Watanzania iwe mvua au jua tupambane kudai katiba mpya, amani inadumishwa na mifumo huru - mfano Kenya

Alishasema yeye "HAPANGIWI CHA KUFANYA" na kama sijakosea pia aliwahi kutamka kwamba katiba mpya "SIO KIPAUMBELE CHAKE" yeye anataka Tanzania ya viwanda tu.

Kwa muktadha huu nachelea kusema tutaendelea kupelekwa kibabe na tutaendelea kusomeshwa namba yumkini hadi awamu ijayo ya utawala.

Huwa najiuliza kimya~kimya ni kwa nini punde tu baada ya awamu hii kuchukua hatamu na madaraka ya nchi wakasema KATIBA MPYA SIO KIPAUMBELE?
 
Wenzetu kenya wametuonesha umuhimu wa vyombo huru vya maamuzi- amani yao haijalindwa na mabomu na wanajeshi kujaa barabarani imelindwa kwa mahakama kutoa maamuzi kwa haki bila kuingiliwa na serikali. hii ndio amani ya kudumu ..huwezi kuilinganisha na ile ya kutumia unyanyasaji wa raia na maonesho ya kijeshi

NB: harakati za kudai na kuitaka katiba yetu mpya zianze mapema kabla ya chaguzi zijazo ili kuweka misingi ya amani ya kudumu ktk taifa letu. lazima tulipende taifa letu na tuliandalie misingi ya kudumu huo ndio uzalendo

kenyata kaonesha uzalendo mkubwa kwa nchi yake hakutaka kuliingiza taifa ktk machafuko ..hakukuwa na kamata kamata ya wangalizi wa ndani wala hakuna komputa za watu zilizotekwa kama sisi mwaka juzi
[HASHTAG]#katiba[/HASHTAG] mpya Tanzania mpya
 
Uko sahihi 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hivi ajenda yetu sio katiba,acheni tumimine viwanda kwanza,Kikwete aliwapa nafasi mkaichezea kwa kufunga plasta midomoni na kususa vikao.Hatuwezi kuchezea pesa kila mara tunajadili katiba
Tunaleta sheria ya matumizi ya ruzuku na ukomo wa uongozi kwenye vyama kwanza halafu mwaka 2050 tutaendelea na tulipoishia kwenye kura ya maoni
 
Back
Top Bottom