Newbies
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 1,476
- 2,147
Hujambo na karibu ndugu msomaji,
Leo sitaandika sana ili nisikuchoshe
Nitaeleza kwa ufupi sana lakini natamani sana unielewe.
Jisikie kuwa ni mwenye bahati kwa kupata kufunuliwa ufahamu huu kuwa Tanzania Tumevamiwa kuna mzimu unatunyemelea na kutumezea mate! Napengine bado kidogo tuu uanze kututafuna, na mbaya zaidi kuna watanzania wanajipeleka na kujisogeza karibu kabisa na mzimu huo wenye njaa Kali bila wenyewe kujua na pengine wewe ni mmoja wao.
Utani ni semi zenye lengo la kufurahisha na kupitisha muda, ajabu nikwamba utani unapozidi huwa ni uchokozi, na hutengeneza chuki ambazo ama kwa hakika madhara yake ni makubwa kuliko pengine wahusika wanavyo dhani. Kwa ujumla utani sio mbaya sana lakini huwa sumu pale unapoanza kuingia katika masuala nyeti ya kinasaba au kikabila, pale ambapo maandishi, maneno ama picha, au video kubeba dhana ya kutania, kudunisha, au mchoro wowote hasi juu ya kabila fulani, hii ni sumu ambayo inaweza kujenga chuki, kuvunja ushirikiano baina ya Jamii na Jamii, au Jamii ya watu Fulani kujiona duni kutokana na namna wanavyo chukuliwa na Jamii Nyingine. Na Mara nyingi katika hiki kizazi cha maendeleo ya TEHAMA.
Kama wewe ni mtumiaji mzuri Wa mitandao utakuwa umewahi kushuhudia picha, ama maneno au maudhui yeyote yanayo dhalilisha kabila au Jamii ya watu fulani, pengine uliichukulia poa, ukacheka ukafurahi, lakini napenda ufahamu Leo kuwa hii ni miongoni mwa masuala yanayo zusha uhasama, kuhasimiana kati ya Jamii na Jamii na inaweza kufika wakati ulee muunganiko wetu, ule uhusiano wetu, Yale maheshimiano yetu, na ule ukarimu wetu kati ya Jamii na jamii ukapotea kabisa nakubaki kuwa historia katika ardhi hii ya matumaini.
Katika karne hii hakuna haja yakulizungumzia kabila fulani kuwa nibora au kabila fulani ni washamba au hawa ni bora Bali tuzungumzie Utanzania wetu ili tuulinde ule muunganiko tuliojaaliwa
Inasikitisha katika karne hii ya maendeleo ya tehama mtu anathubutu kutamka oooh ofisi fulani wamejaa kina fulani ooo kabila fulani ni washamba Mara ooo kabila hili wanajigamba namengine mengi yakukera.
Sisi sote kabila letu ni watanzania tushirikiane, tuepushe chuki miongoni mwetu ili amani na ushirikiano uwepo na uendelee kuwepo baina yetu. FUTA DELATE KABISA , ujumbe, picha, video au matini yeyote yenye maudhui hasi juu ya kabila fulani.
Mwisho.