Watanzania kuleni nyama ya panya ina vitamini adimu mwilini

hivi na nyama ya Mbwa ina vitamini? maana kuna dog nyingi hapa mtaani kwetu..
 
Nimekuja mbio nikijua nishapata kipato cha ziada!! Maanake hawa walioko nyumbani kwangu usiku darini utafikiri wamevaa safety boots!! Wanakimbiza hadi kuku wangu!! Hivi mkuu hawa wa kawaida hawafai kwa kitoweo??
 
Nyama ni nyama tu karucee, ya kuku ya panya zote sawa,
Vegetarian nawaelewa hawali nyama yoyote, sasa ww mwenzangu unakula cow kuku etc.afu unanyanyapaa ya panya, they're all secondary production wanakula majani ndio stake zinatokea, sio sumu best u should try, me nishakula nyoka mamba, tamu sana, nyama zao ni white meat kama samaki, ikikorombezwa poa ukaiona, mate yanakujaa
 
Kumbe kuna watu hawali kabisa ndezi!
Hao wadudu nimewala sana si wa kubanika wala wa kupika.
Tena wale wa kupika unatupa manyoya tu na baada ya hapo unatia nyama sufuriani au chunguni kisha unachukua ule utumbo wenye mavi unaminyia pale juu ya nyama, basi yale mavi yanaleta mchuzi mzito wenyewe tunaita mtwabu (yaani mavi baada ya kuchemka yanatengeneza chuzi zito kama la alizeti au karanga)
Ukila nyama ya ndezi huachi, ni sawa na kula nyama ya noah, utaendelea kula tu.
 
Ndezi wananyama tamu balaa wana majina mengi jina lingine mashuhuri ni SWAVA, Shida ni kwamba ukuanza kuwafuga maliasili wanakukanata siku hiyohiyo
 
Hizo nutrients alizonazo ina maana hazipatikani kwenye chakula kingine chochote?
Mie nizikose tu!!!
 
Ndezi siyo panya, ni jamii yao lakini wana tofauti kubwa sana hawa wanakaribiana karibiana na sungura BTW nlivyokua Ntwara walikua wanawala wale wa porini kabisa I was like heeeeellll noooool!!! ndezi na wle simbilisi nitajaribu ila siyo panya aiseeeeee....
 
Chamaki nchanga ni noma mm kila nikiibuka pande za home lazima nipige hiyo kitu ukifika Ndanda uliza mkorosho haramu wapo kwa wingi bei nafuu

ha ha ha ule mkorosho ulikaushwa kwa mafuta ya panya na nguruwe.,Ila panya ni mtamu bradha
 
Wachaga walikuwa wanamla sana ndezi,wanamuita KIPOPORU

Weeee acha uongo na kuku ngombe, mbuzi, noah, kondoo woote waliojaa kule waache kuwala waje wale huo uchafu kwanza kwenye makulaji hamna watu waojua kula vizuri kama wao embu tutake radhi.
 
Back
Top Bottom