Watanzani wengi wamechakachuliwa

Zhu

Senior Member
Sep 26, 2010
184
0
Katika kufuatilia mambo mbalimbali yanavyoendelea hapa nchini nimegundua kuwa wananchi wengi wanapata habari zisizo sahihi. Unaanza shule kwa kudanganya umri. Unakwenda sekondari kwa kuiba mtihani. Unakwenda chuo kikuu kwa kuiba mtihani. Unapata digrii kwa kuhonga profesa. Unapata kazi kwa rushwa. Utafanya kazi kumfurahisha aliyekuajiri kwa rushwa. Unataraji nini kwa watu kama hawa ambao niwengi. Ukianza na waandishi wa habari. Ukiona habari live kwa Tv na habari ya gazeti tofauti. Habari nzima inachakachuliwa. Je tutafika.
 

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,205
0
Inasikitisha ila ndipo tulipo sasa na ukizoea tabia fulani ni vigumu kuiacha tupende tusipende Tanzania ishakuwa nchi ya wachakachuaji..... kama vile watu wanavyoisema Nigeria ni nchi ya matapeli
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,095
2,000
Zhu ni nyinyi generation ya sasa ndiyo wenye matatizo hayo. Enzi yetu hatukuwa na wazo la kununua mitihani ya sekondari au high school, chuo kikuu tulikuwa tunajiunga kwa qualifications zetu na degree tulikuwa tunapata kihalali kabisa. Ukifeli ulikuwa unakwenda na maji hata kama uko mwaka wa mwisho.
 

Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,532
2,000
We have been brainwashed that we have allowed someone to think on or behalf!
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,979
2,000
Katika kufuatilia mambo mbalimbali yanavyoendelea hapa nchini nimegundua kuwa wananchi wengi wanapata habari zisizo sahihi. Unaanza shule kwa kudanganya umri. Unakwenda sekondari kwa kuiba mtihani. Unakwenda chuo kikuu kwa kuiba mtihani. Unapata digrii kwa kuhonga profesa. Unapata kazi kwa rushwa. Utafanya kazi kumfurahisha aliyekuajiri kwa rushwa. Unataraji nini kwa watu kama hawa ambao niwengi. Ukianza na waandishi wa habari. Ukiona habari live kwa Tv na habari ya gazeti tofauti. Habari nzima inachakachuliwa. Je tutafika.Mambo ya Examination techniques
 

nyondoloja

Senior Member
Nov 10, 2010
190
225
tuko pabaya unashangahayo watu wanajichakachuwa hadi afya zao anaandikiwa dawa nadakitali doz ananunuwa nusu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom