K A B U R U
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 818
- 1,067
Jana nilikuwa natazama taarifa ya habari saa moja usiku kupitia kituo cha luninga cha Channel Ten, nilipata ukakasi baada ya kumsikiliza mtangazaji wa habari za kimataifa akipata taabu kutamka mji wa Munich
Hili alilitaja kimakosa kama mara nne mpaka nikajiuliza ina maana hajawahi hata kulisikia neno hili kabla, ili ajisahihishe?
Leo ninasikiliza Radio Free Africa kipindi cha Watanzania Tuzungumze magazeti, mtangazaji ameanza na gazeti la Nipashe anatamka chama cha wanasheria Tanganyika kama TLC badala ya TLS. Amerudia tena kutamka TLC akipitia gazeti la Mtanzania.
MY TAKE:
Huwezi kujua kutamka maneno yote hasa yale ya lugha za kigeni kama kijerumani na kifaransa, lakini kama mtangazaji ni vizuri ukajiridhisha kama sehemu ya maandalizi ya kipindi jinsi ya kutamka maneno yaliyopo kwenye kipindi chako.
Tuweze kuwa mazoea ya kuwa na uwanja mpana wa ufahamu wa mambo yanayotuzunguka katika taaluma zetu, mfano mtangazaji wa taarifa za habari ni vema akawa mfuatiliaji wa habari mbalimbali zinazotangazwa na vyombo vingine hasa vya kimataifa badala ya kujikita kuchonga sauti peke yake.
The content is what matters the most.