Watanzania hatupaswi kumlaumu Magufuli, tujilaumu wenyewe kwa kuishi kwa mazoea

Mchimwachimego

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
358
271
Watanzania wa kipindi cha kwanza cha Mkapa watakubaliana nami kuwa mazoea yanaharibu sana fikra za jamii. Kipindi cha kwanza cha Mkapa nchi ilikuwa imetoka katika uongozi wa ruksa maana yake nchi ilikuwa haina mifumo imara hivyo alipoingia Mkapa alisababisha watu wengi kuanza kuona kwamba Mkapa amewaharibia biashara na ndipo kodi nyingi zilianzishwa za sehemu mbalimbali . Watu walikimbia kwa sababu watu waliokuwa hawana shughuli zaidi ya uzururaji na ujanja ujanja walimchukia sana jamaa lakini matokea yake yalionekana baadaye, nchi ilianza kujiendesha.

Sasa vijana wa leo nao wanarudi kulekule ambako tulitoka na ndio maana naanza kukubaliana na msemo samaki mkunje angali mbichi. Na tatizo hili linaanzia kwenye mifumo ya sheria kuoneka mizuri anapopatikana rais mpole na kuonekana mbaya na kandamizi akipatikana anayezisimamia sawia.

Wote mashahidi kwamba sheria za kodi hazijabadika hata kidogo, bali kuna udhibiti na ukomeshwaji wa rushwa kwenye biashara. Kwa sasa maghendo, rushwa, kukwepa kodi ni mwiba mchungu kwa wafanyabiashara kwa sababu ndiyo ilikuwa nyenzo kuu za biashara. Sheria ya manunuzi ya umma ilikuwa ni kichaka cha upigaji kwa wahasibu, wakandarasi na mainjinia. Haya yote yalifanya maisha yawe rahisi kwa walio wachache na kutokuwa na mwanga kwa walio wengi. Nchi ilikuwa kama mshumaa unaomulika huku ukiteketea na kuisha.

Kama kweli Watanzania tunataka mabadiliko tuachane na tabia ya kuchagua kwa kutaka urahisi wa mambo tusijizoweshe kulishwa tujaribu kujitafutia rais Magufuli hajabadili chochote kuhusu sheria za kodi yeye alichofanya ni kuwaonyesha namna sheria zinapaswa kusimamiwa kama ambavyo Ulaya wanazisimamia, isipokuwa kwamba Watanzania wameshakuwa samaki mkavu, walishazoeshwa kupata mali kwa njia zisizo halali na hwazitolei jasho hivyo anapopatikana mtu anayetaka utaratibu ufuatwe anaonekana ni kikwazo jamani tujifunze kutafuta kwa kufuata sheria.
 
Mimi nataka afuate haki. AAche kuua watu. Ugomvi wangu mimi na yeye aache kuteka watu. AAche kuwamiminia risasi watu wanaombishia. Huwezi kunimimia risasi 38 halafu 17 zinipate, halafu nipone nikuseme vizuri, mimi siyo mjinga. Magufuli The Killer hata ajengeje nchi, inakuwa maaendeleo ya damu, SITAKI! Full Stop
 
Mimi nataka afuate haki. AAche kuua watu. Ugomvi wangu mimi na yeye aache kuteka watu. AAche kuwamiminia risasi watu wanaombishia. Huwezi kunimimia risasi 38 halafu 17 zinipate, halafu nipone nikuseme vizuri, mimi siyo mjinga. Magufuli The Killer hata ajengeje nchi, inakuwa maaendeleo ya damu, SITAKI! Full Stop
Una hakika na unayoyasema mkuu?
 
Sisi hatuna shida na Magu.. shida ya hii nchi ni CCM.. ccm wameshindwa kutengeneza system stable inayodumu. Ndio maana akitoka rais huyu mwingine anavuruga aliyoyaacha mwenzake.

Dawa ni kumchagua Lissu na CHADEMA ili atupe katiba ambayo itakua backbone ya maendeleo ya nchi hii..

Hatuwezi kuwa tunaongozwa na mihemko ya mtu mmoja. Ambaye siku akiondoka atakuja mtu mwingine kutuongoza kwa mihemko tena.
 
Chagua Magufuli kwa Maendeleo yako na taifa lako.

But mpigie kura Lissu kuathiri maendeleo ya kizazi chako ,rasilimali zako, na Taifa lako kwa ujumla.
 
Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, kura za madiwani pamoja na kura za Wabunge na Rais baada ya kujumlishwa na kuandikwa katika fomu za matokeo, wasimamizi walizipeleka katani ili ziunganishwe na kupata matokeo ya jumla kwa kata husika. Baada ya hapo, nakala halisi za matokeo hayo zilipelekwa jimboni ili kuunganishwa na kupata jumla kwa jimbo huku nakala zingine wakipewa mawakala.

Ikumbukwe hapa ilikuwa ni rahisi kudhibiti ikiwa kutatokea nyongeza ya VITUO HEWA vya kupigia kura.

LAKINI MWAKA 2020;

Baada ya kura kuhesabiwa na kupata matokeo ya kituo husika,ni matokeo ya MADIWANI tu yatakayounganishwa katani lakini matokeo ya WABUNGE NA RAISI kwa kila kituo, HAYATAUNGANISHWA KATANI badala yake yatapelekwa jimboni kuunganishwa.

IMG_20201026_193517.jpg



TATIZO LINAWEZA KUTOKEA:
Tatizo hili linaweza kuwa kuongeza vituo hewa endapo mawakala hawatakuwa na orodha ya vituo vyote vya jimbo na ikiwa hawatakuwa makini wakati wa kujumlisha kura.

VYAMA VYOTE VYA SIASA, CHUKUA TAHADHARI.
Siamini kama kutakua na vituo hewa
Kwani jimboni ndio vyama vya siasa havijui kuna vituo vingapi kwenye jimbo husika?
Basi hivyo vyama vitakua vyakipuuzi sana kwamba visijue jimbo hili lina vituo vingapi.
Vyama vinajua nchi nzima kuna vituo vingapi na wana mawakala wangapi hivyo hewa vitaingiaje hapo.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ni katiba.
Hayo mengine uliyoandika ni ngonjera tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom