zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Salama Mrisho wa Star TV ameleta habari sasa hivi za mauaji ya Raia 5 waliouliwa kinyama na magaidi bila ya hatia.
Magaidi watatu wanashikilwa na Polisi hadi sasa kwa tukio hilo.
Watanzania tuungane tuutokomeze ugaidi, wanatumalizia raia zetu wema hawa magaidi.
=====================
UHALISIA WA KILICHOTOKEA:
Magaidi watatu wanashikilwa na Polisi hadi sasa kwa tukio hilo.
Watanzania tuungane tuutokomeze ugaidi, wanatumalizia raia zetu wema hawa magaidi.
=====================
UHALISIA WA KILICHOTOKEA:
Mods huwa hawapotoshi, wako hapa kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kiko sawa humu jukwaani!
Wanaweza ku-verify mahali husika na kuweka sawa kama jambo halieleweki vizuri na mleta mada kama hili lako!
Lakini pia sisi wanachama wa JF tunaruhusiwa kufuatilia jambo na kuwaeleza mods kama unaweza kufanya hivyo kama kuna utata!
Sasa ngoja tukusaidie hili jambo vizuri:
Kwanza hakuna gaidi aliyeua, wala aliyeuawa!
Pili Watu waliouawa ni watano na ni vibaka ambao jana walikwenda kuvamia msibani na kukwapua sahani iliyokuwa na fedha za rambirambi shilingi 67,000 na wakaondoka nazo!
Tatu baada ya kuondoka uongozi wa Sungusungu wa katika kijiji hicho walianza msako na kubahatika kumpata mmoja wao ambaye baada ya kumhoji alikiri na kuwataja wenzake wanne!
Baada ya kuwataja wakakamatwa na sungusungu,wakati wanaendelea kuhojiwa wananchi wakapata taarifa wakawafuata wakaanza kuwasahambulia kwa mawe na silaha zingine za jadi!
Mmoja alivunjwa miguu yote mwiwili,waliotambuliwa majina ni wawili,mmoja ametambuliwa kwa jina moja na wengine bado hawajatambuliwa jina hata moja!
Hao ni vibaka,wawili waliotambuliwa majina nimMarwa Chacha, Shija Mlingwa, Ezekiel, wakazi wa Nyantorotoro wawili hawajafahamika.
Polisi wanawashikilia watu watatu akiwemo wa kiongozi mmoja wa sungusungu,wanaume wote wamekimbia familia zao kwa hofu ya kukamatwa.
Haya ni maelezo kamili niliyoyapata kutoka kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Leonard Paul katika mahojiano kati yangu na yeye kwa njia ya simu!
Mtoa mada alitaka tu kupamba habari ili ipate sapoti ya wana JF!
Kwa hiyo mods mnaweza kubadili kichwa cha habari vyovyote vile kulingana na hayo maelezo niliyowapa hapo juu,tusipende kuwapa watu presha huu ni mwisho wa mwaka.