Watanzani,hivi tumekubali jamii yetu iharibiwe kabisa kimaadili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzani,hivi tumekubali jamii yetu iharibiwe kabisa kimaadili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Dec 23, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi nauliza,nauliza kwa sababu sielewi mwenzenu,yaani sielewi kabisaaaaaaa.Hivi kwa nini tunanyamaza kimya huku maadili ya jamii yetu yanazidi kuharibiwa na watu wachache,tena wageni wenye ajenda zao za ziri?Hivi kwa nini lakini.Jamani tumepigwa ganzi na nani? Hivi tumekubali kabisa watoto wetu wafolenishwe hadharani na vichupi kwa visingizio vya biashara.Biashara gani hizi uchwara ambazo lazima watu watembee uchi ndio zifanyike.Jamani hivi tumekubali kabisa matendo yanayoashiria ngono yaonyeshwe hadharani kabisa kwenye haya wanayoita makongamano.Hatuoni kwamba huku ni kuhamasisha ngono na kutudhalilisha?Jamani unapiga vita ukimwi huku unahamasisha ngono,ni ujinga gani huu!Watanzania wenzangu nani ametulaza usingizi mnene kiasi hiki?Mbona hatunyanyuki na kukemea ujinga huu na kusema sasa basi.Wazazi mko wapi?Mmekubali watoto wenu wafanywe mataahira mbele yenu kabisa, lakini mkoje?Mbona hamuamki mkaihoji na kuiwajibisha serikali katika hili.Poleni sana ndugu zangu,mtakapo zinduka mtakuwa mmechelewa sana, wenzenu watakuwa wameshamaliza kazi.Amkeni basi katika usingizi wenu mnene mkaliepushe taifa hili na maangamizi ya kutisha yanayo linyemelea taifa letu.Watumishi wa maruhani, wanasema kukaa uchi ni mila yetu.Hawa ni watu waliopotoshwa kabisa kimaadili na maruhani.Wamepofushwa fahamu zao wasijue kwamba katika bustani ya Eden baada ya dhambi kuingia,Mungu mwenyewe aliwavalisha Adam na Hawa mavazi.Wanasahau pia kwamba nyakati ambazo watu walikuwa hawavai nguo,Mungu aliziita nyakati za ujinga,na kwamba Mungu anasema alijifanya hazioni!Lakini sasa anataka watu waenende inavyowapasa.Wanasahau pia kwamba sasa Mungu ameamuru watu wote wavae mavazi ya kujisetiri.Wazazi wenzangu,watanzania wenzangu, tusidanganyike na mafundisho ya mashetani ambayo sasa yamesambaa kila mahali kwa nia ya kutupotosha kabisa.Kwa nia mbaya kabisa maruhani na vikaragosi vyao wanatumia kila njia kulipotosha taifa letu.Tusimame imara na kusema hapana na ujinga wao sasa basi.
   
 2. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2008
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tikerra, kwanza pongezi,jambo hili la kuacha maadili yapotee si jambo la kufanyiwa MAS IHARA na kupuuzwa. Nakumbuka ndani ya muongo wa 1960s lilipita zoezi la kuhakikisha watu wanavaa kwa adabu, sisemi turudi huko lakini na kuacha mambo yende kama yalivyo pia si sawa. Labda niulize ule umoja wa kina mama wa Tanzania UWT bado upo??? Nadhani wao wangekuwa wazuri klishikia bango swala hili. wapange sera inayoelewea waifikishe Bungeni ili sheria itungwe na idhibiti biashara hii isiyopendeza.
   
 3. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Njia rahisi sana ya kupambana na vitu vinavyokukera lakini vimekubalika kwenye jamiii si kukemea, bali ni kuachana navyo. Wewe kama wanaonyesha kwneye TV usiangalie hiyo time wanapoonyeshwa na wala magazeti ya udaku usinunue. Nyumbani kwako elimisha familia yako. Ingawaj familia yako ita-interact directly na vitu hivi unavyopinga, lakini ukiwalewesha vema kimaadili, watajiepusha.

  Itakuwa jambo la ajabu sana na ndivyo-sivyo kupambana na mambo ambayo yako ulimwenguni kote na yanakubalika!
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Hii ni taking the bitter with the sweet ya utandawazi. Zanzibar walipofungua milango ya utalii kwa kuzifanya pwani zake ni maeneo huru ya uwekezaji sekta ya mahoteli. Wakaja wataliono kujenga mahoteli naa ufuska juu yake. Zaanzibar wakajidai wanaofanya sio dada zao bali ni kutoka bara. Leo biashara imechanganyia booking kwa makatalogi tena mabikra wa kizenj kukuwadiwa kwa dau kubwa mpaka sasa kuna mpaka biashara ya kutengeneza hizo bikra na wataalamu ni Wanzanzibari wenyewe.

  Kwani kabla ya ujio wa wageni sisi kwa asili tulivaa nini?. Amini usiamini hivyo vimini ni afadhali!. Ni ukweli usiofichika kuwa maendeleo yanayoletwa na utandawazi yanaharibu maadili ya jamii yetu. Siye tulichezea manati wakina dada michezo ya kujipikilisha na maramoja moja katika mchezo wa kujificha tulicheza mchezo wa baba na mama na nguo zetu. Leo watoto etu wanaona live kwenye tv, midoli ya umeme na manati za play station na PSP.
  Its now too late only ever forward, backward never kuelekea utandawazi kamili ambapo wazazi wataanzia sebleni kwenye kochi eti chumbani mbali!.
   
 5. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Jujuman
  Hao unaowaulizia wao wamevua nguo za ndani siku nyingi, wanazibeba kwenye pochi zao kwa ajili ya maonesho. Umesahau kisa cha Mhe viti maalum Mbeya? Matusi ya Sophia Simba je? Tufikiri mengine, UWT ya CCM si chombo cha kutegemea kutupa mwongozo wa maana.
   
Loading...