Watanzania bado tunatawaliwa na mkoloni mweusi

Kazimzubwee

Member
Nov 7, 2016
51
57
Amani iwe nanyi,kutokana na tafiti nilizofanya tangu ujana wangu mpaka uzee huu nilionao nimegundua watanzania bado tunatawaliwa kimabavu na mkoloni mweusi ambae ni CCM.

Maana matendo ya CCM hayana tofauti na enzi zile za utumwa,kwa mfano kuminya uhuru wa habari, kuzuia matangazo ya bunge,kupiga marufuku mikutano ya kisiasi,kutokubali mawazo ya wengine,kutupa mchakato wa katiba mpya na mengine mengi yamenikumbusha enzi zile za ukoloni.

Kila nikitazama naona ukombozi haupo maana hakuna anaethubutu kupigania ukombozi wa kweli kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Maana ukiangalia ujangili umeshamiri na majagiri yanapewa dhamana na mahakama zetu za kisisiemu,maana watendaji ni wateule wa mwenyekiti wa CCM,Dhahabu inavunwa wachimbaji wadogo wananyanyaswa km wakimbizi Mzungu anakaribishwa aendelee kutonyonya.

Ktk elimu huku bora hata mkoloni watu walisoma bure leo hii tunanyanyasa wanaojiunga na elimu ya juu kwa kuwanyima hata mikopo,mtasema tuna uhuru?

Maovu yote serikali hii ya awamu ya tano inajinasibu kupambana nayo mwasisi wake ni CCM wenyewe,hii inadhihirisha hakuna msafi ndani ya ccm wote wameoza.

Namaliza kwa kuwaomba wenye upeo muwaelimishe wengine wajiandae kutafu uhuru wa pili kutoka kwa mkoloni mweusi CCM.
 
Mkuu nako kule upande wa pili yule sio agent wao..? maana kufika kilele cha mt kilimanjaro sio lazima utumie njia moja!
nikiwaangalia 3,4,5 n.k sioni nguvu yakupindua kwa sasa!
 
images.jpeg
 
Mabadiliko huanza na mtu mmoja mmoja....Na ni rahisi sana kushinda vita hii kama Elimu na ushawishi utamfikia kila mwananchi ambaye kiuhalisia ndiyo muhanga wa hali hii ngumu...Naona wakulu wameamua kwamakusudi kuzuia watu kupata Elimu na taarifa juu ya kinachoendelea ndiyo maana wakaja na kauli mbio ya SIASA MPAKA 2020...
 
Back
Top Bottom