WATANZANIA HATUONI SABABU VIHELA AMBAVYO TUNAPEWA, MAGARI na NYUMBA

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Nyerere ameacha familia yake maskini hakuwa mjinga me ndhani bora nchi iongozwe na dictator, JAMANI tufanye nini ile yale yanayosemwa serikali haion,je watendaji wanogopa kukosa ajira, kukosa nyumba walizopewa au kujengewa na magari ya kifari, Je wakifa wataondoka nayo. Hii mijadala bora ipelekwe Kenya?? SOmaaaaaaaaa
1. labda wananchi hawajui ni kwa namna gani na kiasi gani ufisadi umezidisha
umasikini wao, kwa sasa na miaka mingi ijayo mbele?

2. labda sisi tunaojiita wanaharakati pia tumetekwa nyara kwa namna fulani,
tunafikiri tuna maisha mazuri yaliyotulia?

3. labda tunafikiri tukikosoa serikali yetu tutaonekana wapinzani - itikadi
iliyosimikwa vichwani mwetu kwamba kukosoa serikali ni kuwa mwanasiasa mpinzani na
hivyo ni sawa na kuwa mhaini?

4. pengine kila mmoja wetu anaogopa kuathirika binafsi kama akishiriki katika
vuguvugu - kupoteza kazi na kipato chake cha sasa hivi, kusitisha masomo,
kufungwa...

INAWEZEKANA NDIYO MAANA KAMILI YA AMANI NA UTULIVU

naomba mtu anithibitishie kwamba ninaota, nimepotoka

asanteni

Mr. Irenei Kiria
Executive Director
Youth Action Volunteers (YAV)
P. O. Box 12183
Dar es Salaam
Tel. 2666355/57
Fax 2668015
 
kaka nimependa pinti ya nne,wengi wetu ni waoga sana, kila mtu anamukumia mwenzie.uhahid upo lakini nani tumfunge kengele.watanzania wengi ni wazuri kuongea kama hv. lakini utekelezaji hakuna.serikari haina makali, walioko madarakani asilimia kubwa ni wezi, wanafiki, waongo, wababaishaji na waoga.
upuuzi mwingi sana viongozi wetu wanafanya. lakini kakak mi midhani tatizo kubwa ni kuwa nchi hii watu wake wamekata tamaa, wanapenda udaku na maneno yasiyo kuwa na tija kwa taifa. waliyedhani atawapa maisha bora kwa kila mtu amewaacha hawajui pa kushika, yeye mwenyewe hana nguvu kama mkuu wa nchi. ndio maana unaona hawa wezi wawili wakubwa (mengi na rostamu) wanaumbuana lkn hakuna kinachoendela. usalama wa taifa wa siku hizi bure kabisa na wengi ni ndugu wa wakubwa kule juu. maadili ya kazi hawana,siri za nchi ziko njenje!!
aahh inaudhi sana kaka hasa ninapomuona mkuu wetu wa nchi hotuba zake nyingi maneno yale ya:'tushirikiane, serikari inafanyia kazi, nk
 
jamani mijadala mikali ndo kwanza imeanza kuchomoza kwa kasi...tunapiga hatua pamoja na kasoro zetu nyingi za uwoga, unafiki, uvivu, uzembe na kutokuwajibika vema.

tuzidishe mapambano ya mijadala mikali ama kwa hakika tutavuka na kufikia utawala wa watu kwa ajili ya watu...

tahadhari tujiepushe na tupunguze sana kutumiwa kutokana na tamaa zetu za kupita kama fedha, magari na nyumba..tuwe watu wa kuamini katika uwajibikaji ili kupata riziki ya maisha..

THERE IS A WIND OF CHANGE COMING...
 
Wengi wetu ni watumwa wa ajira na hongo kwavile hatujui cha kufanya nje ya hivi. Kuna waafrika weusi wangapi wenye viwanda angalau hata vya kutengeneza miswaki?

Ndo maana Wahindi na Wachina wataendelea kuwa mabwana zetu.
 
Back
Top Bottom