Elections 2010 Watanzania jiandaeni kwa kipindi kigumu cha miaka 5 ya ufisadi

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Naanza kuandika hii thread nikiwa na huzuni kubwa sana. Najiuliza sipati jawabu kwamba imekuwaje na nini kimetokea kwenye Uchaguzi wa mwaka huu.

Kwamba eti Watanzania milioni 5 wamekubali tena kuipa ridhaa serikali ya mafisadi iendelee kuwatawala kwa miaka mingine 5 ijayo. Sielewi na sipati jibu!

Kwamba serikali iliyoingia madarakani mwaka 2005 ikakuta kilo ya sukari ikiuzwa TSHS.500/= na leo mwaka 2010 kilo hiyo hiyo ya sukari inauzwa Tshs.1800/= sawa na ongezeko la 360%. Hii ina maana kwamba in another 5 years to come kilo ya sukari itakuwa inauzwa Tshs.6400/=! Hiyo ndiyo serikali ambayo Watz wamekubali kuipa ridhaa iwaongoze for another 5 years. Yaani sielewi.

Serikali ambayo tumeshuhudia ikiendeshwa kifisadi kwa kukwapua fedha zetu kwa mabilioni toka Benki kuu(Reserve Bank) huku sisi walipa kodi tukiendelea kunyanyasika na kuishi maisha ya kubahatisha.

Seriakli ambayo wakti inaingia madarakani 2005 iliahidi MAISHA BORA kwa kila Mtz lakini badala yake maisha yamegeuka kuwa MAISHA BOMU(refer Lipumba's speech ya kufunga kampeni). Hakika ni maisha Bomu au lugah nyingine yanaitwa Bora Maisha!

Serikali ambaye imeshindwa kukuza uchumi wa Taifa badala yake tunashuhudia mfumko wa bei ukipamba moto kila siku. Mwaka 2005 US Dollar 1 ilikuwa Tshs. 800/= leo hii Dollar moja iko kwenye Tshs.1550/=. Halafu serikali inadanganya watu kuwa uchumi unapaa!

Serikali ambayo Rais wake anatawala kwa maelekezo ya MAFISADI. Kila mtu ameshuhudia wakti wa kampeni JK alikuwa akiwanadi MAFISADI WALIO NA KESI MAHAKAMANI kuwa ni watu safi wawachague ili warejee mjengoni kuendelea kuwanyonya Watanzania.

Serikali ambayo imejaa mikataba yenye utata inayonufaisha vigogo wa serikali peke yao.Seriakli ambayo hata Rais wake hajui kwanini wananchi wake ni masikini ilhali imejaa utajiri wa asili kama madini ya TANZANITE,ALMASI,DHAHABU,URANIUM,GAS n.k.

Seriakli ambayo haithamini hata wafanyakazi wake wanapodai nyongeza ya mshahara kufikia Tshs.315,000/=lakini inasema haina fedha ya kuwalipa hata kama wakidai kwa miaka 10 ijayo huku nviongozi wake wakitembelea magari ya bei mbaya(mashangingi) yanayouzwa katia ya TSHS.MILIONI 60 -80 lakini inasema haina fedha na KWAMBA HAITAKI HATA KURA ZA WAFANYAKAZI HAO!!!!

Sielewi kwanini Watanzania wamekubali kuirudisha hii serikali madarakani!!!

Nitaendelea..........
o
 
Ninasita sana kuwabeza watanzania kwa sababu wamepiga kura ila kilichotokea kwenye counts ni aibu kusema.
Rais huyu hakuwekwa kwa kura zetu bali wafaidika na uzembe wa utendaji wake ndio walioshinikiza kwa kila mbinu aendelee kutawala.
Mimi nasubiri hiyo mv. dodoma na tren ya umeme to mwanza.
Tunaingia kwenye maumivu ZAIDI kwa sababu ya uzembe wa dola yetu kuamua kuisadia jamii ya wezi kuingia madarakani.
 
thamani ya mtz itapotea, ushoga utaongezeka nchini na kiduku kitachezwa sana
 
Kilio na kusaga meno. Nunueni magunia ya kubebea noti maana inflation huenda ikagonga 20%
 
Back
Top Bottom