Watanzania 27 wajeruhiwa kwenye ajali nchini Uganda

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429
Watanzania 27 wamejeruhiwa katika ajali ya basi kampuni ya Falcon walilokuwa wakisafiria kuelekea kutokea Tanzania kuelekea Uganda, baada ya kuangukia upande wa kushoto njia kuu ya Masaka, Uganda.

Abiria hao walikuwa njiani kuelekea Namugongo katika sherehe za siku ya Martyrs ambayo ahudhimisha na waumini wa Kanisa Katoliki kote duniani kila ifikapo Juni 3. Polisi nchini Uganda wanasema basi hilo lenye usajili namba T967-BTA lilishindwa kupanda mlima iliyopo kati ya eneo la Kyatera na Masaka baada ya breki ya gari hizo kufeli na kusababisha ajali.

Hata hivyo polisi hao wamesema hakuna majeruhi walio kwenye hali mbaya. Miongoni mwa waliojeruhiwa ni Maria Ngonyari, Robert Imman (40), Alex Rono (64), Angela Kigulwe Biringi (65), Gloria Mwisa (29), Emiyana Babweiga (65) na Julliet Arshdes (40).

Kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani nchini, Mohamed Mpinga amesema ni kweli ajali hiyo imetokea na kwamba majeruhi wapo katika hali nzuri. “Majeruhi walitibiwa na kisha kuendelea na safari hakuna aliyeumia sana,” amesema Mpinga
index.jpeg
 
Muujiza huo wa kuponywa kifo uwaimarishe ktk safari yenu ya hija huko namugongo kunako madhabahu ya Mashahidi wa imani na mapendo kwa Kristo na Kanisa lake
 
Pole zao. Kazi ya imani, Mungu awajalie waweze kupona kwa uharaka
 
Watanzania 27 wamejeruhiwa katika ajali ya basi kampuni ya Falcon walilokuwa wakisafiria kuelekea kutokea Tanzania kuelekea Uganda, baada ya kuangukia upande wa kushoto njia kuu ya Masaka, Uganda.

Abiria hao walikuwa njiani kuelekea Namugongo katika sherehe za siku ya Martyrs ambayo ahudhimisha na waumini wa Kanisa Katoliki kote duniani kila ifikapo Juni 3. Polisi nchini Uganda wanasema basi hilo lenye usajili namba T967-BTA lilishindwa kupanda mlima iliyopo kati ya eneo la Kyatera na Masaka baada ya breki ya gari hizo kufeli na kusababisha ajali.

Hata hivyo polisi hao wamesema hakuna majeruhi walio kwenye hali mbaya. Miongoni mwa waliojeruhiwa ni Maria Ngonyari, Robert Imman (40), Alex Rono (64), Angela Kigulwe Biringi (65), Gloria Mwisa (29), Emiyana Babweiga (65) na Julliet Arshdes (40).

Kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani nchini, Mohamed Mpinga amesema ni kweli ajali hiyo imetokea na kwamba majeruhi wapo katika hali nzuri. “Majeruhi walitibiwa na kisha kuendelea na safari hakuna aliyeumia sana,” amesema Mpinga
View attachment 516693
Mkuu sio Kyatera ni Kyotera.
 
Back
Top Bottom