Watanzania hivi hili suala la bei bando limekaaje?

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
5,050
5,078
Nnaomba kujuzwa hivi hili swala la Bei ya Bando nani kamshindwa mwenzie Kati ya Serikali na Makampuni ya Simu? Ndugu zangu hivi tuseme tumeshindwa kabisa kupigania haki zetu au ndio tumekubali yaishe?

Yaani juzi GB 9 zilikua 10k eti leo bei hiyohiyo ni GB 2.5 kwa Tigo. Hivi hakuna namna wanunuzi tunaweza susia hii mitandao ya simu? Tugome kabisa kununua hizi bando mpaka wakubali kurejesha? Huyu Waziri yupo ofisini anafanya nini kama hata mambo madogo kama haya yanamshindwa? Watanzania Tunaburuzwa sana yaani. Au kuna mipango ya kuturejesha enzi za ujima, enzi za giza kwamba sasa wenye uwezo mkubwa ndio wanunue tu hizi huduma?

Tumefika pabaya sana ndugu zangu, wakati Mataifa mengine yanapambana kurahisisha mambo ya mawasiliano sis ndio tunarejeshwa kizani kwa nguvu? Na tumekubali? Alafu kuna kondoo iliyoshiba kodi zetu huko Bungeni inahamasisha tuongezewe kodi kwenye vocha na next time atarejea tena bungeni?

Lini tutashughulika na wapuuzi kama hawa? Eti leo GB 1.5 inauzwa elfu 5 huku kuna wanaotegemea mtandao kufanya biashara zao, alafu kesho utasikia Mwanasiasa anakwambia maendeleo ya wananchi. Wananchi wapi hao wataendelea ikiwa nyenzo muhimu kama mawasiliano yanapandishwa bei kila siku? Nnaandika nikiwa na hasira sana lakini nnadhani yafaa kufanya jambo au laah tukubali kufa Kijerumani na tai shingoni.
 
A narrative has changed et bando linaisha haraka kwa sababu ya setting za simu zetu.

Huyu waziri wa bando mshenzi sana
 
Vda wamerekebisha wakuu , 1GB + 100 dk mitandao yote Kwa wiki , naenjoy hapa wazee , nahs hii ni Kwa DSM...sjajua wanalambaje MB ila Kasi Yao konki sana
 
Sifahamu kama huwa wanaokotwaga wapi hawa, siku kama tatu zilizopita menue ya tigo ilibadilika na 10k ilikua unapata 9GB eti leo 10k unapata only 2.5GB yaani 1.25GB ni 5k, aisee tumeisha kama wanasiasa tunawaachia waamue watakavyo
A narrative has changed et bando linaisha haraka kwa sababu ya setting za simu zetu.

Huyu waziri wa bando mshenzi sana
 
Back
Top Bottom