tutamkumbukamagu
JF-Expert Member
- Jul 3, 2021
- 317
- 270
wasikuchanganyeBaada ya Hayati Rais JPM (R.I.P) watanzania waliopoteza mkate kipndi chake wameanza kutema nyongo, wengine wamefikia mahali na kusema kilichofanyika likuwa ni wizi. hivi kweli ndugu zangu watanzania kuna wakati nchi ilipigwa mchana km kipindi cha awamu ya 4? kuna kashfa ngapi ziliingiza nchi mpaka waziri mkuu Lowassa kuwajibika? tunakumbuka ufisadi wa RICHMOND, KAGODA, MEREMETA, MIKATABA YA MADINI, escrow account, tegeta escrow na nk.
Kuna watu wanahoji mikopo ya pesa nyingi kwa muda mfupi; hivi kuna ubaya gani ukikopa kufanya mambo makubwa kwa muda mfupi? au ni bora kukopa kidogo kwa muda mrefu? sijui watanzania tumerogwa na nani? siku moja nilikutuna na Prof mmoja bingwa wa mifupa akatuambia kuwa watanzania hatujui sekta ya afya ilivyokuwa taabani, lkn sasa vifaa tiba na wataalamu wamejaa, lkn aliongeza kuwa watanzania ni wapole sana. ni hiii kitu ndiyo inatufanya tuendelee kuwa maskini.
Tumesahau mambo makubwa aliyoifanyia nchi yetu tena kwa kipindi kifupi., mfano ni hii hapo chini.
HUDUMA ZA JAMII
NISHATI na MADINI.
- Kutoka asilimia 47% iliyokuwepo mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 69% katika kipindi cha mwaka 2019-2021.
- Kumboreka kwa huduma ya maji kutoka asilimia 47% mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 70.1%.
- Kupungua kwa gharama za kuvuta umeme kutoka 470,000/= mpaka 20,000/=
- Kufuta kabisa mgao wa umeme
- Kuanzaishwa kwa masoko ya ndani ya madini, ikumbukwe kuwa ukikamatwa na madini yanataifishwa na kifungo juu wakati hapakuwa na soko la madini hayo.
- Kupitiwa kwa mikataba ya ulaghai kwenye madini na gas na kupanda kwa mrahaba kutoka 3% mpaka 16%
ELIMU
- Elimu ya bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari na kufuta michango
- Kungozeka kwa wanaopata mikopo elimu ya juu
- Ukarabati shule zote kongwe za sekondari nchini.
AFYA
- Zahanati 1, 198
- Vituo vya Afya 497
- Hospitali za Wilaya ni 71
- Vifaa tib ana mitambo mikubwa ikumbukwe hapo nyuma machine kubwa km MRI na CT SCAN zilikuwa muhimbili na Aka Khan.
- Madakatari bingwa wote walihamia hospitali za watu binafsi.
MIUNDO MBINU
- Fly overs
- Bara bara kila kona ya nchi kama kule Ludewa, makete, Manyara, Kigoma, Tabora
- Upanuzi wa bandari ya Dar es salaam.
MAAMZI MAGUMU:
- kusimamia maamuzi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kuhamia Dodoma
- Ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere
- Ujenzi wa mradi mkubwa wa reli SGR
- Daraka kubwa la Busisi ziwa Victoria
- Kufufua shIrike la ndege sasa lina ndege kubwa km Dreamliner, airbus
- Mapambano ya wazi dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi
- Mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya
1.wengi wanaopiga kelele kama Nape, Membe n.k ni wale ambao mrija ulikatwa
2. wako ambao wanakubali chuki kwa bluetooth tu
nje ya mitandao,JPM anaishi