Watanzani Sir tuna Matatizo

Mwanagandila

Senior Member
Oct 9, 2011
182
100
Watanzania tunaongoza kwa kupenda kulalamika bila kutoa suluhisho mbadala kwa jambo lenyewe.
Mara anarudi usiku tutaendaje kumpokea hao waliorudi mchana lini uliwahi kwenda kuwapokea?

Mara wazazi wake wamekaa kwenye ngazi kwani mliambiwa uwanja wa ndege una waiting Lounge kwa ajili ya wanaowasili?

Ohoo wangeoganaizi VIP hayo mawazo mlikua wapi kuyatoa tangu awali?

Mara figisu za CAF kumleta usiku, sasa wasifanye figisu kumnyima tuzo wafanye figisu kumleta usiku?

Mara Nape hakwenda kumpokea angeenda si ndo nyie mngesema yaani waziri anaacha mambo ya maana anaenda kukesha airport.

Eti mnataka wafanye kama alivofanya Omary Bongo, ile ni Gabon hii ni Tz angeenda Magu uwanjani si mngeongea mpaka mpasuke nyie?

Maana Kikwete alivyokua anatoa sapoti tulikua tunamuona hafai anaacha kuongoza nchi anaangaika na sanaa na michezo, jamani ebu mara moja moja muache lawama zisizo na tija.
 
Wanabongo kama za kalunguyeye,hapo ndo nafikiria Mara mbili kumkosoa Donald Trump.mtu anakutukana unaroho mbaya halafu dakika tano baadaye anakuomba pesa ya vitafunwa.hizo ndo akili za wabongo wengi.
 
Wanabongo kama za kalunguyeye,hapo ndo nafikiria Mara mbili kumkosoa Donald Trump.mtu anakutukana unaroho mbaya halafu dakika tano baadaye anakuomba pesa ya vitafunwa.hizo ndo akili za wabongo wengi.
mkuu nimecheka sana. Sisi wabongo bana
 
Hiki kizazi cha walalamishi kilianza kuchipuka wakati wa utawala wa Rais Ben Mkapa. Tuliokuwa watu wazima wakati ule tunajua kuwa Mhe. alikuwa akiwalaumu sana hao watu, ukiwa mlalamishi kamwe huwezi kuwa na busara ya kutafuta suluhisho au kuwa na uwezo wa kutoa mwelekeo wa mambo.
Naona kuna multiplier effect kubwa ndani ya miaka hii kumi iliyopita. Wapumbavu wengi wamepata balehe katika kipindi hiki na kutumbukia katika janga la kuwa watu wa kulaumu tu.

Nashauri ni bora ukawa mkosoaji maana unaonyesha njia mbadala na kulinganisha na njia aliyopita unayemkosoa. Mlalamishi huwa hana akili za kufikiria.
 
Back
Top Bottom