwa mwaka?
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
3,244
2,000
E
Watanzania kumbe tunaogopa tu kutembelea vivutio vyetu vya utalii. Tukisingizia gharama kumbe si kweli.

Nimekuja Serengeti, nimelipa 11,800 pamoja na VA, m'bongo ni nafuu mno. Mgeni kutoka USA niliyekuwa naye kalipa dola 70, km Tsh.laki na elfu 54.

Swali ni je? Watz tunaogomba nini kutembelea vivutio vyetu vya utalii japo mara moja kwa mwaka?
Embu weka mchanganuo wote wa kiingilio,usafiri na pengine accomodation(atleast utembelee mbuga mbili/siku mbili)
 

G.25

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
1,290
2,000
Watanzania sio kama hatupendi kutembelea vivutio vyetu ila hata hatujui maana ya kutalii, hii wizara imelala sana, unavoona hivi ndani ya nchi....nje ya nchi imezorota zaidi" tuna vivutio Vingi kuliko nchi jirani lakini wao wanauza zaidi kuliko sisi!
Hizi wizara na mawaziri wake huwa siwaelewi.
MF. wizara ya nishati na madini. Eti kuna madini yanayochimbwa tz lakini kwenye stock ya hayo madini na ndo muuzaji mkubwa ni nchi flani! Eti kwenye shirika kuu la nishati ndo kwenye ufisadi wa kutisha!

Hivi wanasimamia wizi na uzembe? Faru tu, ona wanavomsumbua waziri mkuu! Hawa mawaziri ni v....za!
 

Copenhagen DN

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
6,054
2,000
MSOS TU ANASA. IKITOKEA UMEFULULIZA KULA NYAMA KILA SIKU UNAITWA FREEMASON. UKIOGA MCHANA UNAULIZWA UNAKWENDA WAPI?

Kwa tabia hiyo nani atembelee hivyo vivutio?Utaambiwa ooh unaringa, unajifanya na kuiga wazungu.
 

Kalamu Yangu

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
1,031
2,000
Nikashangae nyumbu wakati tunao mitaani tena wa rangi tofauti;Kijani njano na kaki..
Simba wapo kibao yupo yule wa Wasafi,Mr Blue naye simba,Yule aliyekuwa ACT naye simba.
Tembo tumamwona kwenye noti muda wote achana na faru...

Hiyo elfu kumi naweka ya kwenda kwenye Darasa la Fursa


Ila kweli huwa tunatishwa tuu kwa kuhisi nasi tutalipa bei za watu wa nje ya Tanzania,pia gharama za hotel za huko mbugani huwa tukiziona kwenye Mitandao zinatunyong'onyesha...
Lakini pia bado utalii si hulka yetu wengi tunakaririshwa "Utalii huongeza pesa za kigeni" basi mtoto anakuwa akiamini hadi awe na hizo 'za kigeni'.
Bajeti zisizotengemaa miongoni mwetu hatuna, tunatafuta ya kula leo na kesho basi , hatuna vile vibubu kama vile vya nauli za kwendea Moshi.Kwani hao wageni huwa wanakusanya na kutafuta hela maalum kwa ajili ya kufanikisha hilo...

Mwisho wanyama wanabaki kuwa kitu kisichovutia kwa wengi bali kutisha, mfano imeshajijenga akilini simba na chui huua basi usitegemee mtu atafurahia kwenda kutazamana na kiumbe muuaji tena kwa kulipia Utasikia....wabongo si wa kuwaamini simba anaweza kukurukia ukawa kitoweo chake..

Vitu kama milima na sura mbalimbali za nchi zivutiazo bado havijapewa ule uajabu na upekee wa kuwavutia...
Tupo radhi kwenda kumshangaa Rama Mlawatu kuliko kushangaa Maporomoko ya maji ya Marangu...
 

Kishada04

JF-Expert Member
May 1, 2016
955
500
Tatizo serikali imeshindwa kuhamasisha watanzania kufanya utalii wa ndani pamoja na umasikini.
 

ANCIENT FROM EGYPT

JF-Expert Member
Oct 24, 2015
722
1,000
Picha akipiga Mzungu Mtalii....ila ukipiga mbongo..anaulizwaaa....,unazipeleka wapi sura zetu...... sasa leo tunazungumza habari za watu kutokwenda Mbugani..wakati mwalimu wa historia Tabora hajui kama Kipalapala Kuna makumbusho ya Kwihala. achilia mbali mwalimu yupo Mtwara Hajui kama kuna makumbusho ya Makuya,achilia mbali mwalimu yupo Songea..mishipa imemkaza kufundisha majimaji War wakati makumbusho yapo pale. sehemu nyingi zina vivutio vingi vya utalii. na tumekalilishwa kuwa utalii mpaka mbugani wakati hata upishi wa vitumbua ni utalii tosha kama ukipewa mikakati. hata maonyesho ya vyakula vya asili ni Utalii. TUAMKE
 

INGENJA

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
5,004
2,000
Bado nighali sana kutembelea mbuga za wanyama kiingilio si issue ila transportation na accommodation ndio issue kwa harakahara unaweza kutumia 1.5m kukava transaportation na accommodation
 

GREGO

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
4,173
2,000
Sio utamaduni wetu.
Ova.


Waulize watu wa Bagamoyo wangapi wamefika Kaole Ruins
 

pachachiza

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
1,688
2,000
Nyie mnadhani gharama ya uko ni kiingilio tu, jiulize toka Dar mpk Serengeti nauli kiasi gani, gharama za malazi uko, gharama za kukodisha gari ya kwenda ndani ya mbuga, gharama za muelekezaji ndani ya mbuga. Ukinipa mchanganuo wa gharama hizo ulinganishe na kipato cha mwananchi wa kawaida km anaweza kufanya safari moja na familia yake.
 

TEAM VIBAJAJI

JF-Expert Member
Oct 9, 2016
1,856
2,000
Basi tukishindwa serengeti karibuni kisiwa cha saanane kilichopo jijini Mwanz pale garama ninafuu
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,921
2,000
Maisha yenyewe ya Mtanzania ni utalii tosha, sasa Mbugani nikafanye nini?
 

kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,318
2,000
Juhudi zinazofanyika bado hazijawesha kuamsha ari ya watu kujivunia kutembelea hifadhi zetu.

Wengi huchukulia hayo ni mambo ya watu wenye pesa tu lakini naamini watu wangeweza kuwa wanajipanga kwa makundi na kwenda gharama hupungua kwa kugawana (kushare).
 

124 Ali

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
7,603
2,000
Nyie watu acheni kejeri bwana!pesa ya andazi shughuli ndio nitaweza kwenda huko kuangalia vitoweo
 

VeroEretico

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
389
500
Watanzania kumbe tunaogopa tu kutembelea vivutio vyetu vya utalii. Tukisingizia gharama kumbe si kweli.

Nimekuja Serengeti, nimelipa 11,800 pamoja na VA, m'bongo ni nafuu mno. Mgeni kutoka USA niliyekuwa naye kalipa dola 70, km Tsh.laki na elfu 54.

Swali ni je? Watz tunaogomba nini kutembelea vivutio vyetu vya utalii japo mara moja kwa mwaka?
Naoomba ujibu swali la GeoMex kuhusu mchanganuo wote atleast siku moja
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom