Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,087
- 6,568
Mbona kila kukicha hapa bongo yanaibuka mapya? Maana katika kupita huku na kule nimekutana na Mbunge mmoja akiomba kama kuna uwezekano basi katiba ya JMT ibadilishwe ili kuwe na kipengele cha kuhakikisha miradi mkakati inayotekelezwa awamu hii ya tano italindwa mpaka ikamilike hata kama rais Magufuli hatakuwepo madarakani.
Mbunge huyu anayo hofu kuwa miradi mkakati mingi haitakamilika awamu hii ya tano. Na baada ya rais Magufuli kutoka madarakani akija rais mwingine huenda akasaini executive order ya kutoikamilisha nae akaanza na miradi mingine. Nafikiri ni mbunge wa Mboka Manyema, Emanuel Mwakasaka.
Hoja yake inaweza kuwa ina mashiko. Maana zaidi ya JNHPP kukamilika kwa wakati, SGR ni kama ndoto.
Lakini je, sisi tunataka katiba mpya ajiri ya miradi mkakati? Hapana tunataka katiba mpya kwa ajili ya mustakabali mwema wa taifa letu kwa kila namna. Mfano ni kuwa na katiba ambayo itahakikisha kila Mtanzania anakuwa na haki sawa bila dhuluma.