Watanzania huu ni upole au ujinga? Kiongozi anachukuliwa meza kuu, mbele yenu mnapiga makofi!

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,995
2,245
Watu zaidi ya 100 wapo ndani kiongozi wao anachukuliwa kutoka meza kuu wao wanapiga makofi kama vile anapelekwa kupewa cheo kumbe rumande

Eti Mungu anawaona, iko siku yataisha tu, yana mwisho hayo, hawataingia Mbinguni. Hii ndiyo misemo ya watanzania siku hizi mara wanaponyanyaswa na mfumo Imla wa awamu ya 5. Tujiulize huu ni upole au ujinga? Hii ni busara au ujinga? Huu ni uvumilivu au ujinga? Je, babu zetu wangetumia misemo mkoloni angeondoka?

Hata mbuyu ulianza kama mchicha! Wamewazuia maandamano mmekubali, wamewazuia mikutano ya hadhara mkakubali, sasa watawazuia hata mikutano ya ndani pia mtakubali
 
Umewahi kupigana na askari akiwa on duty?

Umewahi kua eneo ambalo askari wamekuja kwa ajili ya kupiga na kukamata?

Umewahi kua eneo ambalo yanapigwa mabomu ya machozi?

Umewahi kuingilia ugomvi wa askari?

Kuongea ni rahisi kweli kweli
 
Wale wangewasha timbwili hilo gari lisingeondoka.....kina mama wangelala chini chali wote mbele ya gari lisingewaua....vijana wangesimama na Mh. wao Zitto hakuna ambacho kingefanyika...

Kufikia hapo Tanzania ni safari ndefu mno..... wacha tuendelee kutawaliwa watakavyo maana nchi hii ni yao na vyote vilivyomo... hii ndiyo nukuu ya katibu mkuu mstaafu Makamba kama mtakumbuka na ni ya kweli kabisa.
 
Sasa wangezui polisi kufanya kazi yao si ingekuwa kujiongezea makosa? Hata hiyo dhamana angepata sasa? Halafu kama ni fujo angeanzisha huyo anaekamatwa achapwe makofi kwanza ndio hao raia wangeona umuhimu wa kuingilia.
 
Wewe mbona hukufanya chochote!

Uvunje Sheria wewe, waijitokeze wengine waende jela ama kuumizwa Kwa ajiri yako, huo ndio upumbavu unaozitesa nchi nyingi za Africa

Au Umeona wapi hata huko nchi za watu wenye akiri, akikosea kiongozi mwanasiasa wanajitokeza wananchi wa kusema watalipia makosa yake, kama sio Kampeni za kijinga za Mabeberu ili tuuwane!!

Kila mtu afuate Sheria, likitokea la kuwakera wananchi wataandama wenyewe na sio kiongozi mjinga wa kisiasa amevunja Sheria Eti niandamane, Bora Tanzania sasa huo ujinga unapotea

Kila mtu Apambane na Hali yake
 
Wewe mbona hukufanya chochote!

Uvunje Sheria wewe, waijitokeze wengine waende jela ama kuumizwa Kwa ajiri yako, huo ndio upumbavu unaozitesa nchi nyingi za Africa

Au Umeona wapi hata huko nchi za watu wenye akiri, akikosea kiongozi mwanasiasa wanajitokeza wananchi wa kusema watalipia makosa yake, kama sio Kampeni za kijinga za Mabeberu ili tuuwane!!

Kila mtu afuate Sheria, la kuwakera wananchi wataandama na sio kiongozi mjinga wa kisiasa amevunja Sheria Eti niandamane, Bora Tanzania sasa huo ujinga unapotea

Kila mtu Apambane na Hali yake
Mkuu umeandika nini?
 
Watu zaidi ya 100 wapo ndani kiongozi wao anachukuliwa kutpka meza kuu wao wanapiga makofi kama vile anapelekwa kupewa cheo kumbe rumande!!

Eti Mungu anawaona, iko siku yataisha tu, yana mwisho hayo, hawataingia Mbinguni. Hii ndiyo misemo ya watanzania siku hizi mara wanaponyanyaswa na mfumo Imla wa awamu ya 5. Tujiulize huu ni upole au ujinga? Hii ni busara au ujinga? Huu ni uvumilivu au ujinga? Je, babu zetu wangetumia misemo mkoloni angeondoka??

Hata mbuyu ulianza kama mchicha! Wamewazuia maandamano mmekubali, wamewazuia mikutano ya hadhara mkakubali, sasa watawazuia hata mikutano ya ndani pia mtakubali!!
Wewe ulichukua hatua gani!?
Si mnasema kuwa mna nguvu ya umma?
Ukitaka kujua kuwa jeshi la polisi lipo kila mahali jaribu kufanya vurugu tu
Kwa hiyo unashauri nini?
Tii bila shuruti kama ukileta ubishi huwa wanatumia nguvu.
Nduli huyo anazidi kuvimba mwisho atapasuka nyie fuatilieni tu kwa karibu. Na vibaraka wake hapo wengi wanatoka pande za chattle.
 
Back
Top Bottom