Deeboyfrexh
JF-Expert Member
- Apr 3, 2015
- 3,240
- 5,248
Huyo mwamba anataka kuendesha shirika kwa siasa kama awamu ile ambayo watu walifikia kugawana hela za michongo yani ESCROW! Umeme ulikuwa kero balaa kumbe ni juhudi za makusudi za watawala kutuangamiza.Mkuu, umeelezea kwa uchungu na hisia kali kuhusu waziri mwenye dhamana kuwa ndiye pekee ambaye anapaswa kubebe zigo la lawama kuhusiana na matatizo ya kihistoria yanayoikabili TANESCO. Lakini nafikiri ni vyema pia hata ungetoa ushauri nini hasa kinapaswa akifanye.
Je! Ni vyema kulazimisha umeme upatikane kwa njia yoyote ile pasipo kujali ushauri na mazingatio ya kitaalamu? Ama la, ni vyema pia kuzingatia ushauri na mazingatio ya kitaalamu kwa kukata umeme kwa muda ili kutafuta suluhisho la kudumu?
Stitch in time saves nine! Waziri inampasa alipitishe Taifa katika njia sahihi bila ya kujali nani anasema nini na yupo wapi. Ni ukweli uliokuwa bayana kuwa hawezi kumridhisha kila mtu.
Watanzania wa mwaka 2021 sio wale wa 2007 ambao unaweza kuwapiga sound za kishamba eti kuwa kiangazi ndio kimefanya umeme usiwe wa uhakika au service ya mitambo. Kinachofanya statement za utetezi huo ziwe ngumu ni vile JPM alipohakikisha umeme hauzimwi kipumbavu na kila ulipozimwa kulikuwa na sababu ya msingi! Kwa hizi kelele za sasa laiti kama hayati angekuwepo Waziri wa nishati angeshakuwa kapigwa chini!