Watanzania kamwe tusitende dhambi kwa kumbeza kikwete ametusaidia sana katika hili... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania kamwe tusitende dhambi kwa kumbeza kikwete ametusaidia sana katika hili...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Mar 12, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanaJF,

  Inawezekana wengine wamefungua thread hii wakiwa wamefura kwa hasira baada ya kusoma title. Lakini ukisoma kwa umakini ninachotaka kueleza bila shaka hasira zitapungua au kutoweka kabisa.

  Tangu tupate uhuru takriban miaka 50 iliyopita nchi yetu imekuwa ikiongozwa na serikali ya chama kimoja cha siasa yaani chama cha 'mapinduzi!' chini ya awamu nne tofauti. Awamu ya kwanza alikuwa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere, awamu ya pili Alhaji Mzee Mwinyi, awamu ya tatu Mzee Mkapa na awamu ya sasa ya nne ni Kijana(?) Kikwete. Kwa ujumla, watanzania wengi hawafurahishwi na kasi ya nchi kuelekea katika neema ya maendeleo makubwa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Pamoja na upatikanaji wa rasilimali nyingi ambazo ndiyo chachu ya maendeleo, lakini chini ya uongozi wa ccm nchi yetu imeendelea kuwa maskini tena maskini wa kutupwa.

  Wengi wetu (ikiwa ni pamoja na Hayati Mwl. Nyerere mwenyewe) tumekuwa tukitamani sana ifike siku moja ccm iondoke madarakani ili tupate mawazo mbadala ya kuongoza nchi yetu kuelekea katika maendeleo ya dhati. Pamoja na matamanio yetu hayo ilikuwa vigumu kidogo kufikiria kwamba kweli ipo siku ccm itadondoka. Ilikuwa kama ndoto vile!Lakini chini ya uongozi wa kikwete kama rais na kama mwenyekiti wa ccm, kwa mbali naona kama ndoto inaweza kutimia.

  Kwa ujumla, nchi yetu sasa ipo kwenye vuguvugu la kimapinduzi. Kwa kuangalia mwenendo wa serikali na chama tawala, sasa ni dhahiri kwamba wakati wowote kunaweza kutokea mabadiliko makubwa ya kisiasa hapa nchini. Mabadiliko hayo yataambukiza mabadiliko kwenye masuala ya kiuchumi na kijamii. Yote haya mwanzilishi wake ni kikwete na sifa zote anastahili apewe yeye. Akiwa mwenyekiti wa ccm kikwete alimteua mzee makamba kuwa katibu mkuu wake. Alichofanya babu huyu kwenye chama wengi wetu tunafahamu. Amekigawa chama katika makundi mbalimbali yanayokinzana kila kukicha. Ni kikwete huyu huyu aliyekitelekeza chama na kuamua kutumia familia yake ishike usukani katika kampeni zake za kurejea madarakani. Ni kikwete huyu huyu aliyeunda serikali ya kirafiki na kusababisha uongozi wa nchi kuyumba huku mafisadi wakiendelea kutamalaki. Chini ya uongozi wa kikwete watanzania wengi wameweza kuamka kutoka usingizini na kuona umuhimu wa mabadiliko ya katiba ya nchi.

  Sasa jamani katika hali kama hii, kwa nini tutende dhambi ya kubeza mchango mkubwa wa kikwete wa kutupeleka kwenye ukombozi wa kweli? Tafakari.
   
 2. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,174
  Trophy Points: 280
  HATA YANAYOONEKANA KUWA MAZURI AMEYAFANYA KWA BAHATI MBAYA, believe or not!
   
 3. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama yapo!
   
 4. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  CCM wameshamaliza kazi yao ya kuleta uhuru, kuijenga hii nchi kiuchumi hawawezi, hili halikuwa lengo la kuanzishwa kwa vyama vilivyoiunda, tunahitaji chama kingine kwa kazi mpya ya kutuletea maendeleo.
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280

  Umenifanya nicheke sana, tena sana, mh. CCM ni wakoloni wengine baada ya waingereza waliofuatia ni CCM, haijaleta uhuru, hakuna uhuru,history will dispute that statement.
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  naunga mkono hoja.

  tatizo lake ni kuruhusu baadhi ya wahindi na waarabu kuigeuza nchi yetu shamba la bibi.

  kwa hilo sitamsamehe kamwe.
   
 7. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tehe tehe kazi ya kiongozi ni kuonesha njia, anatakiwa na vision ni wapi anawapeleka wale anaowaongoza. Kwa bahati mbaya ndani ya miaka 5 kama taifa tumelikosa hilo, na hii itakuwa pia kwa mingine 5 ijayo.

  Hii ni hasara kubwa sana kwa taifa kuwa na ombwe la ki-uongozi ndani ya miaka 10; hatuna jinsi ya kuweza kuurejesha muda huu kabisa.
   
 8. U

  Uswe JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  na kwa kuchagua wakuu wa wilaya kama yule wa manyoni jk amefanya watu watambue zaidi ye ni mwanaume wa aina gani
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kunguru anapo'mchafua' mtu haimaanishi kuwa kunguru ana shabaha bali ni bahati mbaya tuu imetokea.
  Ndio Serikali ya Kikwete ilivyo.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  this must be a joke! Yaani wewe unachojaribu kusema ni sawa na kumshukuru mtu aliyeleta Aids kwa sababu imetufanya tuelewe mabaya ya ugonjwa huo ktk zinaa...

  Mkuu wangu hakuna mtu aliyetaka CCM itoke madarakanikwa sababu tu wananchi wanataka mageuzi. Kama CCM ingekuwa na viongozi wazuri, sera nzuri zitakazotuletea maendeleo vizuri sidhani kama tungetaka iondoke madarakani kwa sababu tu wananchi wameichoka.

  Na sidhani kama Nyerere alikuwa na maana hiyo ama wananchi kwa ujumla isipokuwa hali halisi ya udhaifu ktk Uongozi na kutokuwa na dira ndio imetufikisha hapa..

  Nyerere aliwahi sema ili nchi yetu iendelee tunahitaji vitu vinne -Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi bora, sasa maadam tumepoteza vitu viwili yaani siasa safi na Uongozi bora, Kikwete ni ushahidi wa matokeo ya virusi vya HIV kiuchumi vilivyotuambukiza gonjwa hili la Aids yaani umaskini.

  Na maadam Tanzania hii ni nchi maskini.. HIV imeshakuwa Aids in full swing, hakuna njia ya kupata ponya isipokuwa kwa kudra za Mungu kumpata mganga kama yule wa Loliondo kujenga tumaini jipya la kiroho, ndio tunaweza ondokana na umaskini na wala sii leo wala kesho. Vita yetu kubwa ni kupata tumaini jipya...

  Binafsi sitegemei Chadema wala CUF wanaweza kutuondoa ktk umaskini isipokuwa vyama hivi vinaweza kuboresha sehemu muhimu za maendeleo kama vile kurudisha umuhimu wa siasa safi na Uongozi bora vitu ambavyo tumevipoteza toka Azimio la Zanzibar. Azimio ambalo liliruhusu ngono bila kutumia kinga a.k.a free market economy baada ya kuondoa miiko na maadili ya viongozi...Hapa ndipo makosa makubwa yalipofanyika.

  JK ni tunda la kile kilichopandwa kwani yeye ni reflection yetu sote kama sii viongozi wenzake.. Taifa limeoza na Ufisadi, waswahili wanasema ukiona baniani kahamia mji fulani jua kuna wajinga wengi..leo hii CCM imejaa Baniani.
   
 11. n

  ngoko JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli sisiem wamemaliza kazi yao maana mkuu wao ametamka wazi kuwa Maisha bora kwa Kasi zaidi, Nguvu zaidi na Ari zaidi hayawekani maana mzee nyerere , mzee mwinyi na mzee Mkapa waliacha haya magumu ya maisha hivyo naye atayaacha , kwa maana nyingine kauli mbiu ya uchaguzi ilikuwa ya kuombea kura majukwaani lakini amekiri kuwa haitekelezeki .
   
 12. M

  Mindi JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono asilimia mia moja! Ni kikwete aliyeweza kufanya kile ambacho ni Nyerere tu alikiweza: Kuwaunganisha watanzania wafanye kitu! ila kwa mielekeo tofauti. Nyerere aliweza kuwaunganisha watanzania, kwa kiwango kikubwa, in a positive way. aliweka vision, akawajibika yeye binafsi, hakuwa mbinafsi wala fisadi wala kuwalinda mafisadi. akatuunganisha. Kikwete, yeye anafanya hilohilo lakini kwa kinyume cha Nyerere. Hana vision, sina hakika kama ni fisadi au sio fisadi yeye binafsi lakini anawalinda sana mafisadi. hana maamuzi, hajui kitu chochote, kama alivyosema mwenyewe:
  -sijui Dowans
  -sijui kama siwajui Dowans
  -sijui chanzo cha umasikini wa Tanzania
  -Sijui kama sijui umaskini wa Tanzania
  -sijui kama hali ngumu ya maisha
  -sijui kama bei zinapanda kila siku
  -sijui chochote

  kwa hayo yote, Kikwete amefaulu kuwakasirisha watanzania kiasi kikubwa sana na sasa taratibu wanaungana na kuwa na kauli moja. ni process ndefu lakini tunakokwenda ndio huko. wale wanaomtetea ama hawajamuelewa vizuri, ama hawataki kuamini kile wanachokiona mbele yao, ama wanadhani wanawekeza ili pamoja na udhaifu wake, akikupa ka cheo si mbaya sana! lakini kwa kuwa Kikwete ndivyo alivyo na hatabadilika, taratibu sote tutamwelewa na kuungana dhidi yake na dhidi ya marafiki zake. big up JK! Mission accomplished!
   
 13. m

  mzambia JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Jamani tungoje aka nyingine tano tena.
   
 14. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni dhahiri kabisa na kutoka kla sehemu ya viungo vyao wanakiri hilo,ya kwamba ni kauli ya kuombea kura tu basi,.lami kuzungka klm
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  CCM hawakuleta uhuru, usilete porojo, ccm imeanzishwa lini? "uhuru" umepatikana lini?
   
 16. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Uko sahihi kabisa Mkuu!
  Labda pia tujiulize, hawa Mafisadi wakuu kama Rostam wamembana wapi JK? Mbona anawaogopa sana? Hivi kweli hizi ni fadhila tu au kuna zaidi?
  Mshikaji yupo tayari kuandika historia yake kwa kuonekana rais mjinga zaidi duniani lakini asimguse Fisadi! Au ana hisa ktk mikataba yote mibovu na uovu mwingi ambao Rostamu akiamua kuuweka wazi ameumia?
  Katika nchi kama hii huwezi kuwaamini hawa watu.
  • Thijui Rothtamu ni nani.
  • Thijui Kagoda ni nani na wala petha dha kampeni nilitoa wapi.
  • Thijui kama Raith anapathwa kujua.
  • Thijui kama Uthalama walinithaidia kuchakachua.
  Ktk hali ya kawaida kiongozi wa nchi hawezi kukubali anonekane hana akili kiasi hiki na hayuko in Control kwa ajili ya rafiki zake wawili au watatu tu. Jamani JK ana siri nzito na tukichunguza tutazijua tu siku moja.
  Mbona Rostam haogopi?, mbona uamuzi wa Bunge dhidi ya watumishi wa Umma waliohusika na kuficha aibu ya Richmond hawaguswi?
   
 17. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Big up mtoa hoja. Ni kweli Kikwete anastahili pongezi kwa hili. Pongezi huwa hazitolewi kwa mambo mazuri pekee ila hata kwa yale yanayomwangamiza mhusika huku yakitoa ahueni kwa adui zake. Kuvurunda kwa Kikwete kumetoa fursa nzuri kwetu sisi ya kuyasaka mageuzi na maendeleo ya kweli. Shime Watanzania, wakati ndio huu, tuutupe ukoloni mamboleo wa CCM
   
 18. V

  Vipaji Senior Member

  #18
  Mar 12, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja kwa sababu wanasisiemu bado wanaamini kuwa "Uhuru ni Kazi ya TANU" lakini maendeleo sio kazi yake walidhani ingekuwa kazi ya CCM lakini matokeo yake CCM ikajichahkachua yenyewe kwa kuweka WANAMTANDAO MAFISADI. Umefika wakati wa sisiemu lazima iondoke haraka madarakani kabla wananchi hawajaiondoa
   
 19. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  TANU ni kati ya vyama vilivyoleta uhuru na ni mojawapo ya vyama vilivyounda CCM, na malengo na madhumuni ya kuanzishwa TANU yakahamia CCM, sasa unabisha nini
   
 20. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Absolutely!
   
Loading...