MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Hebu niulize swali mile;
Hivi kila jipu lazima Rais Magufuli atumbue? Yaani awaze wahisani,awaze ya Zanzibar,awaze hali ya usalama wa taifa kwa ujumla, awaze uchumi wa nchi,bado watumishi hewa, achilia mbali ya kwake binafsi! Hivi yeye kama binadamu mwenye damu kama wengine hachoki! Kuna mambo madogo hata barabara ya kijijini kwetu kule mwangeza lsanzu nao wanalalamika Magufuli aende kutumbua majipu, mjumbe wa mtaa wako kala pesa za wananchi ati Magufuli akatumbue jipu jamani??
Kwa system ya muundo wa utawala wa nchi hii hierachy ina utitiri wa viongozi kuanzia ngazi ya urais mpaka mwenyekiti wa kitongoji au mtendaji wa kijiji, hawa wote hawawezi kutumbua majipu? Ndani ya wilaya tu kuna mkuu wa wilaya, katibu tawala,mkurugenzi,Afisa utumishi, wanasiasa kama m/kiti wa halmashauri, mbunge na madiwani hawa wote wana kazi gani? Kwani kati yao hakuna wa kutumbua jipu mpaka Magufuli?
Itafika mahali mtagombana mume na mke ndani ya nyumba na kumuita Magufuli atumbue jibu.Tuache hii aibu,viongozi wa chini wafanye kazi zao sio kila kitu Rais.
Inawezekana kabisa huu mfumo tulionao wa utawala wenye utitiri wa viongozi hauna tija, ni dhahiri kabisa wanachi kudai kila jipu atumbue inamaana walio chini yake hawana kazi wanaongeza gharama za bure. Mzee warioba alishamaliza kila kitu kila tu kuna watu wameziba masikio.