Watanzania hawaruhusiwi kutembelea hifadhi ya taifa serengeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania hawaruhusiwi kutembelea hifadhi ya taifa serengeti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by issenye, Nov 16, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 991
  Trophy Points: 280
  Wadau mimi ni mtanzania ambaye ni mzaliwa kanda ya ziwa, niko kikazi arusha. Leo nilikuwa nasafiri kwenda nyumbani mwanza. Ajabu ni kuwa baada ya kufika katika hifadhi ya taifa ya serengeti niliambiwa kuwa siruhisiwi/watanzania hawaruhusiwi kutumia njia ya naabi - ndabaka kwa kuwa njia hiyo ni kwa ajili ya wazungu tu. Najiuliza je, watanzania hatuna haki kwenye nchi yetu na je kwa nini serikali inapoteza fedha nyingi kwa ajili ya kutangaza utalii wa ndani
   
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  mkuu lete ushahidi hapa ili tushikie bango suala hili. Una picha? audio , muda, siku, namba ya askari aliyekukataza, ulionana na mkuu wa hifadhi hapo.? je walisema maneno hayo kwamba mtu mweusi/ mwenyeji haruhusiwi? Ikiwezekana nenda tena fanya u-FBI ulete facts hapa ili jambo hili lisiwatokee wengine. Huku ndiyo kujitoa kwa maslahi ya taifa.
   
 3. 1

  19don JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  pole mtanganyika mwenzangu walihisi utapiga picha zile hotel walizo jenga mbugani
   
 4. JS

  JS JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Issenye kafanye uchunguzi zaidi tuwaaibishe hawa nchi yangu ardhi yangu mbuga yangu ninyimwe kupita?kisa wazungu?wallah ningelianzisha na habari zingewafikia.haiwezekani fanya uchunguzi utuletee hapa tuwaaibishe. Hivi mbona issue kama hizi hazinipatagi mimi???
   
 5. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  ...Nakubaliana na Kwame kuwa lete ushahidi na data zaidi hapa ili suala hili lifuatiliwe. Pia eleza ilikuwa saa ngapi, siku n.k na ili tukupe jina la Chief Park warden wa pale ili ufuatilie. Kama vp kuna mpiganaji pale mjengoni, ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya maliasili na mazingira pia yy anaweza kusaidia km ikibidi.

  Isijekuwa unajiita Issenye (majangili sana eneo/kijiji hicho) then unakatiza saa sita usiku ukijifanya unakwenda home mwanza kumbe unavizia pofu... lol !!

   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  wakuu mimi naungana na jamaa hapo, kuna ukweli ndani yake, kuna ubaguzi mkubwa sana umekuwa ukifanywa kwa watanzania na si kwa watu weusi kwa sababu wakenya hawanyaywasi kwenye hifadhi zetu za serengeti na ngorongoro. Nitatoa mfano hai.

  1. Watanzania wanao safili na mabasi kutokea arusha kwenda musoma kwa kupitia hifadhi za ngorongoro na serengeti ndo wahanga namba moja,

  - kuna makampuni matatu yanayo safirisha abilia kupitia hizo hifadhi nitayataja.

  1. costline east africa
  2. Kimotico group
  3. Manko express

  1. Ubaguzi namba moja -abilia wote wanao safili na hayo mabasi wanapofika kwenye mageti ya ngorongoro na nabi hushuka chini wote kuhesabiwa kama kuku, but mabasi ambayo unaweza kuta yamekodiwa lakini yamebeba wazungu au wafrica kutoka kenya uganda na kwingineko hawashushwi kuhesabiwa.

  - huu ni ubaguzi namba moja wanao fanyiwa watanzania wanao pitia hizo mbunga.

  2. ubaguzi namba mbili- uko katika vyoo, hili ni kwa hifadhi ya ngorongoro pekee, watanzania wanao safili na hayo mabasi wana vyoo vyao na watu weupe wana vyakwao,

  - wakuu huu nao ni ubaguzi mkubwa sana wanao fanyiwa watanzania, kuna day nilishuhudia costa moja basi iliwa imewabeba wakenya wakienda hifadhi ya serengeti hakuna aliye shuka kuhesabiwa na wakati huo basi lililo beba wabongo waliamuliwa washuke wahesabiwe
   
 7. N

  N series Senior Member

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  manainer zao na jk wao
   
 8. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Duh!! Hii imekaa vibaya sana!
   
 9. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  usijali nikutokana na \tishio la al shabab sasa ulinzi umeimarishwa mbugani pole kwa yaliyo kusibu hata sisi tulitaka kuandamana kupinga malipo ya dowans tukaambia alshabab
   
 10. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  mkuu hebu jibu maswali ya Kwame hapo ili hili swala lishughulikiwe ipasavyo
   
 11. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana mlima kilimnjaro umeshindwa kupita.ungeshinda wange zuiya wa tz wasikaribie jarani na mlima.nchi imelaaniwa pomoja na wanayo iongoza
   
 12. b

  buswe Member

  #12
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa suala la vyoo nalegeza msimamo. Baadhi ya watz siyo wastaarabu kwenye matumizi ya vyoo. cheki wanja wa taifa walivyofanya. walifikia hatua ya kupakaza ukutani. je mtu kama huyo akisafiri hatafanya hivyo? ila kama ni hivyo wahusika wangetoa elimu ya kutosha kwa wasafiri badala ya kuwatenga.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,478
  Trophy Points: 280
  hao viongozi wa hiyo mbuga inatakiwa siku waje ulaya wakae kama mwaka wabaliweeeeee na wazungu wakirudi huku watatia akili wenyewe.
   
 14. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,145
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  MIMI ni mdau wa utalii, na ukweli ni kwamba TANAPA wanazuia yale magari ambayo YANATOKA UPANDE MMOJA WA HIFADHI KWENDA UPANDE MWINGINE WA HIFADHI.(TRANSIT ROUTES)ili kuingia na au kutoka naabi gate,kutumia barabara ya Ikoma gate.badala ya Ndabaka gate na sio watanzania wanaoingia hifadhini kutalii.na barabara hii ndio route rasmi ya barabara kuu ya serkali,FORT IKOMA-NAABI GATE-NGORONGORO-KARATU.na ikumbukwe tanapa hutumia pato lake la ndani kugharimia matengenezo ya barabara hizo.hivyo ni haki yao kupanga
   
 15. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Waende Nchi za nje wakirudi
  si ndo watabeba mbuga nzima chumbani mtu asione kitu...
   
 16. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  pole sana wahanga watz hamruhusiwi kutalii mbuga zenu halafu bungeni utasikia utalii wa ndani sio mzuri tatizo hatulijui mungu inusuru tanzania mambo mabaya sana..
   
 17. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  duh, hii ni hatari sasa...
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu una msimamo wa kiivyo kweli!
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sintoweza kushangaa jambo kama hili kwa jinsi ninavyoifahamu serikali yetu pengine na sisi wenyewe tumelisababisha kwakushindwa kutoka mwaka jana kuchagua serikali iliyo imara na yenyekutaka maslahi kwa taifa, pia naona tunatawaliwa na wakoloni japo indirect kwakuwatumia waTZ wenzetu, TZ amka, vijana amka tulikomboe Taifa letu kwa ata aliyetupigania uhuru alikuwa kijana shupavu je vijana tunasubiri nini?
   
 20. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  lakini mkuu....mdau hapo alikuwa anaenda Mwanza........inakuwaje atumie gate la Ikoma wakati njia sahihi ni Ndabaka....?

   
Loading...