Elections 2010 Watanzania Heshimu Imani za watu katika kumtafuta Mungu.

Gsana

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
4,383
1,321
Watanzania,kumbuka kila mtu ana imani yake. Baada ya kufuatilia mgogoro wa wafuasi wa ccm Sumbawanga kusadikiwa kuwekewa vikwazo katika sakramenti mbalimbali,nimeshangazwa sana na kauli inayodaiwa kutolewa na mbunge Hilarly wa ccm, kuwa ccm wanatumia utatu mtakatifu,yani mafiga matatu,hii ni kashfa kubwa kiimani. Tangu nizaliwe sijawahi kusikia mkiristo yeyote anajiita mtume mhammad,kama yupo naomba kusahihishwa,ila kwa ccm kutamka wazi kuwa wana utume wa nguzo tatu ni fedheha kubwa kwa wenye imani yao. Huu si udini kama watawala wetu wanavodai bali ni kashfa za kudhalilisha imani za watu. Nakumbuka siku Jakaya Kikwete aliporudisha fomu pale Lumumba,Lt.Makamba alisoma vipengele vya biblia kuwa"Kikwete ana sifa za Askofu,na ni mume wa mke mmoja,pia aliyejitoa kuongoza wengine" alieleza mengi wala hakunukuu vitabu vya imani ya mgombea,kana kwamba mgombea hana dini au ni mpagani. Au wapiga kura ni wale tu,wa vitabu vilivonukuliwa?au naye aikubali imani yake? Binafsi nilishangaa kuhusisha mtu wa imani tofauti na Baba Askofu,cheo kikubwa hadhi ya tatu baada ya Baba mtakatifu na Kardinali au pia Monsinyor. Ni fedheha ya kuilaani. Sasa kuna kule sumbawanga ambapo magazeti ya serikali yanaripoti kuwa wakatoliki kutengwa kwa kuichagua ccm! Hivi kuna ugumu gani wa kueleza ukweli kuwa kuna Kashfa ilitolewa dhidi ya ukatoliki? Kumbuka ccm si ya watu wenye imani moja ya kiroho. Kumbuka ushabiki haufai katika imani. Dunia ilikuwapo kabla ya dini zoote. Baada ya Yesu Kristo kuzaliwa historia ya dunia ikakaa ktk vpande 2,kabla ya Kristo BC,na baada ya Kristo, wakati katikati tukawa na mwaka aliozaliwa kristo mwaka sifuri ambao unaitwa A.D yani "Annuo Domini" meaning "in the year of the Lord" ambayo ni karne ya kwanza na leo ni karne ya 21. Pia ni milenia ya kwanza apo mwaka sifuri,mwaka 1000,ndo milenia ya pili,mwaka 2000 ndo milenia ya 3,na leo ni mwaka 2010. Tangu mwaka sifuri mpaka Baada ya miaka takribani 600 ndo tukapata mtume mwingine ambaye alipinga wa kwanza na kwenda kuiji kule Makka akitokea Medina miaka ya 622 Baada ya Kristo kuja. Kila mmoja wao ana wafuasi wake ambao ni sisi aidha waislamu au wakristo. Je,Kama tunaelewa kuwa kila mtu anafuata imani yake,je kuna haja ya kuitilafiana? Nadhani umefika wakati tusikubali kugawanywa na wanasiasa wanaoabudu udini! Sumbawanga,jueni kuna watu wamepewa mamlaka ya kuwaongoza kiroho na ni sharti kuwaheshimu,wawe viongozi wa msikiti au viongozi wa makanisa. Mkiburuzwa na siasa mtaishia kwenye laana na vizazi vyenu kwa kukashfiana! Naunga mkono wale wote wanaopingana na viongozi wao wa kiroho wasipate huduma za viongozi wao. Nakumbuka wakati flani nilipata kuhishi Muleba pale Buganguzi,kuna kundi flani lilitaka kuyumbisha msikiti kwa kutomkubali kiongozi mteule,nakumbuka mtu maarufu Shaaban akiwa na pick up yake aliamua kujenga kibanda kule Kalanda/Buhanga ili kundi lake lijistili kwa muda baada ya kutengwa na msikiti. Mimi nilichukizwa na msimamo wao kwani kiongozi wao wa Imani alichaguliwa kwa vigezo ila eti chuki binafsi hawamtaki! Kubalini kuwa na viongozi wa Imani,hawawezi kufuata mnalotaka nyie,acheni kuleta mtafaruku katika Imani. Nasema tena,wakorofi na wasaliti wanyimwe huduma za viongozi mpaka watubu. Mtu alazimishwi kuwa mfuasi wa dini yoyote,kama hutaki kuwa mkiristo kufuata matakwa ya mapadre na wachungaji,usiseme umejitenga bali tafuta imani unayojua wewe utakuwa mkuu wao,kadhalika kwa dini nyingine zote tafuta panapokufaa na si kuanza kulalama eti unatengwa! Kama ufuati unachoelekezwa,tafuta unakofaa na si kuwachafua wenye imani. Pia wewe kama hauna imani na ukristo acha kujifananisha na viongozi wa imani iyo au mungu wao! Unatafuta laana. Nilikuwa natatizwa na midahalo ya jioni kwenye makoni ya kelele,sana sana magomeni pale dar es salaam, ambayo mwanzo mpaka mwisho si kuhubiri Imani yao bali ni kukashifu na kutukana imani za watu.Nakumbuka Ze komedi walitoa utani kwa mavazi ya mwambao,watu wakaandamana wakielekea Mnazi Mmoja kuwaombea mabaya yawapate,je kuwa na utatu mtakatifu yani Mungu wa Wakristo, katika kujitambulisha kama uyu mbunge wa Sumbawanga si laana. Tusifike mbali,Hilarly,fanya kama ulivosema,mtafute mhashamu Askofu Kyaruzi ukatubu! Usiwaletee wakristo mgawanyo. Namalizia kusema kuwa Watanzania tambueni kuwa kila mtu ana imani yake,heshimu mwenzio,heshimu imani za watu. Huu si udini,ni madai ya kawaida ya kukumbushana ili tuendelee kuhishi vizuri na hatimaye kuwaachia vizazo vijavyo waishi kwa Amani.
 
Umesema neno, hv huyo Hiraly kwanini asitumie maneno ya dini yake hii ni kukebehi dini ya wakristu.
 
Imeandikwa Luka 6:27-36 "Lakini nawaambia ninyi mnaosikia wapendeni adui zenu watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi wabarikieni wale ambao wawalani ninyi waombeeni wale ambao waonea ninyi akupigae shavu moja mgeuzie lapili naye akunyang'anyaye joho lako usimzuilie na kanzu mpe kila akuombaye na akunyag'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie nakama mnavyo taka watu wawatendee ninyi watendeeni vivyo hivyo

Maana mkiwapenda wele wawapendao ninyi mwaonyesha fadhili gani? kwa kuwa hata wenye dhambi wawapenda wale wawapendao nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema mwaonyesha fadhili gani? hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. Na mkiwakopesha watu vitu huku mkitumaini kupata kitu kwao mwaonyesha fadhili gani? hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi ili warudishiwe vile vile basi wapendeni adui zenu tendeni mema na kukopesha msitumaini kupata malipo na dhawabu yenu itakuwa nyingi nanyi mtakuwa wana wa aliye juu kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasio mshukuru na weovu basi iweni na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma."

Tuwatendee maadui zetu kwa roho njema. Imeadikwa Mathayo 5:25 "Patana na mshitaki wako upesi wakati uwapo pamoja naye njiani yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi na kadhi akakupeleka kwa askari ukatupwa gerzani."

Usifurahi katika majonzi ya adui zako. Imeandikwa Medhali 24:17-18 "Usifurahi adui yako aangukapo; wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; Bwana asije akaliona hilo likamkasirisha akgeuzia mbali naye hasira yake."

Imeandikwa Warumi 12:20 "Lakini adui yako akiwa na njaa mlishe akiwa na kiu mnyeweshe maana ufanyapo hivyo utampalia makaa ya moto kichwani pake."

Mungu ametuahidi kutuhifadhi kutokana na maanui wetu imeandikwa Zaburi 18:48 "Hutniponya na adui zangu naam waniinua juu yao walioniinukia na kuniponya na mtu wa jeuri."
 
Wachangiaji,nashukuru. Babuyao,sawa ila nimeshinwda kuweka aya sababu nilipo kwa sasa hamna kyomputa,natumia simu ndo maana hamna aya. Next time ok. Tuungane kuwaelimisha wasiolewa umuhimu wa imani za wengine. Nawashukuru.
 
Back
Top Bottom