Watanzania hawana imani na Waziri wa Nishati January Makamba, anapaswa kuachia ngazi, asipoachia Rais amuondoe

Nchi zingine mbona wanaservice na umeme haukatwi kila siku.Shida watu wanahoji ni hivi inamaana kama wao kuingia tu kila kitu kikawa kibaya hadi crane ya kunenyua tani 29 inabidi inagizwe nje wakati crane nchini zipo harfu unasema tumpe mda.Mtu wa kumpa mda ni yule unakuta ameingia mambo yakiwa mabaya hivo anatakiwa kurehekebisha.Lakini yeye amekutana mambo kwa wananchi yalikuwa mazuri ila sasa wao wameharibu harafu wanasingizia visivyowezekana..eti mashine hazikuwahi kukarabatiwa na nyie watanzaniq mnakubali na kutetea.Je unajua maana ya corrumption syndicates?je unajua Tanzania ni watu gani wanaendesha nchi kwa kuibia nchi?Je unajua unajua ni watu gani walimuua magufuri na wako na sasa ndo wanaendesha nchi ikiwemo kuendesha kukta umeme ili wafanikiwe mambo yao?Tafakari
Una maana Magufuli wetu aliuawa na waliomuua ndio wanaoendesha nchi kwa sasa??!! duh...
 
Anachokifanya January kujenga mazingira mazuri na ya kitaalamu ili aweze kuiendesha wizara yake. Mkuu, kuhusu matumizi ya maneno ya Kiingereza ndivyo ambavyo mtu yeyote anayetumia lugha yoyote anaweza kufanya ili kutokuweza kupoteza maana aliyoikusudia.

Nenda hata katika hicho Kiingereza ambacho unakisema, kimeazima maneno mengi kutoka katika lugha nyingine hasa Kilatini ili kutopoteza maana lengwa. Maneno kama; ceteris paribus, mutatis mutandis, fait accompli, functus officio, ad hoc, n.k.

Hata Nyerere akiwa kama msomi, katika hotuba zake nyingi ndivyo ambavyo alikuwa akifanya. Pole mkuu, kama nimekuharbia siku kwa kuchanganya maneno, sina njia yoyote ile ya kukusaidia.
Mazingira yapi mazuri na ya kitaalam wakati hana utaalam wowote wa maswala ya umeme?kama ni maswala ya uongozi haihitaji muda mrefu wa kujifunza
 
Mkuu, hivi tuseme ni muda gani hasa mtu akiaminiwa kufanya fulani ndipo watu wanaweza kumfanyia tathmini ya jumla? Hata kwa nafasi ya urais watu huanza kuangalia siku zake 100 za kwanza akiwa ofisini.

Mimi kwa upande wangu naona watu wengi wenye kumkosoa January, wanatamani afanane kiutendaji na waziri aliyemtangulia. Hiki ni kitu ambacho hakiwezekani. January ana "approach" ambayo ni tofauti kabisa na ile ya Kalemani.

Watanzania wengi wanapenda kuyasikia yale ambayo hupenda kuyasikia hata kama ni ya uongo. Lakini hawaupendi ukweli mchungu. Mtambo na mashine yoyote ile inayotumiwa kwa muda fulani inabidi ifanyiwe "service & maintenance" mara kwa mara ili iweze kuwa na ufanisi.

Huwezi kuacha kuzingatia ushauri wa kitaalamu na kupuuziac kufanya hivyo eti kwa kuwa watu wana shida ya umeme na wala kiongozi hataki kusikia suala la umeme kukatika. Kama umeme unakatwa kwa kuwa miundombinu ni chakavu na mashine hazifanyiwa "service" kwa muda mrefu, hakuna ujanja hapo, ni kuukata tu.

Ijapokuwa, taarifa zitoke kwa wakati kuhusu nini hasa kinachoendelea. Mimi binafsi nachelea kukimbilia kumtupia lundo la lawama waziri katika muda mchache aliokaa katika nafasi hii.
Kinachoangaliwa ni impact ya approach ya kinachofanyika. Kuna mmoja hapo ana negative impacts nyingi Kuna mwingine ana positive impacts nyingi
 
Sikiliza Kalemani! Kama Kuna madili hukumalizia kuwa mpole tu! Hukuzaliwa kuwa Waziri!

Kama shida ya Umeme ilikuwepo ukiwa Waziri na haijawai kuondoka!

Makamba ndo waziri we endelea kunung’unika tu huko Chato
Exactly,ndio yeye huyo amewalipa wahuni mitandaoni wanamsakama January, mpuuzi Sana kaleeemani
 
Makamba mwenyewe ni gwiji wa personal attacks....ukweli wenyewe ni kuwa Makamba hafai hata kuwa Katibu kata...mtu anayemteta hata rais wake hafai hata kidogo...ni aibu kwa taifa kwa mtu wa aina hii kuteuliwa kwa nafasi yoyote ile ya umma...ni aibu kubwa...


Amemteta wapi ?

Kuhusu jambo gani ?

Mnataka kuanza kumfitinisha na Rais ?



Yatawashinda

Mpewa hapokonyeki

Kama ni hivyo basi Januari he is a greater person.

Itakuwa Mwenyezi Mungu ameweka kitu kikubwa sana ndani yake ambacho wanajimu wanakiona na kukasirika kwa husuda!

Aisee angalieni nawashauri msijemkaugua!

Chuki, husuda, fitina huwa humuumiza mwenye kuzibeba moyoni.
 
Wewe ni mmoja wa lile kundi lililomwagwa humu kumchafua tu na si vinginevyo. Ukiulizwa kafanya lipi baya utaumauma midomo tu.
Twambie kama unajua, Makamaba alisema baada ya siku mbili au tatu atakuja na suluhu ya kudumu ya umeme
Je unajua nini kiliendelea utujuze?

Kama mtu anajichafua mwenyewe sasa sisi tunamchafuaje?

Toa jibu la suruhu ya umeme la siku mbili kama unamtetea,
Je alisemaje?
 
Amemteta wapi ?

Kuhusu jambo gani ?

Mnataka kuanza kumfitinisha na Rais ?



Yatawashinda

Mpewa hapokonyeki

Kama ni hivyo basi Januari he is a greater person.

Itakuwa Mwenyezi Mungu ameweka kitu kikubwa sana ndani yake ambacho wanajimu wanakiona na kukasirika kwa husuda!

Aisee angalieni nawashauri msijemkaugua!

Chuki, husuda, fitina huwa humuumiza mwenye kuzibeba moyoni.
Hivi ukimchukia shetani mwisho wake ni upi???
 
Kila kona manug'uniko ya watanzania ni juu ya dalili za wizara nyeti ya nishati na umeme kuwa na waziri ambae watu hawana imani nae. Tangu ateuliwe kuwa waziri basi taifa limekuwa na mauzauza tu juu ya upatikanaji wa umeme na hata uongozi na uendeshaji wa Tanesco.

Kitendo cha watanzania kutokuwa na imani na waziri huyu ni sababu tosha kabisa ya kujiuzulu au kuwajibishwa maana ni muda mfupi tu ameprove failure

Mtangukilizi wake Dkt Kalemani alisimamia vizuri Tanesco na kudhibiti ukatikaji hovyo wa umeme, pia aliwahakikishia watanzania kuwa mradi wa kuzalisha umeme wa JNHP utakuwa tayari ifikapo juni 2022.

Lakini tangu ateuliwe January Makamba kuwa waziri mradi wa JNHP umeanza kupata mauzauza, ujazaji maji kwenye mabwawa umechelewa kwa sababu zisizo za msingi, huku kukiwa na harufu ya ufisadi.

Nishati ya umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu. Hii wizara haipaswi kuwa na waziri anayetiliwa shaka na umma kuwa mpiga madili.
Mkuu


Nakuunga mkono asilimia 100 ila tatizo ni mtoto wa mama ni sharti abebwe kwa mbereko. Huyo kijana hafai kwa uongozi wa aina yoyote labda ujanja-ujanja wa mitandao lakini sio kuongoza watu wenye akili kubwa.

January hafai
 
Hivi ukimchukia shetani mwisho wake ni upi???


Changamoto ni pale unapotakiwa kuthibitisha kama ni shetani kweli au ni kwa kuzaniazania na mtazamo tu!

Hata sometimes mitihani tunatopitiaga Wanadamu na failures mbalimbali mara nyingi tunazani ni shetani lakini huwa tunakosea , siyo kwa kiasi hicho.

Mitihani mingine hutoka kwa Mwenyezi Mungu, mingine husababishwa na uzembe wetu wenyewe Wanadamu na matendo maovu.
 
Sema wewe na sio watanzania, Hakuna mtu amekutuma utujumuishe kwenye mawazo na mitizamo yako
 
Amehujumu kivipi ?


Kwamba hutakikukubaliana na ukweli kuwa kumekuwa na tatizo la ukame kiasi cha kusababisha hata huduma ya maji ya kawaida kukosekana?

Na unajua kuwa umeme ya nchi hii huzalishwa kwa njia ya Maji ?
Hamna ukweli umeme na maji yanakosekana kwasababu ya ukame. Visingizio pelekeni kwa wake zenu tunataka umeme. Na wajinga wengine hao Dawasco na mgao wa maji. Mimi sio fan wakuendekeza uzembe.
 
Back
Top Bottom