Watanzania Je! Si Bora Tukaongozwa na Hekima Kuandika Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania Je! Si Bora Tukaongozwa na Hekima Kuandika Katiba Mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mtu wa Mungu, Dec 30, 2010.

 1. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa mawazo yangu naona CUF wana agenda yao na suala la Katiba Mpya!!!????; sababu zangu ni hizi hapa:-
  1) Katiba, sheria mama, kimsingi ni suala la bunge-chombo cha kutunga sheria! Mimi nadhani ingekuwa busara kama hatua za msingi za kutupatia katiba kwanza zikawepo-pawepo na sheria ya bunge kuweka mchakato wa kuandika katiba mpya; Hadidu za rejea, chombo gani kipewe jukumu kushughulikia kipi, muda wa kukamilisha kazi na kutoa ripoti, ushirikishwaji wa jamii, na masuala mengine ya kisheria, kiuchumi, kijamii, kisiasa nk.
  2) Mchakato wa kupata katiba mpya siyo jambo la kukimbilia haraka haraka, maana kuna masuala mengi ya kuhusisha bunge, na kupata ridhaa ya wananchi kabla ya hata kura maoni; kilele ni kura ya maoni!!!!!!!
  3) Hawa ndugu zetu CUF ambao wanakimbilia mfumo wa serikali ya mseto wana nini cha kutufundisha juu ya ubora wake wakati Zanzimbar hata mwaka bado?; kwa imani yangu serikali za mseto ni za mpito-hivi wana maana tuingie mseto wakati wa kuandaa katiba mpya au vipi? Wana maana tuanze kuingia kwenye mgogoro mwingine wa kumuondoa Kikwete ili tuunde serikali ya mseto au vipi? Ni wapi duniani serikali za mseto zimejenga demokrasia ya kweli? Kama nikipewa kuchagua, serikali za mseto (mgabe style) ni kuua demokrasia, mimi siziungi mkono katu!!!!!!!-hazina tofauti na chama kimoja; kule Zanzibar CCM na CUF kiutendaji ni chama kimoja-sera muafaka moja, action plan moja,kiongozi mkuu mmoja, wana matatizo ya kisiasa tofauti na Bara;
  4) Haraka haraka haina baraka-hii CUF style!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Tuipuuze-ina jazba, nyingi siyo hekima!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  5) Kwa maoni ya jamii ambayo tumeona kwenye vyombo vya habari, suala la kuandika katiba mpya sasa halina mjadala; kilichobaki ni uundwaji wa mchakato, ambao hauna budi kuratibiwa na bunge-maana hiyo ndiyo moja ya kazi zake za msingi!!!!!!!!!!!!!!!! Sisi Watanzania tutulie, turuhusu hekima ituongoze; siyo huyu!, yule!, wale!..........; itakuwa tumepungukiwa na hekima!; Katiba siyo suala la chama fulani, kikundi fulani, au jamii fulani- ni kujenga taifa muafaka!!!!!!!!!!!!!
  6) Katiba ndiyo msingi wa jamii ya miaka mingi ijayo-tuone mbali tunapoandaa hadidu za rejea-tukubali kujifunza kwa majirani, na hata mataifa mengine yenye katiba aina tunayotaka kwa taifa letu;
  7) Turuhusu na kutumia bunge letu likiongozwa na moyo wa uzalendo-siyo ushabiki wa vyama au makundi!!!!!!!!!!!!!!!!!!Tangu nchi hii ipate uhuru ni mara ya kwanza kwa jambo hili kufanyika kwa namna ya dunia ya sasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...