Watanzania 600 kupata ajira katika ujenzi wa mgodi Ruangwa, mkoani Lindi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Stanslaus Haroon Nyongo,amesema watanzania zaidi ya mia 600, wanatarajia kupata ajira katika kipindi cha mwanzo wa ujenzi wa mgodi wa kampuni ya Uranex inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya bunyu katika wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo,wilayani Ruangwa,mkoani Lindi,baada ya kutembelea eneo utakapojengwa mgodi huo huku akieleza kuwa kampuni hiyo ya kigeni tayari imeshafanya utafiti wa kutosha na imeshapata leseni ya uchimbaji lakini kutokana na mabadiliko ya sheria pamoja na kanuni zake sasa wanasubiri kanuni ziwe tayari ili waweze kuanza shughuli za uchimbaji mara moja na wananchi wapate kunufaika.

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa madini kanda ya Kusini,Mayigi makolobela, akawataka wawekezaji hao kuwa na mahusiano ya karibu na wananchi wanaozunguka mgodi huo.


ITV
 
Ingekuwa zama za JK hawa jamaa wangekuwa wameshaanza uzarishaji, maana utafiti walianza siku nyingi sana..
Sheria mpya zinaleta shida, kutafuta wawekezaji na wakakubali kuja kuwekeza ni kazi kubwa zana kuliko tufikiliavyo.
 
Back
Top Bottom